Mrema: Nachezewa rafu Jimboni na Mbatia

Mrema: Nachezewa rafu Jimboni na Mbatia

Change ni wewe,simama kaoneshe nia ya kugombea,
ama mtengenezeni kijana aweze kugombea,
WaTanzania tumekuwa watu wa nani atamfunga paka kengele..
Hizi ndio Siasa za Tz , yaani Vikongwe wamo ni shiiiida ! akina Ndesa pesa wamo, akina Mkono wamo, akina Cheyo wamo ,akina Mrema wamo,Kasoro Kingunge tu ndio kajibanza pembeni ,sasa Wakongwe wapo busy majimboni wakihakikisha wanakuwa wabunge hadi mwaka 5000.
 
kwan zzk anahusika kwene hii mada? we si mr yes man!!! victor
 
Mrema wa mwaka 1995 na wa mwaka 2014 ni tofauti sana. Kama mbingu na ardhi.
 
Rafu unajichezea mwenyewe Mzee wa Kiraracha.
 
Kwani mrema hamchezei mbatia rafu kweny ubunge wake wa kuteuliwa? Alipomwambia raisi kuwa amfute mbatia ubunge wa kuteuliwa sio rafu! mwosha huoshwa atulie tu!
 
mrema ameshachoka ndo kila mahali anaenda juzi kwenye mazunguzo ya raisi na ukawa nilimwona sijui alienda kule kama na nani na kufanyaje mwakani mbatia lazma tumpe kura mrema ni kibaraka wa ccm njaa zinamsumbua ajiendaa kwenda kulima mahindi

Wenye njaa sio Mrema peke yake, na kule Bariadi kuna mzee mmoja aitwa John Cheyo anapaswa kupigwa chini na kusahaulika kwenye siasa za kileo zinazoenda na wakati, watu wa Bariadi walimheshimu sana Cheyo lakini hivi sasa ana rank kwenye zero
 
Mbunge wa jimbo la vunjo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya TLP bwa. Augusine Lyatonga Mrema amedai kuchezewa rafu na bwa. James Mbatia mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa.
Alisema bwa. Mbatia amekuwa akifanya ziara jimboni kwake na kuwaambia wananchi kuwa Mrema hawezi kugombea tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa sababu ya uzee na afya aliyonayo kitendo ambacho wananchi hao kumwamini Mbatia na kupelekea kumdhoofisha mzee huyo kisiasa.
Source: Majira leo.
Ha ha haha ! Sasa si akanushe kuwa sio Mzee bali ni mtoto! Kwani si tunaona anavyobabuka rangi kutoka weusi wa maji ya kunde kwenda white ikianzia usoni
 
Mbunge wa jimbo la vunjo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya TLP bwa. Augusine Lyatonga Mrema amedai kuchezewa rafu na bwa. James Mbatia mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa.
Alisema bwa. Mbatia amekuwa akifanya ziara jimboni kwake na kuwaambia wananchi kuwa Mrema hawezi kugombea tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa sababu ya uzee na afya aliyonayo kitendo ambacho wananchi hao kumwamini Mbatia na kupelekea kumdhoofisha mzee huyo kisiasa.
Source: Majira leo.
Kwani hakuna refa katika hiyo mechi? Na bado, kama chenga ni rafu basi refa hatakusaidia.
 
Lyatonga Mrema is already a 'dead figure' kwa wanaVunjo....! Kwa wanaofuatilia kwa karibu, watakubaliana na mimi kuhusu hali mbaya ya Mrema ktk maeneo mengi ya Vunjo! Amebakia tu na Kata chache za kwake Marangu, na maeneo ya Mamba, hata Mwika hawataki kumsikia hata jina lake!...Kwa maeneo mengine ndio hasira ipo juu sana,...Kuna Mikutano ya wazee wa Vunjo Magh (Maeneo ya Kisomachi Madukani) ktk Mikutano ya Jumapili ktk Matangazo ya maendeleo, baada ya Ibada, waliweka bayana wakaapa waziwazi kuwa Mrema ni msaliti mkubwa, aliwatusi na kuwadhalilisha sana ktk mikutano yake baada ya Mwaka 2012, 2013 aliyokuwa anaenda maeneo hayo kujieleza kwao hasa maeneo ya Kirua Vunjo na, alipoulizwa '..mbona alipochaguliwa alitoa ahadi nyingi pamoja na kupandisha maslahi ya wakulima wa Kahawa, uimarishaji wa miundombinu hasa barabara na afya, lakini amepotelea mbali na kubali kuisaidia na kuitetea CCM bungeni (ambayo wazee hao walishaikataa zamani), badala ya kutetea wananchi wa Vunjo waliomtuma...?, Na kwa hasira, Mrema aling'aka akasema, anajiamini, atachaguliwa na kama Wanaume hao hawatamchagua, wake zao (wanawake) watamchagua maana wanajua kuwa yeye bado ni kidume..., na kama wanabisha wamuulize hata Mke wake anajua bado ana nguvu (kitandani)..' Maneno hayo yaliwapa hasira sana wananchi wakataka kumwacha peke yake ktk mkutano hadi viongozi wa vijiji walipowaasa wasubirie kidogo afafanue...hakufafanua akaishia zake!...Wazee wakaapa kuwa kura za mwisho kwa Mrema ni alizopata 2010!
Analijua hilo na hakuna analotegemea zaidi ya kujipa matumaini kwa kumpinga Mbatia ili aonekane naye anajitambua...! Kwa tathmini tulizo nazo, Jimbo la Vunjo yote ukiondoa Watu wa Marangu (25%), asilimia iliyobaki Vunjo ni zaidi ya 75% ni imara sana, wamejaa hasira na wanamsema Mrema kuwa Mbaguzi mkubwa kujali Marangu zaidi dhidi ya maeneo mengine, na wanampinga kwa 100% Atashinda kwa 25%??!

Na tathmini ya Vyama kuungwa Mkono sasa na baadaye ktk jimbo la Vunjo, mgawanyiko unakaribia sana kuwa kama ifuatavyo: CCM(masalia) - 20% , TLP - 10%, CDM - 30% na NCCR - 35% na Wasio na maamuzi kamili 5% (Note: Mbatia anaweza kupita kwa kishindo kwa option ya UKAWA au pia kwa NCCR pekee akipambana vyema, na pia CDM inaweza kupita kwa nguvu ya UKAWA, ila CDM pekee bado nguvu inahitajika kiasi ili kuongeza tarakimu...! Ila muhimu ni kuwa...CCM bye...TLP bye! forever..)
 
Akili ya huyu mzee imeshafika pale wachumi wanaposema curve iko kwenye diminishing return. Hana mawazo tena. Wachaga husema amekuwa kyishoiya.
Ameshindwa kusaidia umeme mashulini', majibaadhi ya kata ni issue. Amebaki kucheza ngoma za magamba tu.
 
Back
Top Bottom