Msaada: GB 1 haimalizi saa 24 kuperuzi

Msaada: GB 1 haimalizi saa 24 kuperuzi

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,623
Reaction score
8,441
Je, umewahi kukutana na tatizo kama hili langu ninalopitia mimi wakati huu?
Na kama umewahi ulitumia njia gani kutatua.

Ipo hivi, mimi ni mtumiaji wa mtandao wa vodacom. Najiunga kifurushi cha DAR SUPER UNI ambacho ni sh 2,000 kwa wiki. Wanatoa offer ya GB 1. Sasa cha ajabu hiyo GB 1 haimalizi hata masaa 24 inakua imeisha kwa matumizi ya kuperuzi hapa JamiiForums, twitter na whatsap. Tena matumizi yenyewe hata situmii kufungua videos. Na sio muda wote nakua nipo na simu maana mimi ni mfanyakazi.

Hili tatizo limeanza Alhamis hii. Nilijiunga kifurushi ilipofika Ijumaa nikatumiwa meseji ya mbs zangu kuisha. Ilibidi nishangae maana sikuwa na matumizi makubwa. Ikabidi nijiunge kingine. Ilipofika Jumamosi mbs zikakata. Nikajiunga tena. Jana Jumapili zimekata. Nikajiunga tena naamka leo asubuhi nakutana na meseji ya mbs kukata.

Sasa nimekuja hapa kuomba msaada kwa wale ambao wamewahi kukutana na shida kama hii walitatua vipi
 
Mimi Halotel kwa mwezi naweka royal najiunga kwa mwezi 10,000 lakini jamaa sijui wanazila vipi gb/mb zangu kwakweli naishia kulipa 30,000 au 40,000 kwa mwezi.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Labda kama simu yako ina run background process, kama vile ku upload files kwenda drive n.k

Clean data counter, (ambayo ipo kwa simu nyingi )
Kesha weka 1gb tena uone mpaka ikiisha data counter itasoma ngapi.
 
Mtandao ukiwa na speed Kali , simu nayo inaweza kufanya mambo mengi background bila kukupa taarifa matokeo yake tunaanza kulaumu kuibiwa data
Tumia data counter ya simu yako , utakuja kugundua data Kama umeibiwa au ilijiibia

Sent
 
Download my data manager, itakuambia matumizi yako kwa kila app hapo utajua unaibiwa wapi.
 
Back
Top Bottom