Nimeambukizwa virusi vya UKIMWI (H.I.V)

Don Billionea

Senior Member
Jul 15, 2018
150
193
Habari wanaJF, mimi ni kijana niliyekuwa ninajichunga na kuijali sana afya yangu kiasi cha kuwa na mabox ya vipimo vya H.I.V rapid test ghetto, ikiwa kama nimejichanganya basi nawahi dawa za PrEP.

Dawa za PrEP nimemeza round mbili yaani 2017, 2020 baada ya kucheza rough.

Nilikuwa napima maambukizi na mwenza wangu mara kwa mara, hivi sasa mwenza wangu anamalizia masomo ili mwakani July tuanze kuishi pamoja. Sasa mwezi Agosti mwaka huu nimekutana na mwanamke ambae tunameet na kusekx na huwa tunacheki afya, sasa mwezi huo nikapuuza kwakuwa tulicheki afya mwezi May nikamla then maisha yakaendelea.

Mwezi Octoba juzi tu nikajaribu kupima peke yangu ghetto nikakutana na mistari miwili CONTROL na 1, nilipima zaid ya mara tano hapo hapo gheto inasoma mistari miwili. Dah pressure ikawa kubwa.

Nikaenda Hospital napo inaonesha nipo POSITIVE, wakanianzishia dawa za ARV's hadi sasa ninamaliza wiki tangu nianze dozi za ARV's. Next wiki wananianzishia na dozi ya miezi sita ya Anti-T.B...

Juzi nipo YouTube nakuta kuna shuhuda nyingi sana kwamba kuna Mtaalamu anaponesha hili janga from POSITIVE to NEGATIVE anaitwa TR. MSIGWA, jamani waungwana kuna yeyote mwenye hakika na hili jambo hata ndugu yake alipata kupona kwa huyu docta maana kichwa kinawaka sahizi sielewi, nikapata mawasiliano yake akaniambia dozi ni shilling 280k ya siku 45 inaitwa (4A9).

Wajameni hivi ili suala lina ukweli dawa hiyo ya Asili inasaidia kwa yeyote aliyawahi pata experience hii hata kwa ndugu yake kuhusu uyu mtaalamu TR. MSIGWA na dawa yake ya 4A9 maana nina wiki tu tangu nianze kumeza ARV's lakini nahisi hali ya kuzichoka tayari.

Nawasilisha:
 
Pole sana, zingatia dozi utaishi muda mrefu kama ilivyo kwa wengine

Kwa tiba asili huwa nasikia kumenya kisha kuchemsha cactus ni dawa ila hakuna mrejesho credible mpaka sasa.

1699005439657.png


Huko mitandaoni jihadhari, kuna matapeli wanajinadi ni madokta, wachungaji, ustadh, waganga, ni mabingwa pia wa kuandaa shuhuda za kuvutia wateja.
 
Juzi nipo YouTube nakuta kuna shuhuda nyingi sana kwamba kuna Mtaalamu anaponesha ili janga from POSITIVE to NEGATIVE anaitwa TR. MSIGWA, jaman waungwana kuna yeyote mwenye hakika na ili jambo ata ndugu yake alipata kupona kwa uyu docta maana kichwa kinawaka saiz sielewi, nikapata mawasiliano yake akaniambia dozi ni shilling 280k ya siku 45 inaitwa (4A9).
Hapa unapitia stages of grief tu, ila utakuja kukubaliana na ukweli....

POLE SANA
 
DR. Msigwa niliangalia mahojiano yake kwenye Tv alisema NIMR wamemzungusha.

Labda nenda katibiwe ukirudi umepona tuitumie kesi yako kama ripoti ya mtu mmojammoja anecdotal evidence

Na nipo interested kama kuna mtu ametibiwa na Dr Msigwa akapona hebu ailete ripoti yake hapa!

Na kama ndo wewe mwenyewe Msigwa uloandika au chawa wake, naomba jazeni hii uzi kwa shuhuda halisi. Asanteni
 
Back
Top Bottom