Msaada: "Baba Mkwe ananinyatia!"

Mpe
soma math 7:7

Matayo 7
Usihukumu Wengine
1 Usihukumu ili na wewe usihukumiwe. 2Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea. 3Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? 4Au unawezaje kumwambia ndugu yako, `Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,' wakati jichoni mwako mna pande kubwa? 5Mnafiki wewe! Toa kwanza pande lililoko jichoni mwako, ndipo utaweza kuona vema, upate kukitoa kipande kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.
6``Msiwape mbwa vitu vitakatifu; na msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga kanyaga na halafu wawageukie na kuwashambulia.''

Omba, Tafuta, Bisha Hodi
7``Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. 8Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.

9``Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.''

Njia Nyembamba Na Njia Pana
13``Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.''
Manabii Wa Uongo
15``Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.''
Mfuasi Wa Kweli
21``Si kila mtu anayesema, `Bwana, Bwana,' ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22Siku ile itakapofika wengi wata niambia, `Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?' 23Ndipo nitawaambia wazi, `Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!'
Nyumba Iliyojengwa Kwenye Mwamba
24``Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.'' 28Na Yesu alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu waliomsikiliza walishangaa sana, 29kwa sababu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama walimu wao wa sheria.
 
matatizo mengine mnayaalika wenyewe...! ongea na mumeo... akiwa mbishi shirikianeni muweke mtegoni... akinaswa apigwe faini na atimue kwa mke wake!!
 
Mzee anataka kuchakachua jamani, umemchekea huyo ndiyo maana anakuzoea!!! lazimauonyeshe kuwa upumbavu kwako hauna nafasi.
 
Haya ndiyo yanasababisha Wamarekani wanatoa hisani...Kutukumbusha tuzungumze! Sasa huyu haongei na mumewe kisa!
 
Back
Top Bottom