Msaada hapa nifanyeje? Nilinunua gari wakasema limepata ajali naombeni ushauri

eity 4

Senior Member
Dec 7, 2014
147
206
Mimi nilikuwa nataka kununua Gari, kutokana na kutokuwa mzoefu na mambo ya magari na hii ni mara yangu ya kwanza kununua gari nikaamua kumtumia ndugu yangu ambae ana gereji yake nikiamini angenisaidia kupata chaguo zuri. Basi akanitumia picha nyingi tu za magari mwishowe akanishauri kununua gari fulani kwamba mi lingenifaa. Basi akataka nimtumie ela yeye ndiyo alipe kwa mwenye gari. Nikaenda bank nikamuwekea pesa.

Baadae akaniambia ana kijana wake anaweza kunisafirishia gari kuniletea mkoa ninao kaa. Kwa hiyo nikatoa hela ya kumlipa msafirishaji pamoja na hela ya mafuta. Gari imenunuliwa Mtwara Masasi mi nakaa Mpanda Katavi. Wakaenda dereva na dalali ( maana dalali aliyepewa kazi ya kuuza ni wa Dar)Nikapewa taarifa kuwa gari tayari imenunuliwa kwa hiyo wanaanza safari kuniletea.

Mi nikawaambia kwa kuwa wapo masasi na wanakuja Mpanda basi wapite njia ya songea makambako mbeya mpaka Mpanda, wao wakang'ang'nia kipitia Dar then Moro Mbeya mpaka Mpanda. Dalali ndiyo akawa anaendesha gari na siyo dereva niliyemlipa kufanya kazi hiyo.Kufika mtwara wakapakia abiria wawili. Njiani gari lilmepata ajali. Yaani lipo nyang'anyang'a. Baada ya ajali wakanipigia simu gari limepata ajali na kwamba wamewaacha watu kulilinda wao wameenda hospitali.

Nimefunga safari mpaka eneo la tukio. Sasa niliyoyakuta ni yafuatayo: (1) document zina jina la mmiliki wa awali (siye aliyeuza, yaani alipolinunua hakufanya transfer).(2) Hakuna mkataba wowote unaoonyesha muuzaji kapokea pesa kwa ajili ya kuuza gari japo kawapa kadi orijino na document nyingine za gari na kopi ya kitambulisho chake. Yaani hakuna karatasi inayoonyesha mimi au huyo ndugu yangu amelipa fedha kununua hiyo gari.

Document nimezikuta polisi ambao walikuta zimetelekezwa ndani ya gari.(3) Baada ya kufuatilia huyu dalali na dereva hawakuumia kwenye ajali. Sasa gari ipo porini ambapo kuilindabkwa usiku mmoja ni 40000.huyu ndugu yangu ananiambia niibebe gari niipeleke gereji kwake iringa. Wajuzi wa magari wkiiona gari wananiambia nisihangaike kuitengeneza yaani haiwezi kutengenezeka.

Msaada ndugu zangu hapa nafanyaje
 
eity 4,
Lakini kama ina bima kubwa mwambie mwenye gari akusaidie kiubinadamu zaidi ya hapo mtasumbuana na huyo ndugu yako. Bima ukifanya transfer tu mkataba wake umeisha.

Lakini kwanini umemuamini sana ndugu yako gari yako ya kwanza hukuwa na kihoro cha kutaka kuiona?

Kama ukitumia utamaduni usioshikika unaweza kuwa na matokeo mazuri zaidi kama mmabo yakigoma maana watu wa Mpanda upo vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole hapo naona ukienda kutofautiana na jamaa yako...urafiki undugu uko mashakani...ila utauokoa ukisamehe saba mara sabini

"corona ipo tuchukue tahadhari"
 
Sema umeficha detailz
Gari gani
Imepata ajali wapi na shm gani kuna watu tupo mikoa ya kusini tungekusaidia zaidi.

Umenunua kiasi gani ili tujue thaman ya gari na undugu

Picha ili kuona linaweza tengenezeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama ambavyo ww umeficha baadhi ya mambo ndio sababu ya nduguyo pia kuficha mkataba wa mauziano.. ww funguka gari aina gani ulimtumia bei gani wadau watakwambia ukweli ikiwezekana weka na picha za gari hapa..

kingine sio kila anayeweza kuendesha gari basi anaweza endesha masafa marefu kama huyo dereva wako umesema kabisa ni dalali wa dar kazoea kupiga misele mjini tuu na sio kuendesha gari mkoa to mkoa safari ndefu hawezi yawezekana uzoeafu ndio sababu
 
Rahisisha maelezo,gari aina gani,ya mwaka gani,wameuziwa bei gani?
Kuna wadau humu watakusaidia kupata pa kuanzia
 
Back
Top Bottom