Msaada: Eti nilipe mahari milioni nne (4,000,000)?!

Msaada: Eti nilipe mahari milioni nne (4,000,000)?!

Mimi ni mmoja wa watu wanao pingana na dhana ya mahali maana naiona kama biashara na pia hakuna thamani ya kulinganishwa na thamani ya mwanamke!

Kama una kubaliana na dhana ya mahari lipa hiyo maana huyo mke ni wa thamani zaidi ya hiyo!
Pengine kwanini hutaki kulipa hiyo?
Unafikiri mchumba wako ni wa thamani ya sh ngapi?

Mahari inaweza kulipwa kwa awamu si lazima yote kwa siku moja.
 
Naomba kujua mwisho wa kuandika barua za kwenye karatasi itakua lini?!
Make tuko kwenye ulimwengu wa digital, whatup, phone calls, txt msg etc.
Ivi huko ulaya na asia bado wanafanya ivo!
 
Yaani nilipe mahari milioni nne huyo binti atachakaaaa kinyeo
 
Baada ya kuwa katika uchumba kwa kipindi kisicho pungua miaka miwili tangu tuhitimu wote elimu ya chuo kikuu na binti mmoja mwenye asili ya mikoa ya kaskazini (killer-manjaro) nikaamua sasa acha nifanye mambo yawe formal zaidi ili nichukue mke. Nimepeleka barua ya uchumba miezi kadhaa iliyopita huko kwa wazazi wake Tegeta na kufika juzi jioni ndio nikapata kujua kuwa nimekubaliwa ila ni lazima nitoe mahari (bride price) ya shilingi milion nne ili mambo mengine yaweze kuendelea. Na tangu nipate kazi ndio kwanza nina mwaka sasa na hiyo pesa ni nyingi sana siwezi kumudu kuilipa. Sasa ninajiuliza sijui niombe punguzo au nifanyeje sasa. Ninaomba ushauri wenu nimechanganyikiwa hapa nilipo.

Ridiculous,hiyo sasa ni biashara.Frankly speaking ningekuwa mimi I would call it quits straight away,hao jamaa hawako serious.Ila kwa sababu ni wewe omba, punguzo wakikataa achana nae,wako wengi wazuri,tena zaidi yake.Nahisi ni Mchaga huyo.Tena afadhali awe Mchaga kabila ingine, kama ni Mmachame kimbia.Inawewezekama wanakufukuza ki-silencer,si huna kituu.Hao wanataka nyumba,gari na kabati la mbeho.
 
kijana we sema poa ila kwa sasa unapunguza utamaliza kwa instalments wataelewa...umetaka cha uvunguni...
 
maximum bride price ntakayolipa itakuwa 1.5 million..

mengineyo tutasaidiana kadri miaka itakavyoenda..

1.5m ikiwa ni mahari tu au kila kitu? Nikiwa na maana hapo kuna kondoo, vitenge, blankets, miguu ya ng'ombe na mengineyo mengi tu kutegemea kabila unalooa..
 
Nadhani ndio maana vijana wengi wanakimbia "ndoa rasmi", fikiria kijana ana mwaka mmoja kazini, bado hajajijenga kabisa, unamtajia 4m...azitoa wapi? Inawezekana pia wazazi wake hawana uwezo huo, it's just insane kwa kweli...

Pili, kumbuka mahari ni step moja, bado ndoa..ambazo kwa wadada wengi saivi si rahisi kuikwepa, tena ndoa na "sherehe ya nguvu". Gharama zake toka mfukoni kwa bwana arusi tu zaweza kufika 4m, jamani tunawapa vijana wakati mgumu sana.
 
Baada ya kuwa katika uchumba kwa kipindi kisicho pungua miaka miwili tangu tuhitimu wote elimu ya chuo kikuu na binti mmoja mwenye asili ya mikoa ya kaskazini (killer-manjaro) nikaamua sasa acha nifanye mambo yawe formal zaidi ili nichukue mke. Nimepeleka barua ya uchumba miezi kadhaa iliyopita huko kwa wazazi wake Tegeta na kufika juzi jioni ndio nikapata kujua kuwa nimekubaliwa ila ni lazima nitoe mahari (bride price) ya shilingi milion nne ili mambo mengine yaweze kuendelea. Na tangu nipate kazi ndio kwanza nina mwaka sasa na hiyo pesa ni nyingi sana siwezi kumudu kuilipa. Sasa ninajiuliza sijui niombe punguzo au nifanyeje sasa. Ninaomba ushauri wenu nimechanganyikiwa hapa nilipo.

kaka mkeo ana wazo gani na anakushauri nn juu ya hiyo pesa?
 
Back
Top Bottom