Kama kila kitu kina faida na hasara zake. Je, kuna faida gani za kuwa masikini?

Kama kila kitu kina faida na hasara zake. Je, kuna faida gani za kuwa masikini?

Hasara za Umasikini ni nyingi sana kuzidi faida, Ni sawa na kuwa na duka kubwa la hardware huuzi chochote, unategemea faida ya kuchajia watu simu,

Umasikini unatisha sana, tena bora uwe peke yako lakini ukishakuwa na familia inayokutegemea ni tabu sana, fikiria tu unamuona mtoto wako anakufa mbele ya macho yako kwa kushindwa kumudu laki 5 ya matibabu.
 
Kama kila kitu kina faida na hasara zake je, kuna faida gani za kuwa maskini?
Hakuna anakuja kukutembelea siku za sikukuu.

Matatizo makubwa ya familia hushirikishwi.

Kwenye harusi za watu wako wa karibu hawakuweki kwenye kamati.

Unalala mlango wazi na hata panya tu haingii.

Mwisho kabisa mungu amekupa chapuo ya 85% kwenda mbinguni.
 
Asilimia kubwa ya watoto walio kulia maisha bora au familia ya kitajiri hua wengi wao wamekosa elim kubwa sana ambayo mtoto masikini huipata nayo ni kua na adabu na heshima kwa anacho kipata na hata akipata hela wengi hua na utulivu na kulinda alicho nacho kisipotee na huwezi kuta na sifa za ajabu ajabu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom