MSAADA:GUEST/HOTEL NZURI MOROGORO

MSAADA:GUEST/HOTEL NZURI MOROGORO

Kwa bajeti hiyo na anataka iwe karibu na hapo anapofanyia kikao sio rahis..
Aongezee.. kuna jiran hapo HILUX hotel 50k.kuna Oasis Hotel 60k..
Mkuu nashukuru kwa hili wazo.Binafsi si mgeni sana moro ila si mwenyeji nilimgusia Hilux nafaham ni jirani lakini sister ni bahili ameigomea..Ngoja tuendelee kuangalia tutaona itakuwaje.Thanx.
 
kombuna lodge! ipo vzr sana ipo mitaa ya misufin apo atapata chakula na malazi fresh, na nauli ya boda boda toka apo kombuna mpaka social ni 1000 tu,tena pk pk zipo apo apo! zingatia ilo jina , huo niliokupa ni bonge la msaada
Nashukuru sana mkuu naifahamu sana hii hotel na niliwahi lala pale nikiwa Moro ya bwana mmoja alikuwa anafanya CRDB.Ni kweli ni nzuri kwa wao tatizo kabla ya kumaliza saa tisa kikao lazima awe anamyonyesha hapo kati saa nne-tano..(Means awe anarudi).Sasa safari za boda hapo ni changamoto sana kama ruti nne kwa siku.Shukrani sana mkuu ngoja tulitafakari.
Nashukuru sana
 
Habari wanajamvi? Kuna dada yangu kaomba nimsaidie kupata taarifa.Ana kikao morogoro wiki moja ukumbi wa SOCIAL oppposite na Hospitali ya mkoa.Atakuwa na mwanae wa miezi mitatu na mfanyakazi(Baby sitter).Ni Guest/Hotel gani nzuri ambayo ni ya heshima(Nikimaanisha ambayo angalau itatunza heshima ya kukaa na mtoto isiyo na vurugu),walking distance to venue,baby sitter aweze kupata chakula kirahisi kwa bei ya kitanzania jirani au hapo mchana(KUMBUKA MCHANA MAMA MTU YUPO KIAKONI) na wote jioni bila mwendo mrefu.Msaada tafadhali wadau wa mji kasoro bahari.Asanteni.

NB:BAJETI NI 15,000 -20,000.
Ikiwa Ana mkwanja wa kutosha mwambie aanze na

1 FLOMI HOTEL mkoa mzima wa morogoro hakuna hotel yenye ghorofa nyingi kuliko hii fully huduma za kimataifa ila pesa yke ipo juu hadhi yke ni nyota 4.5

9199b5a926159cd17be09d5e2a4d2057.jpg


2 KINGSWAY HOTEL ipo standard ya juu kidogo fully ulinzi na inatoa huduma za benki ndani ya hotel kuna wakala wa CRDB bank kwa ujumla iko fresh sana Nyota 4

3 EDEMA HOTEL ipo standard fully menu iliyoenda shule na ina kumbi nzuri kwaajili ya mikutano na semina

Ushauri wangu kama huyu ndugu yko hela aende hotel hizo nadhani ziko poa zaidi alafu zoo karibu na stand ya MSAMVU hotel yeyote atakayo chukua ktk hizi hatokuwa na haja ya kwenda stand kwa usafiri maana ni pua ma mdomo!!!
 
Jamani mwenzetu anashida na tukumbuke shida siyo ya mtu mmoja wanaoifahamu muonesheni jaman
 
Aje pentagon hotel and guest house kwa bei hizo anazotaka na mahitaji anayotaka au !!
 
Back
Top Bottom