Habari zenu,
Nipo na project yangu kufanya engine conversion ila sasa nimekwama njiani. Nimeweka engine ya 2jzge non vvti kwenye gari, siku za mwanzo, mafundi walifanya wiring na wakajaribu kuiwasha ikakubali fresh.
Kwa vile ilikuwa kuna vitu vyengine kama exhaust nlikuwa sijamaliza modification, nikapanga na mafundi next day waje waendelee ikiwa nimemaliza kuweka exhaust. Walikuja wakapiga moto, mnyama kawaka fresh tu, kapigwa race bila matatizo.
Sasa mafundi wakapanga waje next day kwa ajili ya kumaliza wiring ya kwenye dashboard na mambo mengine ili kila kitu kifanye kazi kama kawaida. Hapa ndio mtihani ukaanza, wakawasha, mnyama ame race kama kwa sekunde 5 ivi, akazima kama vile mtu kazima kwa funguo. Tukajaribu kuwasha tena haikuwaka kabisa na spark zikapotea.
Tukachomoa betri na kurudisha, mnyama akawaka tena, aka rev sekunde zake 5 akazima tena, ukiwasha tena haiwaki mpaka uchomoe betri na inajirudia ivo ivo.
Mafundi wa umeme wakapima pale wakaona CODE 12, inasema ni RPM signal, lakini wamepima wameona RPM signal inapatikana kwenda kwa ECU haina tatizo, wakaanza kuishutumu Distributor.
Nikawaambia nnavojua mie distriutor kama mbovu, gari haiwaki kabisa, iweje hii inawaka kila ukichomoa betri na kurudisha halafu inakata moto? Wao wakashikilia distributor. Nikanunua nyengine used na kuifunga, Afadhali ile ya mwanzo, hii ndio ilikuwa gari haiwaki kabisa ata ufanye nini. Nikairudisha na sikutaka nyengine.
Kila nlipoenda kwenye spare, jamaa nikiwaeleza gari inavofanya wanasema hio sio distributor ila kuna jengine. Nikakumbuka ECU ilikuwa imeunganishwa na immobiliser (lakini mwanzoni iliwaka bila immobiliser na race ikawa inapiga fresh tu) nikasema tuifunge immobiliser labda ECU ime reset na kudai Immo. Kawaida nnavojua mie, kama gari inadai Immobiliser basi itakuja code 99, lakini haikutokea hii code, lakini mimi na watu wa umeme tukaamua kuifunga, ngoma iko pale pale hamna liwalo.
Sasa apa nimekwama. Mwenye ujuzi wa hili suala anisaidie mawazo. CODE 12 Rpm signal circuit