Nilikuta Mke wangu kapima Afya bila kunishirikisha, Hongera kwake kwa kujitambua

NJOGHOMILE

JF-Expert Member
Jun 11, 2017
657
1,868
Nimekuwa nikisafiri mara kwa mara mikoani kikazi kwani nature ya kazi inahitaji kusafiri ili kutekeleza majukumu.

Nipo kwenye ndoa kwa muda mwa miaka 5 hadi sasa na tumejaliwa kupata mtoto mmoja.

Sijawahi kuchepuka hata siku moja na sitarajii kufikiria kuchepuka kwani nimeridhika na maamuzi niliyochukua(ya kuoa) ili kujisitiri na mabalaa yanayoweza kutokana na kuchepuka.

Lakini mwenzangu anahisi kutoniamini kutokana na kusafiri mara kwa mara japo ni haki yake kutoniamini. Mimi hata sijisumbui sana kumtilia shaka yeye kwani kumchunga mtu mwenye akili timamu ni kupoteza muda ukizingatia nikisafiri namuacha nyumbani.

Ila kilichonishangaza, kuna siku nilikuta karatasi ya majibu ya vipimo vya HIV imezagaa ndani sakafuni. Niliikota na kuisoma maana nilifikiri labda mtoto alichukua karatasi kwenye sehemu ninapowekaga karatasi zangu ambazo nilikuwa nafanyia kazi na kuanza kuchezea.

Nilipoifungua ndipo nikakuta ni majibu ya Maabara ya kipimo cha HIV na aliyepimwa ni wife, majibu yalikuwa negative. Nilipoangalia tarehe ya kipimo, nikakuta ni siku ambayo sikuwepo nyumbani, nilikuwa nimesafiri kikazi.

Baada ya hapo nililiacha hilo karatasi pale pale na kujifanya kama sijaliona na sikumuuliza ila baadae nilikuta nilishatolewa.

Kwa kuwa anaweza kupima kwa nia njema kucheki kama sijamuunga kwenye gridi kwani ninaposafiri anahisi naweza kurudi na connector ya gridi mimi nimebaki sina hofu yeyote siwezi kumuuliza. Hata akiniambia tukapime kama tulivyowahi kupima siku tulipoenda Clinic akiwa mjamzito, siwezi kukataa maana najijua.

Haya mabaharia karibuni mserereke hapa kulingana na hizi indicators niendelee kula maisha bila stress au nichukue tahadhari maana mimi naweza kuwa napambana na uaminifu kumbe mwenzangu anakula maisha kiaina yake.

NB: Alishawahi kuniambia nisimsaliti pindi nikiwa sipo, nilimjibu kuwa "kama ningekuwa nataka kula bata/ujana nisingekimbilia kuoa mapema, sasa nafurahia ndoa yangu labda wewe unisaliti"
 
Ingia Kichwa Kichwa hivyo hivyo Kama yeye Hakuamini Adi anaenda kupima Wewe Una😅😂😅Utavuna Mabua
 
Back
Top Bottom