Seneta Wa Mtwiz
JF-Expert Member
- Sep 23, 2013
- 3,622
- 4,138
Wakuu,
Kama kawaida yangu ya kuamka asubuhi mapema na kuanza kuzungusha mkokoteni wangu wa madumu ya maji nyumba hadi nyumba kitaa cha #madale_mivumoni-
Sasa nyumba ya nne kutoka hiki kibanda cha paa 1 nilipopanga chumba changu kimoja chenye upana wa futi 7 kwa 7,
Kuna dada mmoja ambaye ni afsa mawasiliano wa kampuni moja ya vifaa vya umeme hapa mjini
Kawa mteja wangu mzuri sana wa maji kwani hununua zaidi ya dumu 9 kwa siku na hunipa advansi ya dumu zingine za kesho yake.
Huyu dada ni ile sampuli ya yule dada wa kuiywa [HASHTAG]#witness[/HASHTAG] (yule kibonge wa wakilisha yule),
Yaani kajazia balaaa,
Na ana figa ya maana,
Hips matataaaaa- sio za nchi hii!
-----
Pamoja na kunizoea kibiashara,
Kuna tabia 1 ambayo imenistaajabisha kidogo,
Kuna siku niliwahi kumwomba anielekeze jinsi ya ku_install app. Ya kuonesha eneo ambalo mtu yupo kwenye simu yangu,
Ili inisaidie kuwafikia wateja wangu wa dumu za maji,
Akaniuliza email yangu nikamtajia,
Akashtushwa kidogo kusikia jina langu
seneta wa mtwiz,
Ila akanisetia hiyo app.
Sasa tangu siku hiyo kila nipelekapo maji nyumbani kwake,
Huniomba simu yangu
Anaiangalia sana na kuisifia sana,
Hupenda kujua nimeposti nini kwenye fb, instagramu, jf na hata status za whatsapp,
Yaani anaisifia sana hii simu yangu aina ya tecno p3,
Wakati yeye anamiliki iphone 8.
Imefikia hatua anakuja mpaka kibandani kwangu- anadai kuja kunipa hai na kuiona simu yangu.
--------
Sasa leo nimelala ghetto kwangu mida ya jioni,
Nasikia honi ya gari nje,
Nafungua mlango wangu wa mabati natokea nje
Nakutana na ndinga nyeusi aina ya #nissan_murano,
Kashuka huyu binti kibonge
Ananiambia,
"Excuse me seneta wa mtwiz,
May we exchange the phones please,
I am really fond of your phone-
Trully speaking.
I beg your pardon if it sounds to displease you, my real friend.
Since I am your potential customer,
It can be a good room to enhance our neighborhood as well as friendship if you wont mind."
----
Nikamwambia ngoja nikafanye mpango wa kuchonga laini yangu ya airtel ili iwe maikrochip,
Hivyo tuonane kesho.
Akanitazama kwa haya huku aking'ata lipsi,
Akawasha ndinga akasepa.
Wakuu,
Lengo langu ni kufanya tafakuri wakuu,
Vipi,
Nikimchomolea hii tecno p3 yangu hataacha kununua maji kwangu huyu wakuu??