Msaada, dawa ya kuachana na mapenzi

Msaada, dawa ya kuachana na mapenzi

Mamie ni ngumu kuyakwepa mapenzi ila unauwezo wa kuyapumzisha ushauri wangu kwako jipe likizo ya muda fulani unaweza kuchukua hata mwezi ili utoe ushungu na stress ulizonazo then endelea na maisha kama kawaida

Dada ni kuambie kitu mapenzi ya dhati yapo sema wewe umeshindwa kumpata mtu sahihi wakuingia kwenye mahusiano na wewe ila wanaume wapo ambao wapo wanaojua kupenda, waaminifu, wanajali na wanaoweza kumpa thamani mwanamke sema wewe umeshindwa kuwapata wa namna hii muombe Mungu na sali I hope one day utampata wa namna hii.

Pia mwambie asiwe na matarajio mengi kwenye mapenzi siku za mwanzoni,coz anaonekana anaweka nguvu zake zote kwenye mapenzi. Muda ndo unafaa kuamua wether mtu ni sahihi au la!..ukiamua kwa kuangalia jinsi anavyokufanyia ni rahisi kufanya maamuzi yasiyo sahihi coz wanaume huwa tuna igiza sana ili tumpate mdada then tukipita naye tunajionesha uhalisia wetu.
 
Huwezi kuacha mapenzi kisa kuumizwa.
Mapenzi utayaacha ukiwa mgonjwa ama umekufa.
Relax utakuwa sawa tu.
 
Nakumbuka kipindi nolivo kua na depression kama hiyo niliamua kuachana namapezi angalau kwa miaka mitatu, nikapata pschological counselor, kutoka office fulani ila ndani ya miezi mitatu tulianza mahusiano nae, tena yalikua ya moto hata kuliko ya awali, so napenzi ni sehemu ya maisha ya mtu.
Aisee

But mimi pia ni km mleta mada nimepumzika naelekea kuacha kabisa.
 
Pia mwambie asiwe na matarajio mengi kwenye mapenzi siku za mwanzoni,coz anaonekana anaweka nguvu zake zote kwenye mapenzi..Muda ndo unafaa kuamua wether mtu ni sahihi au la!..ukiamua kwa kuangalia jinsi anavyokufanyia ni rahisi kufanya maamuzi yasiyo sahihi coz wanaume huwa tuna igiza sana ili tumpate mdada then tukipita naye tunajionesha uhalisia wetu.
Yaani wadada hili mpka leo hawajalijua tuu🤣🤣🤣🤣
 
Mpango wa kuacha mapenzi sina, japo yameniotea yakanichapa hatari mpaka nikadata,
Ila hayo mapenzi yajage tu yaniue yataamua yenyewe yazike ama yasafirishe..!
Hahahaaa nimecheka kibwege Sanaa ,yapo kama ngumi yakikuotea utajuta!! sema nini ugomvi wa kiarusha unarudi nyuma unajipanga upya
 
Izo ni dalili za kuwa mchawi hutaki kupenda Wala hutaki kupendwa kunakoelekea utanza kuchukia watu wakipendana
 
Njia ni moja tuu, " kuwa chanzo Cha furaha yako"... Usitegemee upate furaha eti ukiingia kwenye mapenzi. Kwani kabla ya yeye ulikuwa waishije?
 
Kule Tarime nasikia kuna kitu wanakifyatua unakuwa hisialess
 
Tafuta mwanamme asiye na kazi Wala mke na watoto. Kisha nenda Tabora ukafundishwe jinsi ya kumlisha limbwata.
Thank me later.
 
Nahitaji msaada wenu ndugu zangu,

Ni jinsi gani naweza fanya kuachana kabisa na kitu kinaitwa mapenzi? Yaani kamwe nisifikirie mahusiano kabisaaa? Maisha yangu yaliyobaki niwaze tu pesa niifurahishe nafsi yangu.

Kama kuna njia zozote za kisaikolojia naombeni mchango wenu, yaani nisipende tena, hata nisipendwe tena. Hata kama ni kwa dawa za kienyeji au waganga niko tayari

Kuliko kuumiza moyo wangu, mara leo furaha kesho uzuni, kesho kutwa mateso, bora niyafurahie maisha kwa pesa tu, vinywaji tu na viwanja, kuliko unaliamini jitu, unalipa moyo wako, unamnyima mwingine ukiamini kuwa hana malengo nawe, anakulilia, mwisho wa siku unawakosa wote na vidonda juu

Kwa wale ambao mmefanikisha kuishi wenyewe na amani ya moyo msaada wenu tafadhari
We tafuta mtu sahihi tu utasahau yote uyasemayo

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Pole, Kwa mm naona hapa tiba ya ushauri ataiotoa mzabzab tu au smart man Extrovert

Zingatia Sana ushaur wa hawa watu
Mkuu kuwaza pesa ni jambo zuri ila ikiwa kashafanya mambo yanayotakikana...Kama ana watoto kashapata basi focus lazma iende kwenye pesa tu. Kwahio atafute watoto kwanza akili ya pesa huja automatically.
 
Nahitaji msaada wenu ndugu zangu,

Ni jinsi gani naweza fanya kuachana kabisa na kitu kinaitwa mapenzi? Yaani kamwe nisifikirie mahusiano kabisaaa? Maisha yangu yaliyobaki niwaze tu pesa niifurahishe nafsi yangu.

Kama kuna njia zozote za kisaikolojia naombeni mchango wenu, yaani nisipende tena, hata nisipendwe tena. Hata kama ni kwa dawa za kienyeji au waganga niko tayari

Kuliko kuumiza moyo wangu, mara leo furaha kesho uzuni, kesho kutwa mateso, bora niyafurahie maisha kwa pesa tu, vinywaji tu na viwanja, kuliko unaliamini jitu, unalipa moyo wako, unamnyima mwingine ukiamini kuwa hana malengo nawe, anakulilia, mwisho wa siku unawakosa wote na vidonda juu

Kwa wale ambao mmefanikisha kuishi wenyewe na amani ya moyo msaada wenu tafadhari
Si ukatafute Kazi ngumu uone kama utawaza sio unashinda umelala ndani unadhani utaacha kuwaza
 
Any updates mamy??? Vipi saivi kimahusiano akili imetulia??
 
Back
Top Bottom