Msaada: Faida na hasara za kubaki chuo kama tlecturer?

Msaada: Faida na hasara za kubaki chuo kama tlecturer?

bro..mimi nataka nikachukue physics na chemistry je naweza kufikisha hyo GPA kwa hayo masomo

Katika course ambazo unaweza kufikisha G.P.A ya juu ni hizo za science.
Nasema hivyo kwakua hata mimi nilisoma hizo. Walimu wa science hawana longolongo za kujuana. Kwanza wanafunz huwa ni wachache so ni raisi kumfikia lecture kama kuna kitu kinakusumbua...jiamini,achana na maisha ya starehe na jitume sana...inawezekana
 
Mkuu kaza sana!wenzako tunazitamani hizo kazi ila Gpa hizo hatuna!, tuko mtaani tunaganga njaa tu



duu mkuu hebu nimpe moyo mdogo wangu yuko first year semister 1 kapata 4.2, semister 2 hii kapata 4.4, nikampa zawadi ya computer . naona akikaza anaweza pata nafasi nzuri eeh japo ni mwalimu tayari
 
Katika course ambazo unaweza kufikisha G.P.A ya juu ni hizo za science.
Nasema hivyo kwakua hata mimi nilisoma hizo. Walimu wa science hawana longolongo za kujuana. Kwanza wanafunz huwa ni wachache so ni raisi kumfikia lecture kama kuna kitu kinakusumbua...jiamini,achana na maisha ya starehe na jitume sana...inawezekana

asante mkuu itabidi nijitume kweli maana nimechagulwa DUCE
 
Katika course ambazo unaweza kufikisha G.P.A ya juu ni hizo za science.
Nasema hivyo kwakua hata mimi nilisoma hizo. Walimu wa science hawana longolongo za kujuana. Kwanza wanafunz huwa ni wachache so ni raisi kumfikia lecture kama kuna kitu kinakusumbua...jiamini,achana na maisha ya starehe na jitume sana...inawezekana

Ni ushauri Mzuri Wa kutia Moyo ila pia sio kazi rahisi kua na GPA za juu kwenye course za science
 
Nashukuru sana wadau wote kwa kutoa ushirikiano wenu, hakika kwa sasa jibu ambalo nmelipata ni kukaza buti tu na kung'ang'ania hiyo chance coz nnayo hamu sana kuendelea na masomo kadri Mungu anisaidiavyo na hatimaye kuwa reasearcher mzuri sana wa baadaye. Asanteni sanaaa!!!
 
Kuwa lecture ni kuchaguliwa na lectures chuoni ulipo kua unasoma na wala sio GPA kubwa
 
Zamani ndiyo walikuwa wanabakisha kama umepata GPA kubwa zaidi ya wenzio wote.Siku hizi ajira mpaka upitie PSRS_ajira,lakini pamoja na kuwa na GPA kubwa lazima uwe na Mtetezi wa kukusemea.Kuna Vyuo hata iweje bila Refa utavisikia pamoja na kuwa na first class yako.Cha kukushauri wewe kazana kusoma utoke na GPA ambayo itakuwezesha kupata scholarship za kusomea Masters.Kwa mfano tuu yupo jamaa alipata First class akaenda kusoma nje Masters&PhD amerudi kaomba Assistant Lecturer zaidi ya Vyuo 3 kala za uso.Mfano mwingine mimi mwenyewe nilikuwa nataka nisepe kituo changu cha kazi ,nishatimba saili 3 vyuo tofauti na nimekula za uso.So haya mambo ya kujuana yapo sana,(unaweza kuwa na jina tuu la ukanda flani ikawa imekubeba hiyo).
 
Habari zenu wanajamvi wa jukwaa hili la elimu.

Ningependa niende moja kwa moja kwenye kiini cha swali langu kama kichwa cha hoja kinavyouliza.

Naombeni msaada wenu juu ya faida au/na hasara za kubaki chuoni kama tutorial assistant (TA) na baadaye kuendelea kuwa lecturer kama masters graduate.

PHD holder au Professor. Nahitaji majibu kutoka kwa kila mtu, aidha unao uzoefu na kazi hizi;

Au ndugu, jamaa na marafiki ni miongoni mwa watu waliopo vyuoni kwa kazi hizi; na pengine umewahi kusikia tu habari mbili tatu juu ya swala hili.

Uwanja ni wenu wanajamvi wote nakaribisha majibu yenu.

Asanteni!
Usidhani ni rahisi kupata hiyo kazi, lazima ufanye mtihani utumishi, watu tuna maG.PA yetu ya 4.5 lakini tupo nyumbani tu na siko peke yangu ni wengi siku hizi G.P.A sio issue soma elewa vitu vizuri tengeneza connection mapema utapata kazi haraka na pia usiweke akili kuajiliwa sana elewa vitu jiajili mwenyewe.
 
Back
Top Bottom