Ebu Tuone na Kusikiliza hii Single ya Mrisho Mpoto Chocheeni Kuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ebu Tuone na Kusikiliza hii Single ya Mrisho Mpoto Chocheeni Kuni

Discussion in 'Entertainment' started by kibogo, Oct 24, 2012.

 1. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Chocheeni kuni moto uwake ugali uive mnachotaka kitokee
  Halikeni mamruki, wakija wangojee, mikeka wawekee
  Wanachotaka kitokee
  Chochea X 8

  Watanzania mwenda kwao siku zote haogopi giza
  Acheni nirudi nyumbani safari imenishinda
  Nauri zenu ntarudisha

  Mtu anatapika nyongo yake anairamba tena anaangaliwa
  Ni sawa na tawi kavu linapoanguka watu wakapiga kelele ‘’Hayaaaa”
  Katika misimu minne kwa mwaka tuongeze msimu mwingine wa tano wa kujistusha

  Raha ya janvi siku zote ni viraka viraka na dungu linamficha mlinzi wa ndege wakati wa mvua tu.
  Eti ooh imenyesha juzi tu maji sio mengi nisubirini kule!
  Ilishindikana vipi kuyapima maji kwa mti ndo muwaambie watu wavuke?

  Mjomba! Binadamu ni kama ganda la kitabu mpaka umfungue maandishi ndiyo uweze kumuelewa.
  Eti lililotokea mbali tufanye limepita na haliwezi kumdhuru mwingine ‘kweli’

  Inayotaka kunyesha huwa haisubiri mawingu,
  Mi sidhani kama kujiponya katika mambo mazito tunahitaji cheti kilichogongwa muhuri wa moto au mtaalamu wa magonjwa ya akili, zaidi ya kutumia neno sahau tu,
  Unawaulizaje watu magongo ya nini wakati unasema kuna nyoka?

  Mjomba! We si uliwapaka wanja ngoja wao wakupake piripiri harafu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga.

  Mngekuwa mnajua anachokuala nyuki msingethubutu kusema asali ni tamu,
  Niwashukuru kwa kufikiri, kwani mmeonyesha ukomavu wa kutoka chini kwenye shingo na sio juu.

  Mbona hamkumfikiria aliyekuwa ndani kafungiwa kwa nje usingizi hapati anawaza jinsi ya kutoka?
  Nikisema uwezo wa watu kufikiri na mahitaji vinatofautiana mtaanza kusema ninadharau, nina matusi lakini kumbukeni ulimi unauma kuliko meno,
  Mnawezaje kumfikiria aliyekuwepo ndani kajifungia mwenyewe, funguo anazo mwenyewe, kalala fofofofo asijue hata idadi ya misumari iliyoshikiria mlango wake?

  Kulipamba jeneza kumfanya aliyekufa kufufuka nini
  Kama kusema nimekwisha sema sana mwisho wake ntakuwa kama mwanasiasa
  Hawajitokezi mpaka kuwe na maafa”NTATOA KATON 20 ZA SABUNI YA UNGA’ aliyekuambia wale ni wachafu nani, kasafisheni kwanza nyoyo zenu ndiyo mrudi kwa wananchi.
  Ndugu zangu tawi kavu kuanguka wala sio ajabu
  Wakati wao wanatenganisha mavi ya panya kwenye unga nyinyi chocheeni kuni zilizolowa, maji yapate moto ugali usongwe,
  Wakiwauliza waambieni huu ni utani, hapa kwetu tuna makabila 120 tunataniana

  Waliopo hatuwataki, wanaotaka tuwape hatuwaamini
  Maneno siku zote yanauma na yanachefua ukielewa maana yake.
  Kwa mfano neno la kitoto kumwambia mtoto tunasema watoto wanacheza
  Neno la kitoto kumwambia mkubwa tunasema mtoto anakua
  Mtoto akisema baba ile ndege yangu, baba hata kama hana biskeli umwambia ikitua ntakuletea. Lakini maneno ya kitoto mtu mzima kumwambia mtu mzima kunawalakini

  Mimi safari imenishinda na sitaki kuulizwa tena kwa nini.

  Chocheeni kuni moto uwake ugali uive mnachotaka kitokee
  Halikeni mamruki, wakija wangojee, mikeka wawekee
  Wanachotaka kitokee
  Chochea X 8
   

  Attached Files:

 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  ..Makubwa!
   
 3. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maskini Weeeh! Mpoto Amerudisha nauli zetu....
   
 4. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  mjomba wewe si uliwapaka wanja wakati wanakuja? sasa ngoja wao wakupake piripiri harafu kwenye kombolela iwe zamu yaku kuzinga. mia
   
 5. Mfarisayomtata

  Mfarisayomtata JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 419
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  jamani mrisho nenda basi au tukupe nauli ya ndege.
   
 6. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  maajabu mengine ya dunia, watalii waje watembelee kuona waziri wa elimu elimu imempita na wanafunzi wake 5ooo hawajui kusoma na kuandika lakini wapo sekondari. wapi tena duniani hili liliwahi kutokea??
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mesej kwa mkwe re
   
 8. f

  filonos JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  duuuuu WEEE BWANAEE MPOTO AMETUTOSA mmmm balaaaa lishaanza.....Tusubili matikeo....
   
 9. N

  Nyakwec's Bro JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  hahahahaha,inawezekana mjomba ameshapigwa pilipili ndy maana haoni watu wanabutua tu!..

  Mjomba We si uliwapaka wanja ngoja wao wakupake piripiri harafu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga.
   
 10. k

  kisilo Senior Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kibogo ww nmkali,saluti.mpoto afadhal kurud using'ang'anize
  safari wakati hali nimbaya.100
   
 11. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  waliopo hatuwataki na wanaokuja hatuna imani nao.

  mpoto anahitaji kujengewa uwezo ili aielewe chadema.
   
 12. M

  Mundu JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ...hahaha usiombe kucheza kombolela, afu kichaka cha kujifichia kiwe karibu. Kila wakati watakuwa wanabutua...

  Watoto wa siku hizi hawajui hata maana ya kombolela...

  ndo mana walisema...ngoma ya kitoto haikeshi

  Mwenye masikio na asikie
   
 13. T

  Tetra JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Rudi tu mjomba tulijua safari ni nzito.
  NAULI YANGU NUNUA MAJI UNYWE,
  Karibu Karibu Si kila asafirie hupata alichofuata
   
 14. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Asante kwa mistari
   
 15. M

  Mr.creative JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ooh! Mjomba tumeshakata tamaa sasa kulikoni au tukupe ungo upae nao ili ufike fasta?
   
 16. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,534
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Mjomba pole sana,tulikwambia safari huiwezi ukasema tuna gubu,mara hatuna malezi ya baba na mama,leo umekiri mwenyewe safari imekushinda! Naomba tu nauli yangu nilokupa ninunue hata yebo yebo mjomba.
   
 17. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja mkuu!
   
 18. Root

  Root JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,217
  Likes Received: 12,928
  Trophy Points: 280
  Jamani audio yake please

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 19. m

  mpigilie JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Lugha anayotumia ni ngumu kueleweka.
  Ujumbe anaoutoa ni mzito kubebeka.
  Wengi wasiomwelewa wanapenda kumsikiliza.
  Wachache wanaomuelewa wanajifanya hawamuelewi.
  Ngumu kumeza lakini ndo ukweli.
   
 20. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Audio ipo kwenye attachment unaweza kuisikiliza mkuu.
   
Loading...