Mrema: Kufukua makaburi ya Kikwete na Mkapa ni kuisambaratisha nchi

Huyu ni mmojawapo ya wale wazee wetu wagonjwa ambapo kimsingi walitakiwa wakae kijijini wabembeleze wajukuu. Kuendelea kumtwisha majukumu ni kumuumiza bure
 
Ni Wapi Acacia wamesema wako Tayari kulipa? Ivi tumetazama Networth ya Hii kampani mpaka tunataka Trilioni 100, Mzungu wa Kumuamini ni aliyekufa tu si Mzungu Hai
 
Mnamuonea bure tu Mh Mrema. Mlitegemea aongee tofauti na alivyofanya? Anaanzia wapi?
 
Jamani Mrema, kubali kuwa umechoka sasa. Ukiisoma vyema Katiba yetu zingatia kinga kwa rais dhidi ya makosa aliyoyatenda akiwa madarakani (urais)

JK alianza kusaini mikataba mibovu ya madini akiwa waziri wa maji, nishati na madini mwaka 1998 kabla ya kuwa rais, je, na kwa makosa hayo awekewe kinga? Mrema, fafanua hapo!?
 
kama waziri wa zamani anashughulikiwa kwa nini rais wa zamani asishughulikiwe? Huyu Mrema anatetea tumbo lake. Aliwageuka wanachama wake alipomuona Magu pale Moshi akajipendekeza mpaka akafika hapo alipofika mnategemea aseme nini?? Wanategua mabomu bila vifaa vya kujikinga? kwani aliyetamka 'WOTE' ni nani? Mtuonee huruma sasa mmetufilisi vya kutosha jamani
 
Back
Top Bottom