Mrema yupo habari maelezo

Mrema yupo habari maelezo

DAKTA AU DOKTA MREMA??

hana jipya atasema pumba zilizooza tuu;
 
Hako kazee kamepauka. Maoni yake hayawezi kuwa habari. Mimi niliacha kukasikiliza muda mrefu sana.

Mkuu heshima kidogo najua wewe ni Chadema mzuri kupauka kwa Mrema ni ubinadamu tu, aina uhusiano na siasa, kisiasa kweli Mrema muda wake umekwisha
 
twambieni kama jamii sasa ni mali ya washabiki wa chadema maana naona imekuwa web ya kumponda kila aliyetofauti na mawazo ya chadema why? this is no longer a home of great thinkers my friends it is too much.

Usihofu japo ni ukumbi wao lakini sisi tunawapo dozi humu humu.
 
twambieni kama jamii sasa ni mali ya washabiki wa chadema maana naona imekuwa web ya kumponda kila aliyetofauti na mawazo ya chadema why? this is no longer a home of great thinkers my friends it is too much.

Labda na wewe utuambie JF mgt wanauliza kadi ya chama cha siasa kabla ya kuwa recruited?
Ukiona hivo waTZ wamechoka na serikali kandamizi na vibaraka wake. Tafsiri yako ya mtu anayejua haki yake inavotapeliwa na kunyanyaswa kuwa mwana Chadema. Hata kama ni ivo and so be it....
Mrema hana jipya... ashapata uheshimiwa wa kuzeekea akapumzike Vunjo migombani.
 
katika fukua fukua yangu nimeikuta hii pahala.....

Huyu usanii kaanza zamani sana Lyatonga!

Nimecheka weee, mpaka mbavu zangu zinauma.
Huwezi kuamini kwamba nimeona sinema ya vichekesho ambayo naweza kabisa kuipa nafasi ya kwanza kwa kunichekesha vyema mwaka huu.
Kitu kilichozoeleka ni kwamba sinema nyingi za namna hiyo tunaziona kutoka kwa waigizaji wa nje, lakini huyo wa safari hii ni Mtanzania mwenzetu. Sielewi kwanini anakaa akipigizana kelele na serikali badala ya kuingia kwenye usanii na akala mahela yake kiulaiiini, kwani hawaoni wasanii wa sasa wa Bongo, wimbo mmoja tu (wao wanaita single) ananunua gari na hata nyumba.
Huyu msanii siyo mwingine, bali ni Augustino Lyatonga Mrema, mzee wa Kiraracha kule Moshi aisee.
Basi bwana, yeye jana wakati ameshachukua fomu kutoka kwa wakubwa wa usimamizi wa uchaguzi, akapanda baiskeli akiwa na mgombea mwenza wake, mwanamama kutoka Zanzibar. Wakazungushwa mji mzima wa Dar es Salaam wakiwa na wafuasi wao huku bendera za chama chao cha TLP zikitawala.
Ilikuwa ni burudani ya aina yake kwa kweli. hakuna aliyenuna baada ya kumuona Mrema akiwa juu ya baiskeli ya miguu mitatu akiwapungia wananchi kwa ishara ya kuwaambia kwamba anaingia kwenye kinyang'anyiro hivyo anaomba kura zao aweze kula tu kama wenzake wanavyofanya. Hakuna tofauti kamwe miongoni mwa hawa wenzetu.
Naomba kumpa ushauri wa bure, ikiwa atashindwa (jamba ambalo ninalo uhakika), basi aanze uigizaji katika vituo vya trelevisheni vya hapa kwetu na hata nje, kwani hata kama hajui malugha ya wengine anaweza kabisa kuwa mchekeshaji wa ishara tu kama Roward Atkinson (Mr. Bean). Akifanya hivyo hatakuwa mwenzetu tena, atakuwa ni bilionea mkubwa.
 
twambieni kama jamii sasa ni mali ya washabiki wa chadema maana naona imekuwa web ya kumponda kila aliyetofauti na mawazo ya chadema why? this is no longer a home of great thinkers my friends it is too much.

Tuko wengi na wala haihusiani na kuitwaa JF....kwani nyie mwakatazwa kujiunga? Nadhani mko wachache na mnakuwa wengi kwenye kuiba kura tu
 
katika fukua fukua yangu nimeikuta hii pahala.....

Huyu usanii kaanza zamani sana Lyatonga!

Nimecheka weee, mpaka mbavu zangu zinauma.
Huwezi kuamini kwamba nimeona sinema ya vichekesho ambayo naweza kabisa kuipa nafasi ya kwanza kwa kunichekesha vyema mwaka huu.
Kitu kilichozoeleka ni kwamba sinema nyingi za namna hiyo tunaziona kutoka kwa waigizaji wa nje, lakini huyo wa safari hii ni Mtanzania mwenzetu. Sielewi kwanini anakaa akipigizana kelele na serikali badala ya kuingia kwenye usanii na akala mahela yake kiulaiiini, kwani hawaoni wasanii wa sasa wa Bongo, wimbo mmoja tu (wao wanaita single) ananunua gari na hata nyumba.
Huyu msanii siyo mwingine, bali ni Augustino Lyatonga Mrema, mzee wa Kiraracha kule Moshi aisee.
Basi bwana, yeye jana wakati ameshachukua fomu kutoka kwa wakubwa wa usimamizi wa uchaguzi, akapanda baiskeli akiwa na mgombea mwenza wake, mwanamama kutoka Zanzibar. Wakazungushwa mji mzima wa Dar es Salaam wakiwa na wafuasi wao huku bendera za chama chao cha TLP zikitawala.
Ilikuwa ni burudani ya aina yake kwa kweli. hakuna aliyenuna baada ya kumuona Mrema akiwa juu ya baiskeli ya miguu mitatu akiwapungia wananchi kwa ishara ya kuwaambia kwamba anaingia kwenye kinyang'anyiro hivyo anaomba kura zao aweze kula tu kama wenzake wanavyofanya. Hakuna tofauti kamwe miongoni mwa hawa wenzetu.
Naomba kumpa ushauri wa bure, ikiwa atashindwa (jamba ambalo ninalo uhakika), basi aanze uigizaji katika vituo vya trelevisheni vya hapa kwetu na hata nje, kwani hata kama hajui malugha ya wengine anaweza kabisa kuwa mchekeshaji wa ishara tu kama Roward Atkinson (Mr. Bean). Akifanya hivyo hatakuwa mwenzetu tena, atakuwa ni bilionea mkubwa.

Kweli ilikuwa kichekesho! Kwa kuongezea tu alikuwa amevaa yale mavazi ya digrii yake aliyopata, kwani aliambiwa ni lazima mgombea urais awe mwenye digrii. Halafu nilisika kwamba alikuwa analivaa vazi hilo wakati wote hata akiwa nyumbani ili waliokuwa wanamtembelea wajuwe kama yeye ni msomi wa digrii level!

Hata hivyo naamini iwapo atazungumza kuponda wimbi la mageuzi la CDM, basi hiyo itakuwa ni project ya CCM, na hasa hasa itakuwa ni ya kati ya wale wahindi watatu ambao kung'oka kwa CCM ndiyo mwisho wao. Mnawafahamu wadosi hao.
 
nashangaa wanaomsikiliza, nashangaa wanaopoteza muda wao kuandika habari zake, nashangaa waliompa udokta, nashangaa, nashangaa waliomchagua ubunge, nashangaa waliomchagua uenyekiti wa kamati na zaidi nawashangaa wote wasiomshangaa huyu mwehu!, yaani katika watu wa hooooovyo tanzania huyu ni namba 1 akifuatiwa na mafisadi wote! Kama si usaliti wa huyu chizi leo ccm ingekua chama cha upinzani!
 
jamani kaongea nini leo mrema? maana jana nilitoa taarifa juu yake kuwepo leo pale habari maelezo, mwenye taarifa atujuze nimeshindwa kwenda huko leo nilikuwa na majukumu, baraza la wanawake wa chadema walikuwa wanaenda kuwapa pole wanawake wenzao kule gongo la mboto kwenye mabomo....( kanda maalum ya dar es salaam)
 
small mind discus people, middle mind discus event, great mind discus ideas. je a thinker gani anamwita mrema mwehu au amepauka. hata hajamsikiliza. it make me angry discus ideas.probably mwehu ni wewe..
 
Mrema na wafuasi wote wamejichokea sana lakini wamo tu, eti yupo maelezo.Hana jipya.
 
ANGALIZO LA DK AUGUSTINO MREMA KWA CHADEMA NA UHAMASISHAJI WA MAANDAMANO - Global Publishers

Mbunge wa Jimbo la Vunjo, mwenyekiti wa Chama cha TLP na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali za Mitaa Dk. Augustino Lyatonga Mrema akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa angalizo kwa chama cha CHADEMA kutokana na mikutano yake inayohamasisha maandamano akisema kuhamasisha maandamano kunaweza kuleta uvunjifu wa amani kama ilivyotokea kwa nchi za Madagascar, Misri, Tunisia na sasa Libya.

Dk. Mrema ameongeza kwamba kwa kawaida mkiiangusha serikali bila kufuata utaratibu wa kikatiba upo uwezekano mkubwa wa kuleta vurugu katika nchi kama ilivyotokea kwa nchi hizo za kiafrika ambazo hata walipoondolewa watawala ambao walikuwa hawatakiwa bado hakuna utulivu na mahali pengine jeshi limepata mianya ya kuchukua madaraka kwa lengo la kuhakikisha usalama wa nchi zao kama ilivyotokea kwa Misri ambayo kwa sasa inaongozwa na Jeshi.
 
Nani kabaki bila "DR" nji hii? labda ni mimi tu!
Kila mtu ni Mheshimiwa au Dr,....kazi ipo!
 
Aliyoongea Mrema leo kwa mujibu GP.
HTML:
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, mwenyekiti wa Chama cha TLP na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali za Mitaa Dk. Augustino Lyatonga Mrema akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa angalizo kwa chama cha CHADEMA kutokana na mikutano yake inayohamasisha maandamano akisema kuhamasisha maandamano kunaweza kuleta uvunjifu wa amani kama ilivyotokea kwa nchi za Madagascar, Misri, Tunisia na sasa Libya.
 
Dk. Mrema ameongeza kwamba kwa kawaida mkiiangusha serikali bila kufuata utaratibu wa kikatiba upo uwezekano mkubwa wa kuleta vurugu katika nchi kama ilivyotokea kwa nchi hizo za kiafrika ambazo hata walipoondolewa watawala ambao walikuwa hawatakiwa bado hakuna utulivu na mahali pengine jeshi limepata mianya ya kuchukua madaraka kwa lengo la kuhakikisha usalama wa nchi zao kama ilivyotokea kwa Misri ambayo kwa sasa inaongozwa na Jeshi, katika picha kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Mh. Hamad Tao.

My take: CCM kweli imekabwa koo, yaani mpaka wanarudia matapishi yao waliyosema si chochote kuwasemea? lol!. Hii nina uhakika wa 100% kuwa ni kazi ya CCM, Kauli aliyotoa Sophia Simba leo kuhusu maandamano ya CDM ni dhahiri kuwa huu ni mkakati maalum wa kudanganya umma ambao kwa sasa haundanganyiiki kuhusu maandamano ya CDM. Watu wamechoka sana, na kuhudhuria maandamano ni haki yao hataka ni 7days a week kwa miezi sitini mpaka uchaguzi wa 2015.

Naona siku hizi neno Dokta (Dr) limekosa maana kabisa na halina heshima tena, Kina Prof Nkunya M na Kamati yake wanatakiwa kuja na muongozo katika hili kwani ni sawa na kumwita raia Afande wakati hata mafunzo ya kijeshi hayajui. Vinginevyo tunaua elimu kabisa maana vijana wataona hakuna haja ya kujiendeleza katika level hiyo kama anaweza kupata wa heshima na kuitwa kwa jina hilo.
 
aende kwanza loliondo akanywe dawa ya kisukar. Akpona 2tamckilza. Mm huwa nahic akil zmechakachuliwa na kisukar chake! Hana mvuto tn!
 
Hakuna jambo lisilokuwa na mwisho.......kipindi chake kilipita, ashukuru watu wa kiraracha wamemuhurumia kwa ajili ya afya yake kuwa mbaya wakamrudisha mjengoni kwani hali yake ilikuwa taabani, sasa atulie aangalie afya yake na kufuata masharti, hakuna mtanzania anayechukia mafisadi anayemsikiliza labda hawa mafisadi wa ccm wanaomdanganya.
 
His days are gone! Everybody knows that he supports JK
 
Joto linaendelea kupanda.sijui sasa hivi thermometer inasoma ngapi kwa hawa watawala.kivuli cha yanayotokea huko kaskazin kinawawewesesha watawala dhalimu.wanatumia chochote kupunguza kasi.ha ha ha!
 
Mwalimu wangu wa philosophy aliniambia ukiona mtu anaacha kujadili hoja anaanza kumjadili mtoa hoja basi hana hoja..kwa hii hali badala ya kujibu hoja ya Mrema naona wapambanaji wanashambulia afya yake, hii ni kuonesha umbumbu na ububusa
 
Back
Top Bottom