sundoka
JF-Expert Member
- Oct 9, 2011
- 2,067
- 2,757
Habari za mida wadau,
Leo katika pitapita zangu huku kijijini nikakuta mahali AMREF wameweka mahema yao wanatoa huduma za kupima magonjwa kama HIV, TB, Cancer, tezi dume, n.k bure.
Kwa kuwa nlikiwa napanga several times kwenda mjini kupima ngoma nikaona bora nimalizie shida yangu ya kupima pale.
Sasa baada ya kutolewa damu nikaambiwa nisubiri nje kama dk. 5 then nitakuta majibu yako tayari.
Wakati nipo pale nje akatokea kijana mmoja mle ndani tayari amepima na kapewa kadi yake tayari na nikaona nyuma imeandikwa HIV neg na ameandikiwa tar ya kurud kupima tena. Nikamuuliza aliingia ndani pale muda gani akaniambia asa hivi tu na aliniona natoka mimi ndo akaingia.
Baada ya dakika 6 nikaenda tena ndani kwenye hema kufata majibu lakini hapo nishaanza kuwa na wasiwasi nikaanza kujiuliza kwa nini mimi nimeambiwa nisubiri dakika 5 wakati huyu bwa mdogo hakuchukua hata dk 3 katoka na majibu???
Nilipofika ndani yule mama mpimaji akaniambia majibu yangu ni mazuri sina maambukizi ya UKIMWI. Akanipa hii kadi
Baada ya kuona hii kadi moyo wangu uliripuka kidogo. Kila nikipima sijawahi kuandikiwa hivi "Non Reactive" sasa iweje leo?? Nikatoka nikiwa na maswali mengi na nikiamini kuna kitu cha ziada hapa. Sababu zinazonifanya niwe na mashaka labda huyu mama ananificha kitu ni hizi:
1. Kitendo cha kunisubirisha mimi nje muda mrefu wakat kuna mwingine amewahishwa (nahisi alikuwa anapanga anitoke vipi)
2. Kitendo cha yule mama kutaka kuninyima ile kadi yenye majibu. Baada ya kuniambia sijaathirika nilinyoosha mkono kuchukua ile kadi akaniambia hata nisipoichukua ile kadi niende zangu tu home niendelee na ishu zangu akiniambia eti ile kadi anapewa aliyeathirika ili aendelee kupima TB. Nikamwambia nataka nipime na TB maana huwa nina tendency ya kubanja sana sana nikiamka usingizini akajaribu kunidiscourage lakini nikakaza hadi akanipa ndo nikaondoka zangu.
Wakuu naombeni mniondolee utata hapa. Neno HIV Non Reactive lina maana gani katika HIV testing??
Mbarikiwe zana