Mrisho Gambo: Wapinzani watapotea

Mrisho Gambo: Wapinzani watapotea

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kusema kuwa wapinzani wa Tanzania kama hawatabadili aina ya siasa wanazozifanya sasa basi watapotea kwani serikali ya awamu ya tano imepata Rais ambaye hataniwi na wala hatishiki.

Gambo amesema kuwa wapinzani baadala ya kuanza kupiga porojo zisizo na msingi bali wajipange tu kumsaidia Rais John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano.

"Nataka niwaambie wanasiasa hawa wa upinzani wasipobadilisha aina ya siasa wanayofanya kwa ninavyoiona mimi serikali ya awamu ya tano watapotea, kwa sababu tumepata Rais ambaye hatanii, unajua wameshazoea wengine wakitishwa tishwa kidogo wanaingia mitini huyu Magufuli akinyooka amenyooka, ananyoosha rula tu utaamua mwenyewe ukae kushoto au kulia. Kwa hiyo mimi niwashauri tu itakuwa vizuri badala ya kupiga porojo wajipange kumsaidia Rais aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano" alisema Gambo

Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Arusha amesema kuwa kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kutaka kuikwamishan serikali basi watadili naye asubuhi mchana na jioni.

"Kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kuikwamisha serikali isitekeleze malengo yake nataka niwahakikishie kwa uwepo wangu hapa tutahangaika naye asubuhi, mchana na usiku kwa mbinu zote zile, kama wanataka porojo wasubiri 2020, sasa hivi kama wanataka tusaidiane kupeleka huduma na maendeleo kwa watu, haiwezekani tukawa na serikali au nchi ambayo kila siku ni porojo tu, kila siku siasa" alisisitiza Mrisho Gambo

Chanzo: EATV

My take:

Kwa kauli hizi, Wakuu wa mikoa na Wilaya wapo kwaajili ya kupoteza upinzani sio kuketa na kusimamia Mendeleo.

Inawezekana vipi mkuu wa mkoa asijue umuhimu wa wapinzani? Sipati picha wajumbe wa nyumba kumi watafanyaje. Wanasiasa wetu hawana elimu ya siasa.

Wnachukulia vyeo kama zawadi na wamesahau cheo ni dhamana. Juzi kati Nape alikuwa anapinga bunge live lakini leo analilia bunge live. Huu ni mfano wa kwamba maisha hupanda na kushuka. Tutende haki bila kumuonea mtu wala kumuogopa Mtu. Acha na yule mkuu wa mkoa anayeharibu shamba la mwanchadema na kuacha shamba la mwanaccm waliyepakana naye.
Kashiba rambirambi huyo.
 
Msimlaumu sana kwani upeo wake wa kufikiri umegotea hapo! Anajidanganya na au hajasikika siku nyingi kwenye media ndio kaona atoke kivile.
Huenda anataka kujua kama mmesahau zile rambirambi alizopiga na vile alivyokimbia msiba wa mzee wetu kule Moshi.
Asifikiri watu wa Arusha wamelala kama wa kule kwao. Ipo siku watayaamsha madude na ataikimbia Arusha bila viatu. Ni muda tu haujafika!
 
Kilichopotea ni CCM, haipo tena, it's a one man show/big man rule.

Hakuna taifa in modern democracy ambalo upinzani ulipotea/umepotea/utapotea. Kilichopotea/Kinachopotea/kitachopotea ni utawala unao kiuka haki na demokrasia. Magufuli's regime is a sinking ship, any rational thinker analiona hilo kwa uwazi kabisa.

Tupo kwenye kipindi cha mpito ambacho on second thought, it was necessary kwa taifa kupata ukombozi na kuondokana na minyororo ya CCM. Ni suala la Muda tu.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kusema kuwa wapinzani wa Tanzania kama hawatabadili aina ya siasa wanazozifanya sasa basi watapotea kwani serikali ya awamu ya tano imepata Rais ambaye hataniwi na wala hatishiki.

Gambo amesema kuwa wapinzani baadala ya kuanza kupiga porojo zisizo na msingi bali wajipange tu kumsaidia Rais John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano.

"Nataka niwaambie wanasiasa hawa wa upinzani wasipobadilisha aina ya siasa wanayofanya kwa ninavyoiona mimi serikali ya awamu ya tano watapotea, kwa sababu tumepata Rais ambaye hatanii, unajua wameshazoea wengine wakitishwa tishwa kidogo wanaingia mitini huyu Magufuli akinyooka amenyooka, ananyoosha rula tu utaamua mwenyewe ukae kushoto au kulia. Kwa hiyo mimi niwashauri tu itakuwa vizuri badala ya kupiga porojo wajipange kumsaidia Rais aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano" alisema Gambo

Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Arusha amesema kuwa kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kutaka kuikwamishan serikali basi watadili naye asubuhi mchana na jioni.

"Kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kuikwamisha serikali isitekeleze malengo yake nataka niwahakikishie kwa uwepo wangu hapa tutahangaika naye asubuhi, mchana na usiku kwa mbinu zote zile, kama wanataka porojo wasubiri 2020, sasa hivi kama wanataka tusaidiane kupeleka huduma na maendeleo kwa watu, haiwezekani tukawa na serikali au nchi ambayo kila siku ni porojo tu, kila siku siasa" alisisitiza Mrisho Gambo

Chanzo: EATV

My take:

Kwa kauli hizi, Wakuu wa mikoa na Wilaya wapo kwaajili ya kupoteza upinzani sio kuketa na kusimamia Mendeleo.

Inawezekana vipi mkuu wa mkoa asijue umuhimu wa wapinzani? Sipati picha wajumbe wa nyumba kumi watafanyaje. Wanasiasa wetu hawana elimu ya siasa.

Wnachukulia vyeo kama zawadi na wamesahau cheo ni dhamana. Juzi kati Nape alikuwa anapinga bunge live lakini leo analilia bunge live. Huu ni mfano wa kwamba maisha hupanda na kushuka. Tutende haki bila kumuonea mtu wala kumuogopa Mtu. Acha na yule mkuu wa mkoa anayeharibu shamba la mwanchadema na kuacha shamba la mwanaccm waliyepakana naye.
Mwambieni aweke akiba ya maneno. Tena mkumbusheni hapa duniani hakuna umilele. Kila mtu ataondoka pamoja na yeye.Lakini swali moja tu. Wapinzani watapoteaje?
 
Atapotea yeye kwenye siasa kwa kutegemea vyeo vya kupewa na mtu awaulize walio mtangulia wako wapi?
Mimi huwa nawasikitikia sana vijana wenzangu wenye fikra za aina hii. Kwanza they are in the wrong side of history, it doesn't need one to be a brain surgeon kutambua kwamba future ya Taifa letu- CCM is no where to be found. Lakini pili na muhimu zaidi ni kwamba hizi kazi za kuteuliwa Muda wake ukiisha utafanya nini bado ukiwa na nguvu nyingi chini ya umri wa miaka 50? Angalau basi uwe na PhD yako kwani hautakosa kazi hata ya kufundisha masuala ya uongozi baada ya kupata uzoefu kupitia nafasi hizi.

Tutakutana nao mitaani kwani wengi hata wa awamu iliyopita tupo nao mitaani na Sasa wanatuelewa vizuri sana tulikuwa tuna maanisha nini. Watakuja tu.
 
kijana amelewa madaraka, anadhani atatawala milele. yalikuwepo madikteta shababi Leo yako wapi akina Mobutu, nduli iddi amini, ghadafi n.k
 
NI MPUUZI NA MJINGA TU NDIYE ANAYEOMBEA VYAMA VYA SIASA VIPOTEE.
 
Hawa watoto wa ajabu sana. JK aliwainua leo wanamsema hivi? Halafu wanaelewa kweli upinzani maana yake ni nini?
 
Hahahahah, CCM ndiyo chama pekee duniani, hakuna anayebisha. Si ulisikia Mh. Rais alipoita mwenyekiti yeyote aliyepokea mwanachama toka CCM kuhamia upinzania, ila wapi, hakuna aliyejitokeza, hahahaha, wewe ndiyo zuzu, njoo CCM!
Kasome uandike upya, bk 2 zipo.
 
Endelea kujitekenya na kucheka mwenyewe!Upinzani uliopotea hauzungumzwi kila siku
Upinzani uliopo ni masalia. Yaani hauna jipya. Yaani ulishakufa siku nyingi mno. Tz hatuna upinzani. Rais aliposema mtu yeyote aliyepokea mwanachama/wanachama wa CCM aje awapokee pale kibaha mbona walikosekana? Yaani chama sasa ni CCM tu!
 
Kajisahau sana, waliokula kwa kikwete sasa wako wapi? miaka kumi ni kama second, anaweza kimbia nchi asipojiangalia mkuu wa mkoa is just a normal person at any time t!
 
Ndo yale yaupo uringoni unapigana na mtu uliemfunga pingu.... Alafu unajisifia umeshinda pambano
 
Gamboooooooo

Chama cha siasa sio kabila unaweza ukanyanyaswa huko uliko na ukahamia upinzani

Ukiondoa huo uRC wako wewe ndani ya chama dola sio chochote
Aminitu kwamba unaweza kuamka na cheo hicho usilale nacho
 
Upinzani uliopo ni masalia. Yaani hauna jipya. Yaani ulishakufa siku nyingi mno. Tz hatuna upinzani. Rais aliposema mtu yeyote aliyepokea mwanachama/wanachama wa CCM aje awapokee pale kibaha mbona walikosekana? Yaani chama sasa ni CCM tu!
Hahahhaaaaaaa,yaani mkutano wa ccm unatafute viongozi wa CDM!Na sisi tukiitisha mkutano,tukauliza wa ccm ambao wamepokea wapinzani atapatikana hata mmoja wa kujitokeza?Hoja za kipuuzi kabisa!!!!!!
Kama kweli upinzani umekufa,hahahhahaa,kama umekufaa kweli,teh teh teh,kama mnaamini umekufa kweli,hahahhaaaaaaaaa
-"Mwambieni JPM aruhusu mikutano ya siasa watu wamwagike"

Lakini kila siku mnapiga kelele upinzani umekufa ila mnatumia nguvu kubwa kuwadhibiti,nawafananisha na yule generali wa nchi ile ambaye alikuwa anatangaza nchi yake inaelekea kushinda vita huku wamezidiwa kila kona!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom