Mrisho Ngasa aikacha Simba

Mrisho Ngasa aikacha Simba

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
4,225
Reaction score
869
Taarifa za hivi punde zinadai kuwa Mchezaji Mrisho Ngassa ameamua kuachana na timu yake ya Simba na kurejea Dar es Salaam bada ya kuzozana na mmoja wa viongozi wa timu hiyo kutokana na kufungwa na Mtibwa Sugar mabao 2-0.

Picha hii inaashiria hali ya hatari kwa wekundu wa Msimbazi na hasa ikizingatiwa kwamba tayri Klabu hiyo imepoteza mwelekeo na sasa inayumbayumba,

Wajameni okoeni hili kabla ya jahazi kuzama.

Source:Redio free Africa michezo.
 
Kufuatilia soka la Bongo ni kujitafutia maumivu ya kichwa, haiwezekani timu ikifungwa badala ya kuuongeza juhudi ili warekebishe makosa wanaanza kutafutana uchawi, na matokeo ya soka yanafahamika, KUFUNGA,KUFUNGWA NA SARE kitakachopatikana katika hayo ni lazima kukubaliana nacho na kujiandaa na hatua nyingine......kwa wabongo sio.
 
Mrisho Ngassa si mchezaji bali ni mwana mazingaombwe kama walivyo karibia 99% ya wachezaji wa Simba na Yanga. Mtu yeyote mwenye sifa ya ukocha hawezi kumpanga Ngassa kwani hana any talent zaidi ya kukimbia tu uwanjani. Wachezaji wazuri wako mikoani si hawa wana mazingaombwe wa Simba na Yanga.
 
Soka letu linakuwa la vituko na vitimbwi tupu.Uswahili umezidi.Yaani mchezaji mwenye mkataba na timu anaweza kuaamua tu kuikacha timu? Mkataba wake unasemaje? Kiongozi ameanzaje anzaje kumzonga mchezaji kisa timu kufungwa? Mipaka yao ikoje?

Hizi timu zetu haziamini kufungwa kabisa katika maisha yao. Kufungwa lazima watafute lawama na chokochoko. Kesho utasikia wanachama wanataka kufanya mapinduzi ya uongozi. Ni ujinga juu ya ujinga. Vile vizee vya Msimbazi vinavyoshinda klabuni vimevaa malapa vikiamua hakuna anayebadili. Soka la majungu, fitina na ushirikina mtupu.Hatutaa tuendelee, kuwafuatilia hao wendawazimu ni kupoteza muda tu
 
hiyo pcha ikowapi?..............................
 
Dah, kweli ukinza kwa kucheka kikija kilio inauma.
 
Kufuatilia soka la Bongo ni kujitafutia maumivu ya kichwa, haiwezekani timu ikifungwa badala ya kuuongeza juhudi ili warekebishe makosa wanaanza kutafutana uchawi, na matokeo ya soka yanafahamika, KUFUNGA,KUFUNGWA NA SARE kitakachopatikana katika hayo ni lazima kukubaliana nacho na kujiandaa na hatua nyingine......kwa wabongo sio.
UMEONGEA POINT NZURI SAAANAH! siku zote maendeleo ni kufanyia kazi makosa na sio kusaka mchawi. Yanga walifungwa na Mtibwa 3-0 wakabadili kocha haraka sana leo wapo pazuri. Simkoko wakati kaipeleka Tafa star ethiopia katika challenge cup miaka kama sita iliyopita ni kocha aliyewahi kukubali udhaifu wa fomesheni yake ulioifanya Rwanda itushinde. Alifanyia makosa ufundishaji wake na leo ni kocha anyaefanya vizuri katika makocha wazalendo.

Simba wafanyie kazi makosa ikiwabidi hata kubadili kocha. Na ikitaka kubadili kocha , isifanye makosa ya azam, yaani kuleta boga na kutoa mlango wa chuma ili mwizi asiingie ndani. Yaliyowakuta wanayajua wenyewe mpaka wakamrudisha kocha wao wa zamani. Simba kwanza lazima wajiulize, kwa nini hawashindi ugenini?
 
Huyo ametangulia tu Dar kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mapinduzi siku ya kesho pale msimbazi kwa kumfukuza fisadi Aden Rage.
 
huyo kiongozi kama ni kweli amekwaruzana na Ngassa basi ni mpumbavu, hana maadili ya uongozi na hafai kuendelea kuwa kiongozi wa Simba, kwa mpira wa leo Ngassa hastaili kulaumiwa hata chembe.
 
huyo kiongozi kama ni kweli amekwaruzana na Ngassa basi ni mpumbavu, hana maadili ya uongozi na hafai kuendelea kuwa kiongozi wa Simba, kwa mpira Ngassa hastaili kulaumiwa hata chembe.

Eti eeh!

Ni Rage mkuu, je utafuta kauli?

Shida ya Simba ni kucheza mpira mdomoni. Ligi ilipoanza mlichonga utafikiri mmecheza fainali vile
 
niipeleke wapi mkuu,mbona unakuwa na tabia ya kunyanyapaa thread za wenzako mkuu??!!!!

hili ni jukwaa la siasa na si jukwaa la michezo, ukielekezwa jambo jema busara kusikia na kujifunza, tuache ubishi ujana.
 
Mrisho Ngassa si mchezaji bali ni mwana mazingaombwe kama walivyo karibia 99% ya wachezaji wa Simba na Yanga. Mtu yeyote mwenye sifa ya ukocha hawezi kumpanga Ngassa kwani hana any talent zaidi ya kukimbia tu uwanjani. Wachezaji wazuri wako mikoani si hawa wana mazingaombwe wa Simba na Yanga.
Timu pamoja na wachezaji wa hizi timu hawajitambui,wanadaganyana eti sasa hivi tuanze 'professional league',wakati kilabu hazina mipango endelevu!!!,wahezaji hawana malengo;mafunzo wa makocha hawazingatii,wanapika majungu wakipewa mazoezi magumu mpaka makocha wanatimuliwa kazi.!!!
 
huyo kiongozi kama ni kweli amekwaruzana na Ngassa basi ni mpumbavu, hana maadili ya uongozi na hafai kuendelea kuwa kiongozi wa Simba, kwa mpira wa leo Ngassa hastaili kulaumiwa hata chembe.

viongozi hawana nia ya kuongoza,hataki kutafuta tatizo la kufungwa wanatafuta mtu wa kumsingizia.!!
 
Eti eeh!

Ni Rage mkuu, je utafuta kauli?

Shida ya Simba ni kucheza mpira mdomoni. Ligi ilipoanza mlichonga utafikiri mmecheza fainali vile
sifuti kauli, huyo Rage anasogeza siku tu za kuwa Mwenyekiti wa Club tukiamua hata sasa hivi tunamtanguliza...tu huko, ngoja kwanza arudishe pesa alizompatia Mbuyu Twite kinyume na taratibu.
 
Back
Top Bottom