Msaada: Fedha zangu Tigo Pesa

Bukya

Senior Member
Apr 1, 2014
195
121
Natumai hamjambo wanajamvi. Kitendo ninachofanyiwa na watu wa Tigo Pesa hakika sitakisahau maishani. Nilimtumia ndugu yangu fedha kumbe simu aliyokuwa anaitumia aliibiwa hivyo basi no yake haiko hewani.

Baada ya kuibiwa simu akatafuta simu na line nyingine bila kurudisha no ya zamani. Mimi nikakosea kutuma fedha kwa line iliyoibiwa.

Katika kufanya fatiki nirudishiwe fedha nilipiga no 100 nikaongea na mtoa huduma kwa wateja akaniambia kwamba fedha ipo na wameizuia hivyo nitarudishiwa ndani ya saa 24.

Hakika hii ni wiki ya tatu. Kila nikipiga naambiwa nitarejeshewa baada ya saa 24. Maneno hayo ni wimbo sasa hadi nimechoka. Nilituma hiyo fedha kwa lengo la kutatua matatizo. Ninapowaambia wairudishe kwenye namba yangu ili niitume kwenye namba sahihi nazungushwa hadi najuta. Nawapigia watoa huduma kwa wateja hadi nachoka.
 
Tigo wanamchezo huo sana ku withhold pesa za watu kwa muda mrefu sana bila sababu za msingi!!! Zamani kweli zilikuwa zinarudishwa ndani ya 24hrs sijui ni biashara gani wanazofanya na pesa za watu ambazo sio zao,nafikiri sasa niwakati muafaka wa CEO wao aite press conference na ku address hiyo because simply is against there own company policy which clearly says that the refund shall be done within 24hrs
 
Back
Top Bottom