Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,553
- 41,061
Ni ukweli usiopingika, tangu ofisi ya CAG ianzishwe, hakuna wakati ulipokosekana wizi ndanibya Serikali na taasisi zake. Kinachobadilika ni wizi kuwa mkubwa, mkubwa sana au mkubwa kupindukia.
Awamu pekee ambayo ama hakukuwa na wizi au kulikuwa na wizi mdogo sana, ni awamu ya Mwalimu Nyerere, awamu ya kwanza. Na hilo lilidhihirishwa hata na maisha yake mwalimu Nyerere na familia yake. Wakati wa Mwalimu Nyerere, Urais ulikuwa wa kwake binafsi, lakini siku hizi, Urais unakuwa wa familia nzima, hata marafiki wa familia ya Rais. Ndiyo maana tunashuhudia wanafamilia kuwa sehemu ya misafara ya Rais nje ya nchi.
Awamu ya Mwinyi iligubikwa na wizi wa ajabu kupindukia, ambapo inasemwa kuwa zaidi 60% ya pesa zote za misaada, hazikuwahi hata kufika nchini, watu waliziweka kwenye akaunti zao binafsi huko mataifa ya nje. Wakati wa awamu ya Mkapa, kulikuwa na unafuu, lakini haukukoma. Baada ya hapo, wizi ndani ya Serikali umekuwa kwenye mwendo wa kupaa.
Kwa kuwa wizi unaanzia juu kabisa mpaka chini, hakuna wa kumwajibisha mwingine. Kwa sasa, wizi mpaka umehalaljshwa, ndiyo maana hata wanafamilia wa viongozi wakuu wanakuu matajiri wakubwa hata bila ya kuwa na vyanzo vilivyo wazi vya mapato ya kuwawezesha kuwa matajiri. Wameona hiyo haitoshi, sasa wamefikia mpaka hatua ya kuidhinisha malipo kwa wake wa marais. Na tunavyoenda, siku moja itawekwa rasmi kuwa kuwepo kwa malipo kwa wanafamilia wote wa marais na viongozi wengine wakuu, japo hata sasa wakati sheria hiyo haipo, wanafamilia wamekuwa wakifaidi pesa za wananchi maskini, ni kama vile kuolewa na Rais au kuwa mtoto wa Rais, tayari amefanya kazi kubwa sana kwa Taifa, kiasi cha kustahili kulipwa.
Mjadala wa wizi wa pesa za umma uliofanywa na viongozi na watendaji wakuu wa Serikali na taasisi zake, kupitia report ya CAG, kama ilivyotarajiwa, umeisha na hakuna chochote cha maana kilichoamliwa na bunge bandia (ni bunge bandia kwa sababu ndani humo kuna wabunge wengi bandia kwa kadiri ya hukumu ya mahakama kuu, na kuna wabunge wengune bandia 19 waliomo humo ndani kinyume cha katiba).
Huu wizi wote umeasisiwa, unaendelezwa, na kulindwa na CCM. Hao wevi ni viongozi wakuu kupitia CCM, na wengine ni watendaji wakuu kwenye Serikali na taasisi za serikali, ambao kiuhalisia, kama wewe siyo kada wa CCM huwezi kuteuliwa kuziongoza. Kwa hiyo wizi huu wote wa kila mwaka, kila wizara, kila halmashauri na kila taasisi unafanywa na makada wa CCM, unaendelezwa na CCM, na unalindwa na utawala wa CCM.
Maadam CCM ipo madarakani, wananchi inabidi waukubali na kuuzoeazoea, maana hakuna tegemeo wala mwanga kuwa kuna siku utakoma, au kuna siku wevi watachukuliwa hatua makini, zaidi ya hizi za kiinimacho, kama kupiga kelele sana bungeni, na mishowe kupongezana na kufunga mjadala.