Nimetumiwa CV ya Prof. Maji Marefu kutoka kwa mpiga kura wake ambaye hakutaka jina lake litajwe ili asije wehuliwa na Mb huyo. Nayo iko hivi:
Jina kamili: Steven Hilary Ngonyani a.k.a Prof. Maji Marefu
Alikozaliwa: Shamba Kapori, Mruazi Kata ya Mnyusi, Wilaya ya Korogwe
Asili yake. Mngoni. Wazazi wake walikuja kama Manamba Mashamba ya Mkonge.
Elimu: Aliishia darasa la 4 kwa kukosa ada ingawa anadai kafika darasa 7
Uzoefu wa kazi: kulima miraba mkongeni, kucheza goroli, kupiga ndege kwa manati, kuchezesha mazingaombwe hasa shule za msingi.
Dini: Mkristo lakini ana wake 4.
Kiini cha kuchaguliwa: Kumwaga pesa kwa zaidi ya miaka 3 kabla ya uchaguzi, kugharimia mazishi na shereha kabla ya uchaguzi.
Yajapo mengine nitawajuza.