Mrisho Gambo ni Rais ajaye

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,348
14,621
Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo ameonyesha siyo mnafiki na yuko tayari kukataa hongo hata kama hiyo rushwa anapewa na viongozi wake wa chama.
Kitendo cha kuanika hadharani ufisadi uliokuwa unafanywa na mkurugenzi wa jiji la Arusha pamoja na katibu wa ccm ni cha kijasiri mno na upekee wa hali ya juu sana , kumbuka waziri mkuu Kassim Majaliwa amethibitisha ufisadi huo kwa kuwasimamisha kazi wahusika na kuiagiza Takukuru iingie mzigoni mara moja .

Kama ilivyo ada ili nchi iendelee ni lazima iongozwe na mtu ambaye siyo mnafiki na msema kweli daima , Mrisho Gambo ameonyesha hilo kwa uwazi kabisa, na kuwa Tanzania ina vijana wengi wa hovyo wapenda ufisadi basi tutarajie kuona Gambo akianza kupigwa vita na kushambuliwa mfululizo licha ya uzalendo wake alioufanya kwa taifa.

Nasihi Mrisho Gambo apewe ulinzi maalum ili mafisadi wasimsababishia shida kwani ameonyesha ni kiongozi mzuri anayeweza kuja kuwa Rais wa nchi yetu.
 
Hivi cheo cha Urais mbona kina najisiwa hivi? Mara kuna dude litazomoka huko na kudai kuwa DAUDI ALBERT BASHITE nae anafaa kuwa presdaa mara Mnyeti hivi kweli mpo serious?
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom