Msaada akaunti ya bolt kufungiwa

Msaada akaunti ya bolt kufungiwa

aBuwash

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2023
Posts
310
Reaction score
558
Habarin wana JF

Naomba nieleze kidogo changamoto yangu iliyonikumbuka Wenda Kuna wajuzi wanaweza nisaidia ndani humu.

Mwezi wa tano nilisafiri kwenda mkoa kwaiyo nilikuwa na pkpk ambayo ilikuwa inafanya shughuli za bolt kwa ajiri ya kujipatia kipato

Basi Kuna kijan nikamuachia pikpk aendelee kunipa hesabu kipind ambacho sipo lakin badae dog akawa analalamika hali ngumu wateja hamna anatak nimfungulie bolt mim nisivyo na hiana nikaamua kumpa akaunt yangu aendelee kufanya biashara.

Sasa baada ya wiki akaunt ikawa inahitaj face verification yeye bila kujua akaweka sura yake kama mara tatu hivi bila kujua na badae ikapelekea akaunt yangu kufungiwa

Juzi nimeenda makao makuu bolt wameniambia kwamba hiyo ndo basii haiwez funguliwa Tena mpka wazungu wenyewe watakapoamua kuifungua
Ety wao hawana access ya kuifungua

Ombi langu kama Kuna mtu asahawah pata changamoto kama hiii na uliwezaje kuisolve. Maana maisha ya boda bila bolt ni magumu sana aiseee
NAOMBENII MSAADA wenu

Screenshot_20260623-140031.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom