Mrema: Nachezewa rafu Jimboni na Mbatia

Mrema: Nachezewa rafu Jimboni na Mbatia

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Mbunge wa jimbo la vunjo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya TLP bwa. Augusine Lyatonga Mrema amedai kuchezewa rafu na bwa. James Mbatia mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa.
Alisema bwa. Mbatia amekuwa akifanya ziara jimboni kwake na kuwaambia wananchi kuwa Mrema hawezi kugombea tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa sababu ya uzee na afya aliyonayo kitendo ambacho wananchi hao kumwamini Mbatia na kupelekea kumdhoofisha mzee huyo kisiasa.
==============================

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, Bw. Augustino Mrema, amedai kuchezewa rafu jimboni mwake na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia.

Alisema Bw. Mbatia amekuwa akifanya ziara jimboni kwake na kudai, ametumwa na Rais Jakaya Kikwete kwenda kugombea ubunge wa jimbo hilo kwa madai Bw. Mrema hawezi kugombea tena katika Uchaguzi Mkuu 2015 kwa sababu ya uzee alionao.

Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu akiwa Mjini Dodoma, Bw. Mrema alisema Bw. Mbatiaamekuwa akimtangaza vibaya kwa wapigakura wake kuwa yeye ni kibaraka wa CCM na kuwashawishi wananchi wasimchague katika uchaguzi mkuu ujao.

"Juzi tulipokutana na Rais Jakaya Kikwete kwenye kikao ambacho kilishirikisha viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge vinavyounda Kituo cha demokrasia (TCD) katika Ikulu Ndogo, Mjini Dodoma, Rais Kikwete aliniuliza kuhusiana na ubunge wa Vunjo.
"Mimi nilimwambia amemtuma Bw. Mbatia aje kuning'oa Vunjo na Rais Kikwete mbele ya wajumbe wengine, alimuuliza kama alimpa ubunge wa kuteuliwa au kuja kunivua ubunge...Mbatia alikaa kimya hivyo ni muongo kusema ametumwa," alisema.

Bw. Mrema aliongeza kuwa, haoni tatizo kwa Bw. Mbatia kutangaza nia ya kuwania ubunge wa Vunjo bali kinachomkera ni kitendo chake cha kutumia jina lake (Mrema) na la rais kutaka ubunge pamoja na kumchafua kwa wapigakura wake.
"Kwanini aseme nimetangaza jimbo langu lipo wazi na sitagombea tena kwa sababu ni mzee na kudai ametumwa na Rais Kikwete kugombea wakati si kweli," alihoji Bw. Mrema.

"Kampeni hazijaanza, yeye amekwenda Vunjo kunipaka matope kwa wapigakura, kwanini anichezee rafu na kauli anazotoa jimboni zimekuwa zikiaminiwa na wananchi ambao wanamuunga mkono wakijua ni kweli nimetangaza kutogombea tena," alisema.
Alisema hajawahi kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimbo hilo hivyo yeye ni mbunge na ataendelea kuwa mbunge akiwataka wananchi kutomsikiliza Bw. Mbatia kwani yuko fiti na hajazeeka kiasi cha kushindwa kuwatumikia wananchi.

"Naomba Mbatia aache kunichezea rafu, asubiri muda ufike kwani anavyofanya ni kuwapotosha na kuwachanganya wananchi, mimi ni mbunge halali wa Vunjo kwa sasa na jimbo hilo haliko wazi.

Alisema amekuwa mbunge kwa miaka 10 ndani ya CCM na aliwahi kuwa mbunge wa Temeke na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hivyo anaaminiwa na wananchi pia kuna miradi mingi hajakamilisha hivyo anatakiwa kuikamilisha.
"Wapo baadhi ya watu waliotangaza nia ya kuwania ubunge wa Vunjo lakini sijawalalamikia, namlalamikia Mbatia kwa sababu ananichafua ndio maana nimeamua kulizungumzia hili," alisema.

Gazeti hili lilipomtafuta Bw. Mbatia katika simu yake ya mkononi ili aweze kuzungumzia madai hayo haikupatikana.

Chanzo: majira
 
Mbunge wa jimbo la vunjo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya TLP bwa. Augusine Lyatonga Mrema amedai kuchezewa rafu na bwa. James Mbatia mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa.
Alisema bwa. Mbatia amekuwa akifanya ziara jimboni kwake na kuwaambia wananchi kuwa Mrema hawezi kugombea tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa sababu ya uzee na afya aliyonayo kitendo ambacho wananchi hao kumwamini Mbatia na kupelekea kumdhoofisha mzee huyo kisiasa.
Source: Majira leo.
Kwani Mbatia anasema uongo? Mrema kwisha habari yake!
 
mrema ameshachoka ndo kila mahali anaenda juzi kwenye mazunguzo ya raisi na ukawa nilimwona sijui alienda kule kama na nani na kufanyaje mwakani mbatia lazma tumpe kura mrema ni kibaraka wa ccm njaa zinamsumbua ajiendaa kwenda kulima mahindi
 
Mbatia alichemka kugombea dar pale,,hili jimbo lipo wazi kwake.
 
Hahaha huyu mzee bana
hata msaliti zzk akizeka atakuwa na tabia km za huyu bwana
 
Mbunge wa jimbo la vunjo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya TLP bwa. Augusine Lyatonga Mrema amedai kuchezewa rafu na bwa. James Mbatia mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa.
Alisema bwa. Mbatia amekuwa akifanya ziara jimboni kwake na kuwaambia wananchi kuwa Mrema hawezi kugombea tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa sababu ya uzee na afya aliyonayo kitendo ambacho wananchi hao kumwamini Mbatia na kupelekea kumdhoofisha mzee huyo kisiasa.
Source: Majira leo.
Tararilaaaa! Mwanzo wa UKAWA kumalizana, niliyasema haya na bado..
 
Hivi hakuna mwananchi anayejipanga kumg'oa john cheyo? huyu nae hafai!
 
Mrema alikimbia biashara ya jumla(urais) kaenda ya rejareja(ubunge) na sasa rejareja imeingiliwa sijui atakimbilia wapi
 
Mbatia mwakani atachukua jimbo Maana Mrema sasa ni kikongwe kama alivyo Mzee Cheyo na Kingunge ,Mrema kapumzike CCM watakupatia mafao yako ya Cheo cha Naibu Waziri Mkuu.
 
Hivi hakuna mwananchi anayejipanga kumg'oa john cheyo? huyu nae hafai!

Atajing'oa mwenyewe kwani kufika mwakani atakuwa na Miaka 800 meno yameng'oka kuongea itakuwa Shiiida ! Wenye kulipenda jimbo lake Mnakaribishwa sana kwani sasa Hana mapesa Kama zamani .
 
Hizi ndio Siasa za Tz , yaani Vikongwe wamo ni shiiiida ! akina Ndesa pesa wamo, akina Mkono wamo, akina Cheyo wamo ,akina Mrema wamo,Kasoro Kingunge tu ndio kajibanza pembeni ,sasa Wakongwe wapo busy majimboni wakihakikisha wanakuwa wabunge hadi mwaka 5000.
 
Back
Top Bottom