Msaada: Anayejua mahari za wamasai anisaidie

chogobilo

Senior Member
Aug 28, 2013
113
77
Wanabodi habari za jioni,

Naomba mnisaidie,yeyote anayefahamu utaratibu wa mahari kwa ndugu zetu wamasai umekaaje anisaidie,nakaribia kwenda umasaini kwa issue za mahari,mwenye uzoefu aumwage hapa ikiwa ni pamoja na gharama au vitu wanavyohitaji.

Nawasilisha
 
kama uko seriius ni pm na ujue kabisa mahari ya kimasai si pesa na hailipwi yote mpaka unakufa na watoto watalipa pia kama demu wako masai muulize au akuunganishe kwa masai mtu mzima hapo ulipo
 
We ua simba then nenda na mkia au kichwa, baaaaaaaaaasi hautadaiwa chochote
 
andaa sime ya mjomba, mashuka mawili ya bibi na babu chumbani, ngombe na mbusi wa kutosa, hapon itapata mke...:rockon::rockon:
 
#masaidada njoo msaidie shemeji yenu,,,

huyu jamaa ana mengi madogo madogo yakufata

lakini cha kwanza apeleke wazee wake either mjomba na Baba(mara nyingi maonaga hivi)
hapa ni kubisha hodi

wakishakwenda huko watapewa ABC zote maana inategemea boma na boma
na pia inategemea ni wamasai au waarusha lakini pia inategemea
1.kama umempa binti mimba kuna faini
2.kama umeenda kichwa kichwa kuna faini kwamba umeenda kutukana

so njia nzuri ni kutuma wazee pale taratibu zote mtaelekezwa
mara nyingi mahari sio kubwa especially kwa remekii sema wengine hujiongeza
kwa mfano mara nyingi utaambiwa
brangeti la mama,kondoo ya mama
suti ya baba,sijui kitenge,shangazi nae anapata kitu

alafu unakuja kuambiwa ndama dume kadhaa mara nyingi 1 au 2,
pia kuna kipengele cha kupeleka pesa ya kufungia mlango
ZAMANI HAPA ILIKUA UNAPLEKA PETE AU BANGILI

pia kuna siku ya kupeleka soda(kipindi cha vikao vya mahari)
zamani ilikua pombe

ila hapo inayegemeana sehem na sehemu
SO CHA KWANZA KATUME WAZEE
 
kama uko seriius ni pm na ujue kabisa mahari ya kimasai si pesa na hailipwi yote mpaka unakufa na watoto watalipa pia kama demu wako masai muulize au akuunganishe kwa masai mtu mzima hapo ulipo

teh teh
mambo hayaendi kienyeji hivyo
si unajua ndo tamaduni iliyobaki inaenziwa
 
teh teh
mambo hayaendi kienyeji hivyo
si unajua ndo tamaduni iliyobaki inaenziwa
hivi process za kupeleka lotion,mbavu za dume iliyochomwa ni waarusha au wamasai?ila napenda sana waarusha wanavyofanya ingawa sidhani tofauti yao na wamasai
 
hivi process za kupeleka lotion,mbavu za dume iliyochomwa ni waarusha au wamasai?ila napenda sana waarusha wanavyofanya ingawa sidhani tofauti yao na wamasai

kuna tofauti kubwa sana kimila kati ya wamasai na waarusha
vile vile kati ya ukoo na ukoo
vile vile kati ya boma na boma

taratibu zingine za mahari hutokana na wazee wa ukoo pale au wazee wa boma watakovyosema lakini mara nyingi hufanana fanana
sema mambo ya utandawazi nayo kidogo yanapenya zamani ilikua pesa upeleki hata sumni lakini now kwenye barua ya kifunga uchumba waweza peleka pesa

zamani ilikua bangili na pete
lakini hii pia inategmeana koo kwa koo
mi ni muarusha akiongea mmasai siwezi msikia vyema naokota kimoja kimoja..tofauti ipo
 
Napenda sana ndoa za kiarusha,hizo process za wazee itakutesa sana na gharama,ila siku ya harusi zile zawadi bhana wanajengea wanae future nzuri,unakuta baba yake msichana anatoa ndama,

hapo hapo familia inatoa ng'ombe wa maziwa,makochi,vitanda,mama mkwe(mama wa msichana)bado anakuja na kabati iliyojaa glasses,sahani.

Upande wa kaka nao zawadi zao si haba,aiseee unakamilika siku ya send off au kufunga ndoa.Yaani kwa upande wa kuoa ni mila nzuri sana,1998-2004 niliishi huko mitaa ya Olkereyani basi raha tupu
 
unapewa mpaka chungu,kipekecho,fagio
teh teh
kaoe huko Olkereyani
 
unapewa mpaka chungu,kipekecho,fagio
teh teh
kaoe huko Olkereyani
hahaha sasa hivi ninapoishi ni bara lingine....ila bhana kwenye ndoa waarusha nimewapigia saluti inatakiwa waigwe na wengine,niliishi Olkereyan enzi hizo,Engototo,Moshono,Njiro,suye kule masai Camp shahidi Mr Rocky,nahisi arusha siku hizi imebadilika,ila wakati huo hehehe nilikuwa mdogo nikawa natamani nioe,mchumba wangu nikiwa under 18 yrs nilimpoteza huko maana sisi watu wa kuja,halafu wao wakahama,aisee waarusha mila yao nzuri bhana
 
Last edited by a moderator:
hahaha sasa hivi ninapoishi ni bara lingine....ila bhana kwenye ndoa waarusha nimewapigia saluti inatakiwa waigwe na wengine,niliishi Olkereyan enzi hizo,Engototo,Moshono,Njiro,suye kule masai Camp shahidi Mr Rocky,

nahisi arusha siku hizi imebadilika,ila wakati huo hehehe nilikuwa mdogo nikawa natamani nioe,mchumba wangu nikiwa under 18 yrs nilimpoteza huko maana sisi watu wa kuja,halafu wao wakahama,aisee waarusha mila yao nzuri bhana

aiseee pole sana
ulishakaa oldonyosambu??
pale ndo home
 
aiseee pole sana
ulishakaa oldonyosambu??
pale ndo home
hahahha nilikuwa nasikia,tulipomaliza darasa la saba form one nilichaguliwa Oldonyosambu,Nduruma huko kwenye maembe,na oldadai,ila nilichagua oldadai,hheehe tulikuwa tunaenda kuchota maji kule alaluwa,ukichelewa unarudi na kichura chura
 
Peleka Sukari kilo 5 na Majani ya chai kwa ajili ya utambulisho, mara ya pili unapeleka crate 2 za soda, utapangiwa siku ya kukutana na boma, utapeleka crate 4 za soda na nyama mguu wa nyuma + Mbavu, blanket, mgoroli, unsubiri kupewa mke, hio inatumika kwa wamasai na waarusha
 
Kijana pole sana...

Hakuna kabila linapenda mahari kama Wamaasai wakifuatiwa na Wachaga...

Kama hujajipanga unaweza toka jasho la ulimi...
 
Back
Top Bottom