Naomba ushauri nataka kununua gari

mwendapole12

Member
Apr 2, 2022
21
26
Wakuu habari zane nimeleta uzi huu mnifumbue macho kwa hili nisije kuingia mkenge,

Nataka kununua gari maana nimeendesha pikipiki kwa muda mrefu sasa imetosha bwana naomba.

Ninatazamia kununua gari IST au Vitz mkononi ila changamoto inayokuja nakosa amani na madalali kwani wao wengi unakuta tayari wana document ila la kipengele mawasiliano ya mmiliki wa kwenye kadi hawana.

Nami napata ofu nadhani mtu anaweza kuweka gari bondi akakopa mwisho wasiku akachelewa kulipa fari ikauzwa au mtu akachukua doc za nduguye akaamua kuuza.

Gari sasa nifanyeje ili niweze kununua gari kwa dalali maana magari ni mengi.

Je hayo magari yote yanayouzwa na mdarali wanaoenda kuyatumia wanafanyeje ikifika wakati wa kufanya transfer ofu ownership?
 
Kwenye ownership transfer lazima uwe na kopi ya NIDA ya mmliki (jina kama linavyooneshwa kwenye kadi) picha yake passport size na pia lazima Ofisa wa TRA atampigia simu mmiliki wa gari kupata ridhaa yake ya kubadilisha umiliki.
 
Wewe nunua tu, hayo unayoyatilia shaka ndio yakague uthibitishe ndipo utoe pesa

By the way unabajeti ya shiling ngapi na umeitoa wapi
 
Mmmh.

Nunua ya mkononi ikiwa una mjua muhusika. Kusanya taarifa za kutosha na mmiliki ikiwezekana akupatie aliyenunua kwake uthibitishe. Ni suala la uhakika
 
Kua makini tu. Jambo la msingi tafta fundi ambaye kidogo unamwamini. Na pia tafta elimu kidogo ya magari....mfano kutambua gari lililopata ajari, kuangalia gear box , na engine na body kama zipo vizuri...just basic. Pia usiwe na haraka sana. Unaweza kupata kwa mmiliki kabisa kwani kwa gari hizo wengi wanazo na wanauza
 
Mkuu big up kwa kupiga hatua moja mbele katika maisha..
Kuwa makini,madalali ni pasua kichwa sana,gari mwenyewe anataka m6,wao wanaanzia hata m9,unashangaa gari moja ina madalali hata 6,kila mtu na bei yake.
Kuna gari,madalali toptop ilikuwa m7.5 hawapunguzi,na ni namba B,lakini kwa njia ya ajabu,tukanunua kwa muhusika kwa m5.7..
 
Ukitulia ukaweka pupa pembeni ,,basi nakubashiria utapata gari nzuri na utakaa nayo sana ,, mimi nakumbuka wakat naingia kwa mara ya kwanza ulimwengu wa magari ,nilinunua Toyota sienta ,,kwa mzee mmoja wa kichaga,,aisee nilijuta kwann nilinunua gari ,maana sikumbuka kama nishawahi kupata furaha wakati nipo na gari lile ,,kwanza ilikuw na ugonjwa wa kupoteza nguvu ukipanda mlima ,,alaf punde likawa linaleta taa ya check ingine...basi sikukaa nalo sana nikamrudishia mwenyew gari lake nikamwambia natak pesa zangu ,, ilikuwa kuna mvutano kwenye kurudisha pesa ila kilichonisaidia nina mkoba wa uganga wa bi.mkubwa ,,basi nilimpa mwezi mmoja yule mzee atafute pesa aniletee ,,nilichokifanya nikaenda mzimuni kushtakia ,,ebwana yule mzee aliandamwa na mabalaa ,anajua yeye na mungu wake ,,mwisho wa siku akanipigia akanambia kijana nakulipa pesa zako ..basi nikampa account numbee yangu akaingiza mpunga wangu wote ,,, Hapo akili ikanikaa sawa ,,ikabidi nivute pumzi ,,nikaanza kutafuta gari taratibu hadi nikapata Gari nzuri aina ya toyota Alphard Ambayo mpaka sasa nipo nayo na nashkuru Haijawahi kunisumbua ..
 
MAliza mtihan wako wa kidato cha
4 huwenda sometime ukawa serious na post za watu
 
Wakuu habari zane nimeleta uzi huu mnifumbue macho kwa hili nisije kuingia mkenge,

Nataka kununua gari maana nimeendesha pikipiki kwa muda mrefu sasa imetosha bwana naomba.

Ninatazamia kununua gari IST au Vitz mkononi ila changamoto inayokuja nakosa amani na madalali kwani wao wengi unakuta tayari wana document ila la kipengele mawasiliano ya mmiliki wa kwenye kadi hawana.

Nami napata ofu nadhani mtu anaweza kuweka gari bondi akakopa mwisho wasiku akachelewa kulipa fari ikauzwa au mtu akachukua doc za nduguye akaamua kuuza.

Gari sasa nifanyeje ili niweze kununua gari kwa dalali maana magari ni mengi.

Je hayo magari yote yanayouzwa na mdarali wanaoenda kuyatumia wanafanyeje ikifika wakati wa kufanya transfer ofu ownership?
Ukishlipenda gari kupitia dalali nenda na mmiliki TRA ukajue ABC zake kuanzia umiliki halali, umiliki mara ngapi na mikopo kwenye taasisi za fedha pamoja na uhalali wa nyaraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye ownership transfer lazima uwe na kopi ya NIDA ya mmliki (jina kama linavyooneshwa kwenye kadi) picha yake passport size na pia lazima Ofisa wa TRA atampigia simu mmiliki wa gari kupata ridhaa yake ya kubadilisha umiliki.
Hapa si TRA wataleta pua zao kutaka Kodi.
 
Back
Top Bottom