Msaada: Biashara ya kutafsiri filamu za nje ya nchi

jino

Member
Dec 21, 2013
33
12
Tangu mwaka 2014 nilikuwa nahangaika jinsi ya kuweka subtitle za kiswahili katika movie za nje kwa sababu nilipokuwa nyumbani na wadogo zangu nilikuwa napata tabu sana kuanza kuwasimulia kila kitu kinachotokea katika movie tunayoangalia.

Nikaona kwanini nisijifunze jinsi ya kuweka subtitle ili wawe wanasoma wenyewe? Nikaanza kufanyia kazi wazo langu na hadi juzi nilipoona nimefanikisha na kuomba kujisajili na web moja inaitwa subscene kwa ajili ya kuwa naziweka huko.

Wamenimbia hadi wazikague kama zipo vizuri, ila changamoto nilizonazo ni mbili

1. Kuandaa subtitle zina tumia muda mwingi sana hadi nakata tamaa.

2. Mzee wangu ananiambia nitafute kazi nyingine na niachane na hayo mambo.
Naomba ushauri kwa hilo

Na pili sasa hivi nimeanza utafiti wa kuweka audio na kutoa audio zile zilizopo na kuweka za kiswahili kama vile Wafilipino wanavyofanya wanaweka audio za kingereza japo ndo nianza utafiti.

Kama una cha kunishauri au kuongeza naomba pia ushauri.

Asanteni sana.
 
Kuna software nyingi tu za kutumia. Rahisi ni iliyoko kwenye "Notepad" Windows OS. Lakini inabidi uwe unafahamu lugha iliyotumiwa kwenye hiyo movie, kwa ufasaha, ili tafsiri yako iwe sahihi. Baadhi ya bongo movie wanaweka tafsiri za hovyo za kiingereza
 
Za audio ndio zinapendwa zaidi yani zile zakusimulia kama wafanyavyo kina dj muphy
Audio nazo zungumzia hapa Mkuu siyo kama za madj mfano movie ni ya kiingereza ila wanaongea kihindi na hakuna kuweka matangazo ila kinacho tamkwa kinakuwa kile kile ila kwa lugha ya kiswahili
 
Yaa hata Mimi naitumia ila changamoto yake ni hadi uwe na subtitle ya movie usika lakini kama hauna inakuwa ngumu kutumia nfano movie nyingi za kichina hazina subtitle hivyo inakulazim kutengeneza.
Kwann usianze hizi zenye subtitle, kwa sababu ni nyingi sana kwa kuanza kazi ,hapo sioni tatizo mkubwa
 
Kwann usianze hizi zenye subtitle, kwa sababu ni nyingi sana kwa kuanza kazi ,hapo sioni tatizo mkubwa
Asante ndugu yangu kwa ushauri si unajua mtu akifika hatua moja na kuifaulu anatamani kwenda hatua kubwa zaidi nashukuru sana mkuu hizo zipo subscene wakikubali nitaziweka huko.
 
Audio nazo zungumzia hapa Mkuu siyo kama za madj mfano movie ni ya kiingereza ila wanaongea kihindi na hakuna kuweka matangazo ila kinacho tamkwa kinakuwa kile kile ila kwa lugha ya kiswahili
Nimekuelewa ila iyo prosesi yake ni ndefu kidogo kuliko izi za ma dj.
mfano iyo unayosema ww inahitaji watu wengi kuingiza sauti kama mwanamke anaongea unaingiza sauti ya kike kama mwanaume hvyohvyo.mfano kama muvi inawatu ishirini yahitaji utafute watu 20 wakuingiza sauti zao.

au mm nawaza tofauti??
 
Hapana kwasasa kuna program ambayo yenyewe unaandika tu maneno yenyewe inakupa sauti unayota iwe ya mtoto,mkubwa yeyote unaemwitaji.Na unaweza kudomload sauti.
 
Back
Top Bottom