Mrema: Nitagombea tena Ubunge

Mrema: Nitagombea tena Ubunge

Kama anasomaga JF naona nimpe ka ushauri tu. Apokee hiyo hela yake ya pension aondoke nayo taratibu. Akifika kule Kahe kwake, aongezee ng'ombe zake na mbuzi na kondoo wake. Aoteshe miti mingi tu ya matunda.
Lakini, kama anayo imani kuwa Wapo watu bado wanampenda, sisi tulio huku tunamwambia asome alama za nyakati.
APUMZIKE KWA AMANIIII
 
Sitampa kura yangu, ameshindwa kusimamia maji tuliyoyafanyia kazi sisi wanataka kuja kutufungia mita.
 
Mrema hakusanyi kodi.
Hujui usemalo, kila wilaya, kila kijiji kuna utaratibu wa umeme na maji kutoka fungu la serikali, pia ana mfuko wa jimbo, nje ta hayo tulishamwambia tuko tayari kuchanga umeme na maji upelekwe panapostahili huyu babu ahadi kabao hazina utekelezaji, nikuambie nina elumu nzuri ambayo sio ya kuunga kama ya Mrema ya online, nitapambana nae.
 
Tujikumbushe historia

1995-2000; Mbatia (NCCR)
2000-2005; Makundi (TLP)
2005-2010: Kimaro (CCM)
2010-2015 :Mrema (TLP)
2015-2010 : ????

Wana Vunjo hawakupi vipindi viwili. Ni kimoja tu!!!
Wana vunjo natarajia kugombea ubunge 2015 ,naombeni kura zenu mbee
 
kama anataka kupoteza alichopata kwa wakati huu ajaribu kugombea tena aone maana safari hii Chadema itamsimamisha mgombea wa Nguvu. akibishana na mawazo yangu atakuwa sikio la kufa

pengine CCM au TLP watumie ruzuko yote kwake bila hivyo mrema atamalizia ehemu ya pension yake ktk kampeni halafu itakuwa imekwenda.
 
CCM naskia wameandaa mtu maalum kurudisha maendeleo ya katika Jimbo hilo.

Watu wa vunjo hawahitaji maendeleo yaletwe na ccm! Wana maendeleo kabla ya kuwepo kwa ccm! mimi simpendi kabisa huyu babu..
 
Sipingani naye sana lakini napenda kujua mchango wake kwa watanzania kwa kipindi chote akiwa mbunge na pia mchango wake wa Vunjo akiwa kama mwakilishi wao. Kama hamna au kama ni mdogo ni heri akapumzika kupisha wengine
 
Alivyokuwa anaongea kwa kutetemeka hadi alikuwa anatia huruma.Hana hati miliki kwenye jimbo la Vunjo.Ni haki yake kikatiba kugombea but 2015 there will be no room for him again.Apumzike tu hatuna mfumo wa umangi tena uchaggani.

Ana uhakika CCM itamsaidia kushinda kama ilivyokuwa uchaguzi uliopita. Anazeeka vibaya.
 
inji hii itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno...teh teh...
 
Hujui usemalo, kila wilaya, kila kijiji kuna utaratibu wa umeme na maji kutoka fungu la serikali, pia ana mfuko wa jimbo, nje ta hayo tulishamwambia tuko tayari kuchanga umeme na maji upelekwe panapostahili huyu babu ahadi kabao hazina utekelezaji, nikuambie nina elumu nzuri ambayo sio ya kuunga kama ya Mrema ya online, nitapambana nae.


CCM/CDM walisimamisha vijana tena wenye elimu nzuri kuliko ya Mrema lakini haikumzuia kuwagaragaza.
 
Daaaah hawa ndo wanataka kufia madarakan mmhhh kagombeee mzee jimbo lako naona uko mwenyewe
 
Ila katika kampeni za 2010 aliaga kuwa anaomba kura za kustaafu siasa kwa heshima, sasa sijui kipindi hiki atakuwa na hoja gani ya kutaka kuendelea wakati ameshikilia kuuza ardhi za wakulima wa Kilototoni, Lotima, Riata, Kahe etc.

kwa kipindi chote yeye ni kuomba kulipwa kiinua mgongo chake cha naibu waziri mkuu, TLP imekuwa na makao makuu Vunjo......asifikiri watu wa vunjo ni wehu.........
 
Hao wote walipeleka vijana akawagaragaza, 2015 bado ana nafasi ya kushinda. Mrema anakubalika sana Vunjo hasa kwa akina mama.

Akina mama wanampenda sana kwa sabubu huyu mzee huwa akienda sokoni huwa anaonja maziwa ya mgando na hao akina mama
 
Back
Top Bottom