Mrisho Ngasa aikacha Simba

Mrisho Ngasa aikacha Simba

Nilimshuhudia Mrisho Ngasa siku alipocheza mechi Taifa, alikimbilia Upande wa yanga, Akashangilia sana Goli alilolifunga, Akapewa JEZI YA YANGA NA MNAZI WA YANGA, Akaivaa, Simba walishuhudia hlilo. Ina maana kweli hakuna mtu mwenye Uwezo wa kufikiri simba, na kuelewa maana ya Kuvaa jezi ya timu nyingine, ukiwa uwenjani unacheza na timu nyingine. Nadhani viongozi wa simba WALIKUWA WANAWAZA na si KUFIKIRI wakati wanamsajili Ngasa. Yanga walimuachia Ngasa akachume, na Arudi nyumbani kwa Muda utakaotaka.
Ndo maana Mzee Hassan Dalali(Mwenyekiti wa zamani wa Simba) kaamua kurudi shule na mwaka huu yuko Form III
 
Mrisho Ngassa si mchezaji bali ni mwana mazingaombwe kama walivyo karibia 99% ya wachezaji wa Simba na Yanga. Mtu yeyote mwenye sifa ya ukocha hawezi kumpanga Ngassa kwani hana any talent zaidi ya kukimbia tu uwanjani. Wachezaji wazuri wako mikoani si hawa wana mazingaombwe wa Simba na Yanga.

Sizitaki mbichi hizi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
 
Taarifa za hivi punde zinadai kuwa Mchezaji Mrisho Ngassa ameamua kuachana na timu yake ya Simba na kurejea Dar es Salaam bada ya kuzozana na mmoja wa viongozi wa timu hiyo kutokana na kufungwa na Mtibwa Sugar mabao 2-0.

Picha hii inaashiria hali ya hatari kwa wekundu wa Msimbazi na hasa ikizingatiwa kwamba tayri Klabu hiyo imepoteza mwelekeo na sasa inayumbayumba,

Wajameni okoeni hili kabla ya jahazi kuzama.

Source:Redio free Africa michezo.

Kwetu sisi tunazidisha sala ili waendelee kusabaratika zaidi kwani vita ya panzi ndiyo neema ya kunguru. Na bado huo ni mwanzo tungoja wakakutane na kisango cha watoto wa ROCKCITY ndipo watapukutika zaidi kama majani ya mkungu.
 
Huyo ametangulia tu Dar kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mapinduzi siku ya kesho pale msimbazi kwa kumfukuza fisadi Aden Rage.

Kwani Rage kawaibia nn? Kama ni uwanja si anajenga au kala hizo pesa?
 
Rage kaomba taarifa toka benchi la ufundi ili atoe uamuzi. Milovan huenda akatimuliwa kwani kabla ya mechi ya Azam alipewa mechi 4, bado mechi moja.
 
Ngasa hasingekubali kupelekwa Simba kwa lazima
 
Jamani mnamlaumu Ngasa bure mwenyewe hakuwa tayari kuichezea Simba,kila wanachofanya viongozi wa Simba yeye kwake anaona ni mauzauza tu.
 
Back
Top Bottom