Mrembo mmoja wa Kiafrika amewachekesha wengi baada ya kuelezea masahibu aliyopitia na Mzungu

MOONFISH

Senior Member
Jul 30, 2022
136
266
Mrembo mmoja wa Kiafrika amewachekesha wengi baada ya kuelezea masahibu aliyopitia wakati wa mtoko na mpenzi wake mwenye asili ya Kizungu.

Mrembo huyo anaelezea kwamba ilikuwa ndiyo mara ya kwanza wanakutana na mpenzi huyo Mzungu ambapo waliingia katika mgahawa kushtaki njaa na kilichotokea baada ya chakula ni kumbukumbu za tukio ambalo atakwenda kulala kaburini likiwa kichwani mwake.

Katika video aliyoposti kwenye TikTok, mrembo huyo anasema kuwa, baada ya mlo, mpenzi wake Mzungu aliingia mfukoni na kutoa kalamu kisha kuanza kupiga hesabu.

Anasema kuwa, Mzungu alipiga hesabu ya bili yote na kumtaka binti wa watu washirikiane kulipa ile bili pasu kwa pasu!

“Tafakari kwamba upo katika kukutana kwa mara ya kwanza na mpenzi wako Mzungu na anavuta kalamu kutoka mfukoni na kuanza kupiga hesabu ya bili yake na kuacha nyingine ambayo wewe umekula,” mrembo huyo ameeleza kwa masikitiko makubwa.

Watu mbalimbali wametoa maoni yao ya jinsi walivyojikuta katika visa kama hivyo huku wengine wakisema mrembo huyo alikuwa mpole mno, kwani angezua tafrani hapo hapo.
 
Ni kawaida sana kwa wazungu maana unaweza kaa nae hotel akanywa juice tu akijua hataki kutumia hela bila ulazima wowote wakati katoka kula

Ila sio wa kwetu wanaokula kwa kukomesha kwa baadhi
Ila napenda kumtolea dem kama anajielewa

Sisi tuna tamaduni tofauti na wazungu kabisa
Mzee mmoja mzungu nilikutana nae kwenye training moja akaniambia ana mke wa kikenya ila ana ndugu zaidi ya 40 na wote wanamuomba na kumlilia matatizo
 
Embu niache kwanza ati ndugu 40?🤣🤣🤣 mmmh nao wajistukie bana kuomba omba sio viziri.. Kha!

Shikamoo.
 
Ni kawaida sana kwa wazungu maana unaweza kaa nae hotel akanywa juice tu akijua hataki kutumia hela bila ulazima wowote wakati katoka kula

Ila sio wa kwetu wanaokula kwa kukomesha kwa baadhi
Ila napenda kumtolea dem kama anajielewa

Sisi tuna tamaduni tofauti na wazungu kabisa
Mzee mmoja mzungu nilikutana nae kwenye training moja akaniambia ana mke wa kikenya ila ana ndugu zaidi ya 40 na wote wanamuomba na kumlilia matatizo
Hao wenzetu wanatia aibu,kuna jamaa Youtube ana Chanel yake yuko east Africa tour yaani Kenya ni aibu wanavyoomba omba na kujipendekeza kwa hao tourist
 
Embu niache kwanza ati ndugu 40? mmmh nao wajistukie bana kuomba omba sio viziri.. Kha!

Shikamoo.
Halafu mzee muwazi sana anasema atatuma msg Shangazi ooh Ada na nguo za watoto
Mjomba nae analia hili mara mdogo wake anasema anataka aende college
Wengine shida za mlo
Anasema analisha Taifa Zima la kenya
Wengine jamani hawanaga aibu halafu mzee kama mimi
Ila kanizidi kidogo yeye kaishastaafu na hela zinaliwa na wajukuu Kenya

Nilimuambia unakoelekea utauza nyumba shauri yako hawa ni mchwa
 
Hao wenzetu wanatia aibu,kuna jamaa Youtube ana Chanel yake yuko east Africa tour yaani Kenya ni aibu wanavyoomba omba na kujipendekeza kwa hao tourist
Wao wamezidi kwa kweli ukifika eastleigh Nairobi utakuta wamevaa Ninja wakijifanya wasomali
Kuomba mpaka kero
 
Back
Top Bottom