Msaada: Brand nzuri ya projector

Msaada: Brand nzuri ya projector

mkadiriajimajenzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
551
Reaction score
618
Nataka kununua projector kwa ajili ya marumizi ya ofisi,je ni vitu gani nizingatie? brand ipi ya projector inaongoza kwa ubora?
 
vitu muhimu zaidi kwenye projector
1. resolution
2. lumens
3. umbali wa kuonyeshea.

resolution ni ubora wa picha, ukikosa kabisa atleaelst 720p kwa lugha nyengine HD (1280x720) ila lenga upate 1080p au full hd (1080p)

lumens ni wingi wa mwanga unaotoka kwenye projector kama utaitumia mchana au nje maeneo yenye mwanga itabidi iwe na lumens za kutosha, ikiwa ni ndani au usiku lumens za kawaida zinatosha

kuna projector hata ikiwa umbali wa mita moja tu basi inamulika ukuta mzima wakati nyengine hadi ziwe mbali ndio ziweze kumulika ukuta mzima.
 
Accer sikushauri, nunua Epson ndo wababe wa projector kwa sasa
 
Ungemsaidia mkuu kwa specs pia ungesaidia wengi sana kama mdau wa Pili alivyojibu general technicalities
 
Epson nyingi zina specifications hizo hapo juu, ila zinaongezeka hizi HDMA port, in and out USB port, wireless and LAN connection, Multimedia Projection(yani ina speakers+HD image resolutions)
 
Vipi kuhusu Sony nilisikia nao wako vizuri
 
Karibu zote nimezitumia mkuu, Epson ndo the best kwa upande wangu
Wewe unajua projector, kwa sasa hakuna inafikia Epson, ninazo kama 5 kwa kazi zangu,
Zamani nilikuwa najaribu kuchanganya aina tofauti mara Sony, Acer, Ila nikagundua hakuna kama Epson
 
Accer sikushauri, nunua Epson ndo wababe wa projector kwa sasa
Katika taasisi yetu tulifunga projector 15, ni za aina mbili Epson zipo 4 ambazo tulinuna kwa bei ya juu sana na Accer zipo 11, ambazo tumezipata kwa bei nafuu, tunazitumia sasa kwa miaka 3, tayari Epson 2 zimeshakufa na moja inasumbua, uzoefu umetuonyesha kuwa kwa umeme wetu wa kibongo ambao una panda na kushuk ovyo, Accer ndio zinafaa, na hata clearness ya picha ziko vizuri zaidi, kuhusu specifications, rejea mchangiaji Chief Mkwa kaweka wazi kila kitu
 
kifupi hakuna brand ya malaika kila brand ina bidhaa nzuri na mbaya, ukikariri epson nzuri unaweza ukauziwa epson ya mwaka 2000 kimeo mwisho wa siku usipate huduma nzuri.

ni vyema kupitia site za wataalamu kujua zaidi kuhusu haya mambo,
 
Zote kati ya aina zote mbili za projector zilikuwa ni latest versions kwa wakati huo, na kwa kuongeza hizo epson zilinuliwa kutoka UK moja kwa moja na hizo Accer zilinunuliwa hapa Dar es salaam,
Nilichofanya hapo juu ni kumsaidia ndugu yetu aangalie kinachoweza kumfaa na sio kukaririshwa brand, kuna baadhi ya vitu tunauziwa bei juu haliyakuwa havina ubora. Ninae zungumza hapa IT ndio fani yangu
 
mkuu projector latest inayotick box zote kwa vitu kama 4k. HDR na lumens za kutosha ujue tunazungumzia milioni kama 7 hivi kupanda. sidhani kama kampuni yenu ilitoa milioni 7 kununua projector
 
Nadhan ndugu yangu mkwawa tutaenda mbali zaidi, kiukweli hizo projector ni za bei ya kawaida tu, kwani sikumbuki ilikuwa ni Pound ngapi lakini kwa Tsh, iligharimu km 1.4 M kila moja, wakati hizi tulizo nunua hapa ilikuwa ni Lak 6.5, sasa jiulize wewe kwanini kitu cha nusu bei kidumu huku kile cha bei ya juu kife haraka ?
 
ndio mkuu tusipojua exactly aina ya hizo epson itakuwa ngumu kujadili zaidi, na hamkupewa warranty mzirudishe?
 
Back
Top Bottom