MSAADA: Afisa Utumishi amegoma kusitisha makato yangu hata baada ya kuwasilisha barua ya kusimamisha makato hayo kutoka benki

mfate42

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
3,797
4,316
Miaka miwil iliyopita nilienda kukopa benki fulani hapa Tanzania, na wakatuma deni kwa Afisa Utumishi na deni lilikuwa ni 12M, kilichotokea Afisa utumishi akakosea akaandika bilioni 1.2!

Cha ajabu baada ya kumaliza mkopo benki ikanipa stop deduction nimpelekee afisa utumishi ili aondoe deni kwenye mfumo maana nimeshamaliza, cha ajabu Afisa Utumishi huyohuyo anakataa anasema ni kazi ya benki, narudi benki nawaeleza wanasema wao hawawezi maana wanaohusika ni Halmashauri!

Nimejaribu kuwasilisha hiyo barua kwa Mkurugenzi ila hakuna lililofanyiwa kazi mwezi huu wameendelea kukata, hapa niko njia panda.
 
Ili kutaka kujua mchezo mzima, waambie benki wakueleze. Hiyo pesa inayokatwa inaenda wapi?

Kwa sababu kama bado kuna deductions maana yake hayapotelei hewani, kuna sehemu zinaenda. Je, zinaenda wapi na nani anazipiga?

Kama ni benki, basi wawajibishwe. Kwa sababu wanatumia hela isiyo yao.

Kama zinarudi kwa mwajiri basi mhoji Mhasibu wako pamoja na DED. Watamkemea Afisa utumishi mara moja na kisha omba makato yako ya miezi miwili irudi.

Kila kitu kiende kwa maandishi Mkuu. Usipende sana maelezo mengi. Huyo afisa Utumishi akuandikie barua rasmi kuwa hawezi kusimamisha kwa sababu hana uwezo huo.
 
Huko local gment kuna shughuli. Maafsa utumishi wengi wa halmashauri wana changamoto sana, wanapenda kutukuzwa kama vile wao ndiyo waliosoma peke yao. Fanya mchakato umpeleke hata mahakamani iwe fundisho kwa wengine.
 
Back
Top Bottom