Mrisho Gambo ajijue yeye sasa hivi ni Mbunge sio Mkuu wa Mkoa tena

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Lazima utofautishe ziara za kiutendaji na ziara za kisiasa.

Gambo haya unayolialia uliyatengeneza ukiwa RC Arusha dhidi ya MP/Mbunge godbless_lema.

Leo yanakurejea wewe mwenyewe pole usilie lie,ila Mbunge nafasi yake ni kubwa kuwakilisha wananchi na kuisimamia Serikali (Kuanzia Rais, mawaziri ,manaibu n.k). Ziara zako hazihitaj wataalamu au watendaji wa Manispaa/Halmshauri au Jiji. Ww sikia shida za wananchi zibebe zifikishe sehemu husika.

Yaani Mbunge akifanya ziara yake yeye Kama Mbunge sio ziara za kiutendaji sababu hana mamlaka ya kutenda au kuagiza kitu fulani kifanywe. Ni tofauti na Waziri, Naibu waziri, Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya au Mkurugenzi hawa wanaweza kutembea na watendaji wa idara ktk ziara zao sababu wana mamlaka ya kuagiza (Power of ordering).

Ziara za Mbunge ni ziara za aidha kusikia changamoto za wananchi wake ,kuzibeba na kuzipeleka Sehemu husika (Serikalini) kushawishi Serikali izitatue na kuisimamia Serikali izitatue au ziara za kutembelea miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika Jimbo lake kuona mafanikio na kasoro hivyo kuwasilisha sehemu husika kwa utatuzi zaidi.

Lazima Gambo ajiondoe ktk viatu vya nafasi ya ukuu wa mkoa nafasi aliyekuwepo, sababu sasa hivi yeye sio mkuu wa mkoa ,yeye ni Mbunge hana mamlaka yeye binafsi kutembea na watendaji wa idara au wataalamu wa Halmshauri, Manispaa au jiji katika ziara zake anapotaka yeye bila idhini ya viongozi wa Serikali aidha Mkurugenzi, mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa.

Sababu hao watendaji/wataalamu ni watu wa Serikali wapo chini ya Mkurugenzi, Kama Mkurugenzi hajaridhia wataalamu au watendaji kuambatana na Mbunge ktk ziara zake hilo huwezi lazimisha.Sababu hata wakihudhuria hawawezi pokea maagizo kutoka kwa Mbunge.

Mbili ,Mbunge mamlaka yake ni makubwa sana sio wa kugombana na Mkurugenzi,Mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa ,sababu Mbunge ana nafasi ya kuonana na waziri mkuu mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali, Mbunge ana nafasi ya kuonana na waziri yeyote, Naibu waziri yeyote kuwasilisha changamoto za wananchi wake ktk Jimbo husika.

Lakini Mbunge na yeye ni mjumbe ktk kikao cha Baraza la madiwani hivyo ana nafasi kubwa ya kuwasilisha changamoto alizozisikia na kuzikusanya kutoka kwa wananchi.

Lakini pia Mbunge ni mwenyekiti wa kamati ya fedha za mfuko wa Jimbo ,hivyo ana nafasi ya kushawishi kamati fedha fulani iende Sehemu fulani kutokana na changamoto alizokusanya na kuzisikia ktk ziara zake ili kidogo zikatatue hizo changamoto.

Lakini pia Mbunge ana nafasi ya kupata mtandao mkubwa wa wafadhili kutoka nje au mashirika tofauti kupitia Manispaa au Halmshauri aliyopo na wakaja kutekeleza miradi mbalimbali. Hii njia alikuwa anaitumia saana Mh.@zittokabwe Kigoma mjini.

Zitto alitafuta wafadhili mwenyewe Bil 100 kutoka JICA (Japan) kwa maboresho ya Bandari ya Kigoma ila Serikali tuu ndio ilikwamisha ku saini, Mradi wa Bonde la mto luiche Serikali ya Kuwait (Kuwait Fund ),Bandari ya Ujiji, Barabara za Pavement blocks ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji inayotoa Euros mil.65 Kigoma tu, Mradi wa mchikikichi kupitia wafadhili TradeMark East Africa.

Hii ni mifano dhahiri ya namna Mbunge anaweza tumia nafasi yake katika kutatua matatizo ya wananchi wake.Kulazimisha kufanya ziara pamoja na watendaji/wataalamu wa Halmshauri,Manispaa au Jiji haisaidii kitu sababu hawatafuata agizo la Mbunge ila agizo la Mkurugenzi ambaye ni boss wao,au mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa au kiongozi yeyote mkubwa wa Serikali ila sio Mbunge.

Mnavyozozana na kugombana waziwazi ikiwa nyinyi nyote ni wanachama wa chama kimoja alafu bado mnagombana tafsiri yake nini?, Sababu zamani wabunge wa vyama pinzani walikwamishwa kwa Serikali kutosaini miradi ya wafadhili sababu ni wabunge wa upinzani au Halmshauri/Manispaa ipo chini ya upinzani. Sasa hivi je?

Tutaona mengi ,usipotumia akili ktk kuwakilisha, kutetea na kuisimamia Serikali ktk kuletea wananchi maendeleo Mbunge utaishia kulalamika hatimaye na hutafanya lolote hadi miaka 5 inakwisha.

Rai yangu haina maana RCs, DCs ,DEDs kuingia migogoro isio na maana na Mbunge, Mbunge ajue nafasi yake na hawa viongozi wajue nafasi zao ubaya tunafanya kazi kwa kila mtu kutaka kuonekana kwa mkubwa kwamba anafanya kazi tatizo. Wajibikeni kwa ajili ya wananchi na kwa maslahi yao.


Abdul Nondo.
 
Mbunge nae anataka atembee na wataalamu katika vikao vyake

Yaan daktari, mwalimu, bwana afya, nesi aache kuhudumia wananchi abakie na porojo za kisiasa.

Nadhani wanakosea sana hawa wanasiasa labda kama mmekubaliana tena kwa muda mfupi sana na hao wataalamu

Mbunge kazi yake ni kutembea na kupiga porojo na kupokea kero

Gambo ndio anastuka kuwa cheo chake cha awali kilikuwa kikubwa kuliko hiki alichonacho sasa

Tena ashukuru maana mwenzake wamempaki kama chuma chakavu (screpa)
 
Bandiko lako zuri sana kiongozi. Isipokuwa hapo tu penye hizo takwimu za bosi wako kuhusu miradi na ufadhili siwezi kupapokea bila kujua kiundani.

Mambo mengine yote na hoja yako umeiweka vema na mimi nadhani huyu mbunge wa Arusha huenda ndiye mbunge namba moja CCM walijichanganya. Huenda ndiyo sababu pia alishawahi kutenguliwa ukuu wa wilaya na mkoa!

Huenda CCM wakaanza kujutia kumpa dhamana ya kugombea Ubunge.
 
Alijua kwasababu yeye ndie mbunge lupitia CCM basi atafanya kila atakalo sababu anatoka chama kilichoko madarakani, akasahau kwa kufanya hivyo atakuwa anaingilia mamlaka nyingine za serikali na kusababisha mgongano kati yao.

Atambue tu hakuna jambo lisilo na mipaka yake, ajue mipaka ya ubunge wake ni ipi, asitake kufanya wengine waonekane wanakosea wakati yeye ndie sababu anataka kuwatoa wenzie nje ya mstari kwa mihemko yake ya ubunge alioupigania na kushinda kisanii.
 
Waliona Gwaji boy amezunguka nao, na yeye akaiga kunya kwa tembo, anapasuka msamba .. Aaangalie
 
Mbunge nae anataka atembee na wataalamu katika vikao vyake

Yaan daktari, mwalimu, bwana afya, nesi aache kuhudumia wananchi abakie na porojo za kisiasa.

Nadhani wanakosea sana hawa wanasiasa labda kama mmekubaliana tena kwa muda mfupi sana na hao wataalamu

Mbunge kazi yake ni kutembea na kupiga porojo na kupokea kero

Gambo ndio anastuka kuwa cheo chake cha awali kilikuwa kikubwa kuliko hiki alichonacho sasa

Tena ashukuru maana mwenzake wamempaki kama chuma chakavu (screpa)
Shida yake aliona kama lema anafaidi sana.

Acha alambe umeme kwa mdomo
 
Back
Top Bottom