Mrisho mpoto

ni kweli kabisa....mafumbo yanapokua mazito mno, panakua na udhaifu wa mwandishi japo amefanya kazi nzuri!
Lakini pia Shaaban Robert alikua na mafumbo mengi na mazito japo miongoni mwake, yaling'amuliwa na hadhira yake.

"Mjomba wewe si uliwapaka wanja ngoja wao wakupake pilipili afu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga"

hapo kwenye RED nimeelewa kwamba, Kiongozi Mkuu amekua akiwalea lea watu fulani, ilhali watu hao si wema. Matokeo yake sasa wao huenda wakaja kumsababishia matatizo katika uongozi wake kiasi cha kumfanya kumwona adui, anayetaka kumharibia...kwa maana ya kombolela unapozinga unapaswa kumzuia adui asibutue!
Hii inamuhusu Jakaya Kikwete! Walioko chini yake ndio wanaomungasha!
 
anaweza tukawa hatumpendi kwa unafiki wake na undumilakuwili... ile angesimamia kile anachoimba, nafikiri angekuwa kweli mwanamapinduzi....!
 
Mimi napenda mnapotoa hoja basi iwe nzito. NIPENI SABABU KWANINI JAMAA NI MNAFIKI?. Ingawa c mfuatiliaji sana bt kuna kaelimu hapa nataka kupewa. Kwanini mnamchukia?
 
Hii inamuhusu Jakaya Kikwete! Walioko chini yake ndio wanaomungasha!

Hii kauli naonaga km ni ya kumtetea sana na kumbeba JK inamaana yeye hajui km flan utendaj ni mbovu? Sasa km hajui yuko hapo km nani na yy ndo mwenye dhamana ya mwisho na ndo aliyemchagua? HII KAULI SIIPENDI SANA IKO KISIASA MNO!
 
tatizo hampendi kuumiza akili wa TZ ndo maana hakuna maendeleo kl kt utafuniwe -----
 
tatizo hampendi kuumiza akili wa TZ ndo maana hakuna maendeleo kl kt utafuniwe -----
wanataka watafuniwe kila kitu, hawapendi kabisa kuumiza vichwa,chukua mfano mr zero kasema rasimu ipo okey wooote wameitikia wito na kuifiki bila hata kuisoma
 
Mimi napenda mnapotoa hoja basi iwe nzito. NIPENI SABABU KWANINI JAMAA NI MNAFIKI?. Ingawa c mfuatiliaji sana bt kuna kaelimu hapa nataka kupewa. Kwanini mnamchukia?

Mrisho upande wangu nilimdharau na kumpuuza siku alipoenda kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya kiswahili na akajitambulisha kuwa yeye ni mKenya..ana njaa zaidi ya kicheche muuza ishu
 
.... SIJUI HUWA ANAVAA MAGAUNI, gunia AU U PRIMITIVE tu unamsumbua....

... mnafiki sana huyo...

Eti anajifananisha na watu wa enzi za Yesu.
Wale walikuwa wanavaa nguo safi, yeye magunia ya midabwada sijui anaiokotea kwenye mitumba ya Soko gani!
 
ni kweli kabisa....mafumbo yanapokua mazito mno, panakua na udhaifu wa mwandishi japo amefanya kazi nzuri!
Lakini pia Shaaban Robert alikua na mafumbo mengi na mazito japo miongoni mwake, yaling'amuliwa na hadhira yake.

"Mjomba wewe si uliwapaka wanja ngoja wao wakupake pilipili afu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga"

hapo kwenye RED nimeelewa kwamba, Kiongozi Mkuu amekua akiwalea lea watu fulani, ilhali watu hao si wema. Matokeo yake sasa wao huenda wakaja kumsababishia matatizo katika uongozi wake kiasi cha kumfanya ashindwe kumwona adui, anayetaka kumharibia...kwa maana ya kombolela unapozinga unapaswa kumzuia adui asibutue!

Binafsi namheshimu sana kijana huyu na siwaelewi kabisa wanaosema eti anatunga mafumbo ambayo hata mwenyewe hayaelewi! Huu ni wivu usio na maana wala faida kwa Taifa . Yeyote mwenye nia njema na tafakuri nzuri anaweza kuelewa ujumbe wa kijana huyu ambaye mashairi yake hubeba mafundisho na ujumbe muhimu katika jamii. Mfano ni kama hiyo verse uliyoinukuu mkuu.
Mashairi yake yanapendwa ndani na nje ya Tanzania na nimeyasikia pia Burundi, DRC, Kenya, Uganda na sehemu kadhaa nilizotembelea Kiswahili kinakozungumzwa. Sina uhakika kama wanaomponda sana uwezo wa kughani tunzi kama zake.
 
me ndo naijua definition ya huo mvuto ambao amekosa so hao kina sukar ni wenu. Mwanaume mbaya ka utando wa uji wa ulezi uliolala, tifutifu ka furushi la magimbi loh na huo unakfi wake bhaaassss ful kinyaa

Jamaa kajisahau sana, anajua kula tu kufanya mazoezi ya kupunguza unene hajui.
 
Jamaa yuko vizuri sana namkubali

Nakumbuka alishawahi kukutana na Mzee mmoja mwanamashahiri mkongwe, yule mzee alimwambia Mpoto kuwa mashairi anayoimba siyo. Akamwambia kuwa Vina na Mizania haviendani kabisa na kanuni za mashairi, Mpoto akaishia kusema kuwa yakwake ni ya kisasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom