BM-40 OPERATOR
Senior Member
- Oct 13, 2012
- 153
- 56
Baada ya kuwa katika uchumba kwa kipindi kisicho pungua miaka miwili tangu tuhitimu wote elimu ya chuo kikuu na binti mmoja mwenye asili ya mikoa ya kaskazini (killer-manjaro) nikaamua sasa acha nifanye mambo yawe formal zaidi ili nichukue mke.
Nimepeleka barua ya uchumba miezi kadhaa iliyopita huko kwa wazazi wake Tegeta na kufika juzi jioni ndio nikapata kujua kuwa nimekubaliwa ila ni lazima nitoe mahari (bride price) ya shilingi milion nne ili mambo mengine yaweze kuendelea.
Na tangu nipate kazi ndio kwanza nina mwaka sasa na hiyo pesa ni nyingi sana siwezi kumudu kuilipa.
Sasa ninajiuliza sijui niombe punguzo au nifanyeje sasa. Ninaomba ushauri wenu nimechanganyikiwa hapa nilipo.