Msaaada wenu waungwana katika hili!

Wakuchakachua

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
346
9
Kuna kaka mmoja alikuwa akimfuatilia rafiki yangu (wote wanafanya kazi) ni kwa muda mrefu atlast dada akaamua kuanzisha mahusiano nae kama wiki tatu zimepita.

Tatizo alilonielezea ni kuwa kaka kila akitoka ofisini lazima apitie bar na kunywa (monday to friday weekend ndo mziki na bar ni time table) kwa binafis yake hapendi hiyo tabia kwani hakuna muda wa yeye kukaaa na BF na kupanga the wayfoward to their life/relation(kama mnavyojua earlystage in relation zinavyokuwa) kwa kuwa akirudi kalewa huku day time ni kaz hawana muda wa kuongea.

Kingine at the first week baada ya kukubali uhusiano aliandaa keki ya kumshukuru huyu mpenzi wake kwa kumpenda ie "just to say thanks for loving me" but huyu kaka hajamlete zawadi yoyote ile so anajisikia vibaya mno

Amesha mueleza kuwa hizo bia za daily sio nzuri hata kwa afya yake ila ameendelea kunywa tu.
Anaomba ushauri je amuache au aendelee maana kama ktk stage hiyo na kaka ndo anabehave hivyo ni bora kumuacha mapema kuepusha maumivu ya moyo wake au mnashauri nini ma great thinker????

ILA anampenda tu na wish yake ajekuwa baba watoto
 
we si useme tu kama ni wewe??

kama kwa mda mrefu anamfuatilia inamaana alikuwa hajua (ulikuwa hujui) kama huyo boyfriend wako ni mnywaji????

wewe ukitoa unategemea kurejezewa???? jifunze kutenda wema uende zako usingoje shukrani!! Aalaaah usiniudhi bure !!
 
asnte kwa thoughts zako
ila si mimi
 
Sasa wewe unataka tuwashauri nini wakati hao jamaa si wanandoa? Huyo mdada tayari ameshagundua tabia ya huyo mme wake mtarajiwa siyo nzuri, kajaribu kumshauri lakini bado hataki kubadirika, sasa hapa anachotaka ni nini tena? Mimi mwenyewe yameshanikuta kama ya huyo mdada. Mimi bado sijaowa, kuna binti nilitokea kumpenda kiasi kwamba huyu binti ndo niliona anafaa kuwa wife wangu, lakini baada ya kumchunguza tabia yake looo! Nilijuta kumfahamu. Nikagundua anatabia ambayo siipendi kabisa! ni mlevi, siyo mwaminifu, hana heshima kwa wazazi wake na majirani n.k kwa vile nilikuwa nampenda nikajaribu kumshauri ili ache hizo tabia lakini wapi! huyo dada ukimwona alivyoumbika huwezi ukaamini kama ana hizo tabia ama kweli uzuri wa m2 siyo sura! Sasa basi, kwa vile lengo langu kwa huyo mrembo ilikuwa kumwoa na tayari nimeshagundua huyo ninayetaka kumwoa hana sifa ninazozitaka, imebidi niachana naye japo nilikuwa ninapenda. Sasa wewe ni nini unachong'ang'ania? Si afadhali umewahi kujua tabia yake kabla hamjaoana? Acha king'ang'anizi!!!!!
 
Kama hata hilo nalo ushauriwe,basi tena!

Ni kweli speaker inaonekana halihitaji ushauri ila mim ni rafiki tu na akamua kunishirikisha ila kwa sisi ladies unaweza mwambia mtu achan nae akahisi tofauti ila akipata ushauri kwa watu wasiomjua ni rahisi sana thts why nikamsaidia ku present hmu kwani na yeye ni member atasoma tu
 
Either way she was asking kwa kuwa ni maapema mno au ni sawa tu yey kufanya maamuzi ya kumuacha just to get various ideas.......
 
Sasa wewe unataka tuwashauri nini wakati hao jamaa si wanandoa? Huyo mdada tayari ameshagundua tabia ya huyo mme wake mtarajiwa siyo nzuri, kajaribu kumshauri lakini bado hataki kubadirika, sasa hapa anachotaka ni nini tena? Mimi mwenyewe yameshanikuta kama ya huyo mdada. Mimi bado sijaowa, kuna binti nilitokea kumpenda kiasi kwamba huyu binti ndo niliona anafaa kuwa wife wangu, lakini baada ya kumchunguza tabia yake looo! Nilijuta kumfahamu. Nikagundua anatabia ambayo siipendi kabisa! ni mlevi, siyo mwaminifu, hana heshima kwa wazazi wake na majirani n.k kwa vile nilikuwa nampenda nikajaribu kumshauri ili ache hizo tabia lakini wapi! huyo dada ukimwona alivyoumbika huwezi ukaamini kama ana hizo tabia ama kweli uzuri wa m2 siyo sura! Sasa basi, kwa vile lengo langu kwa huyo mrembo ilikuwa kumwoa na tayari nimeshagundua huyo ninayetaka kumwoa hana sifa ninazozitaka, imebidi niachana naye japo nilikuwa ninapenda. Sasa wewe ni nini unachong'ang'ania? Si afadhali umewahi kujua tabia yake kabla hamjaoana? Acha king'ang'anizi!!!!!

Ni ushauri mzuri na unabusara
 
Mwambie wa kufanya maamuzi sahihi ni sasa maana baadae mtatuletea tena Ooh! Mume mlevi sana ila nashindwa kuondoka wanangu watateseka and blah blah. Mwambie Its now or NEVER.
 
Keki ya kumshukuru???? wanaume wetu w ibongo wengi hawajazoez mambo kama hayo na zawadi ndio kabisaaaa hivo nenda nae taratibu huku ukimwambia hupendi nini na unapenda nini mwisho kama anakupenda atabadilika
 
Gaga siku nyingine unaongeaga point!!!
 
Keki ya kumshukuru???? wanaume wetu w ibongo wengi hawajazoez mambo kama hayo na zawadi ndio kabisaaaa hivo nenda nae taratibu huku ukimwambia hupendi nini na unapenda nini mwisho kama anakupenda atabadilika

Gaga u made this day thanks for your advice hope naye anasoma
ubarikiwe
 
Back
Top Bottom