Nina miaka 25 Jamani Mimi huwa nashangazwa na baadhi ya tabia zangu mfano napenda kujitenga mwenyewe kimya, au nasikiliza mziki Kwa sauti ya Chini mno,nnaposema napenda kujitenga ni pamoja na kuchukia kampani ya mtu yoyote Yule Yani Mimi nusu saa huku namsikiliza mtu au watu wakiongea kwangu ni kero sana..nikiwa mwenyewe kimya mara nyingi najisomea vitabu nakuwa na furaha pia nahisi Sura yangu ikiondoa mikunjo, ila nikiwa na rafiki yangu yoyote nakuwa nahisi kabisa kuwa anagundua namna nnavyoboeka..napenda mahusiano ila nikikaa na girl Tu mara ya Kwanza ya pili zile exaggerations zao zinaniboa au wakija getto redio sauti ya juu na ni relationships nyingi nimevunja mwenyewe Kwa kuomba kuachana ambapo wengi wakiuliza tatizo nini niliwajibu haikupangwa tuwe pamoja na ila uwa wananiachia kibwagizo kuwa siko sawa, sio muongeaji kabisa kazini ambako ndo mahali pangu pagumu mno kuishi uwa nachukuliwa mtu makini, mstaarabu uwa wanadhani ni mtu nnaewasikiliza Sana ila mara nyingi uwa sijui huwa wanazungumzaga nini maana ni kama nakuwa katika ulimwengu wangu ila wao wanapiga kelele kuni disturb Girl ukiona nimekuapproach ujue hakika wewe ni mrembo maana mpaka kufikia umri huu nimewahi kutongoza kama mara mbili Tu ila wengi uwa wanajiweka kwenye reli kama kuniactivate
Jamani naomba msaada Nina mambo mengi naweza kukaa ndani kuanzia ijumaa jioni Hadi jumatatu asubuhi najisomeaa Tu na sijui napenda kusoma au natafuta nini katika kujisomea Hali hii inanifanya nisipende kuwatafuta watu wangu wa karibu kwenye simu,marafiki zangu ni walewale wa siku zote walionizoea since sina mlango Kwa marafiki wapya Yani hata kazini sina wakusema ni mshikaji ila wananipenda nadhani Kwa sababu siko kwenye upande wowote wa wafanyakazi wenzangu pia Mimi ni mbishi nasimamia misimamo yangu Tu ila sio Kwa sauti so huwezi kunipinga, since sipendi mikusanyiko sio mtu wa majumba ya ibada ila getto nipo full biblia na Qur'an nnazo na nasoma Sana vitabu vya theology.
