Mrema akagombee Arusha!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,539
40,172
Kama habari za kutoswa kwa wana CCM kule Arusha zina ukweli, nadhani umefika wakati kwa Mrema kurudi Bungeni kwa kwenda kugombea kiti cha wajanja hao na liwe pigo la kwanza kwa CCM. Kile kiti kingine kinaweza kugombewa na mwanaharakati mwingine kama Tundu Lissu hivi. Huo ndiyo uzuri wa nchi yetu... Na bila ya shaka ataweka rekodi ya kuwa kiongozi aliyewahi kuwa Mbunge wa majimbo matatu tofauti katika mikoa mitatu tofauti!!!
 
rekodi haina ubaya - watu wanajaribu kuziweka kila siku.. ila kubwa ni hilo la Uwakilishi. Ninaamini viti vyote viwili vikiwekwa wagombewa wazuri Wapinzani watashinda, na watu kama Mrema tunammiss Bungeni...
 
Kama habari za kutoswa kwa wana CCM kule Arusha zina ukweli, nadhani umefika wakati kwa Mrema kurudi Bungeni kwa kwenda kugombea kiti cha wajanja hao na liwe pigo la kwanza kwa CCM. Kile kiti kingine kinaweza kugombewa na mwanaharakati mwingine kama Tundu Lissu hivi. Huo ndiyo uzuri wa nchi yetu... Na bila ya shaka ataweka rekodi ya kuwa kiongozi aliyewahi kuwa Mbunge wa majimbo matatu tofauti katika mikoa mitatu tofauti!!!

Mtafute umwambie hivyo. Mrema, Slaa na Zitto watarudisha uhai katika bunge lilikosa imani kwa Watanzania walio wengi. Kuna uwezekano CCM ikapoteza viti vyote viwili...Oh! well kama hawakuiba kura.
 
..kweli Mrema akisimama ubunge hata $$$ nitampatia kusaidia kampeni yake,jamani tunahitaji wapinzani kule bungeni la sivyo itakuwa kelele tuu na mwendo wa ufisadi..mwanakijiji najua unaweza kumpata Mrema mkaongea naye na umshauri afanye hivyo na umwambie Koba atakuchangia dola mia tatu(serious) za kampeni kama akigombea
 
Kabla ya MKJJ kumtafuta Mrema, hana budi kutafuta hotuba za Mrema kabla ya kwenda NCCR- Mageuzi, Then hapo ndio mtajua kuwa Mrema ni FISADI vilevile...
 
Alishakuwa ktk CCM.. then ni fisadi tu

Si dhani kama uko serious KIunango?

Ninacho jua alipo ona hawezi kuvumilia huo ufisadi ndani ya CCM aliamua kule Dodoma ndani ya Bunge Chimwaga enzi zile namnukuu..
''NITASEMA KWELI MUNGU NISAIDIE''.. Mrema aliamua kusema kweli na wakamtema.. ama nasahau mkuu??

Ndo maana pamoja na kuishiwa kwakwe lakini huo ujasiri wake alio uonyesha siku ile alipo simama kusema kweli na kujitenga na Mafisadi wa CCM, unamtumainisha mtu yeyote kwamba ni mwakilishi mzuri ambaye yuko tayali kuachia ulaji wake kwa kutetea maslahi ya wanyonge.. in short is another Zitto of those days!!
 
Rwabugiri
Ni Mrema huyohuyo aliwataka Wazenj kutokimbilia kwenye vyama vya Upinzani, akitishia kutokea kwa vita, yeye akasema iwapo itatokea vita TZ yeye na Mohd Raza watapanda ndege na kwenda nje ya nchi. Hotuba hii aliitoa alipokuwa akifungua Polisi Post ya Majestic Cinema huko Zenj...

Iwapo aliweza kumkumbatia Mohd Raza, basi yeye ni FISADI tu.. . Huko Dodoma alikuwa ni Mfa Maji...
 
kumbe kila aliyepitia CCM ni fisadi? hata mimi niliyempa JK kura ni fisadi? Mrema siyo fisadi bwana mbona alikuwa kinara wa kuwaumbua vigogo wa ccm enzi zake? bado akaondoka na kuacha ulaji ndani ya chama tawala?
 
rekodi haina ubaya - watu wanajaribu kuziweka kila siku.. ila kubwa ni hilo la Uwakilishi. Ninaamini viti vyote viwili vikiwekwa wagombewa wazuri Wapinzani watashinda, na watu kama Mrema tunammiss Bungeni...

...mzee nadhani mara byingine pitia hoja mara mbilimbili kabla ya kuzijibu kwani labda wengine wanataka kujaza thread kwa maswali yasiyo na umakini. lakini umemjibu vyema ila not all challenges must be accepted. just advice

Naamini Mrema akienda atapata na inabidi vyama vingi waanze kuandaa safu za ushindi. Nampongeza muungwana kwa kuwatosa hao wadau wake ili hatimaye wapinzani waingie bungeni...
 
Kwani Kuna Viti Viwili Vya Ubunge Vimetenguliwa Na Mahakama ..if So ...ni Arusha Na Wapi!???

Ikitokea Nafasi Yoyote Wazi Wapinzani Watumie Kujiimarisha....
 
Phillemon, huhitaji kutenguliwa na mahakama kuwa na viti wazi.. Kwa vile Katiba yetu inasema huwezi kuwa Mbunge hadi uwe na chama cha kisiasa, sasa chama chako kikikuvua uanachama unapoteza Ubunge papo hapo. Na kwa vile haturuhusu wagombea huru wale waliovuliwa uanachama (ingawa hawajavuliwa uwakilishi) hawawezi kuendelea kuwa Wabunge. It is one of those stupid laws ambazo mwalimu aliita ni za Kipumbavu!
 
kisiasa jimbo pekeee ambalo linaweza kuchukuliwa na yeyote ni arusha mjini...lakini kule kwa lekule laizer na monduli kama si masai kaka hawakuelewi....kule monduli kwenyewe wazee wanampigaga lowassa vijembe chini chini kwa kuwa familia yao ilihamia pale ..na lowassa ana asili ya arumeru...kuna wakati wazee walimuita joseph sokoine aje wampe ubunge ...lowassa akamzuia kistaarabu kwa kuongea na rafiki yake kikwete akiwa pale foregn ampeleke nafasi ya washington haraka sana ...wazee wakapoa...ila ujue ile nafasi ya ubunge monduli lowassa anamshikia tu ..joseph nafikiri mwaka 2015 anaweza akamwachia....hata hivyo joseee anamuheshimu sana lowassa kama kaka na kama msaidizi[Personal assistant] wa zamani wa baba yake..

kuhusu pale arumeru kwa mla na mtoa rushwa mashuhuri na aliyeiuwa NATIONAL MILLING..na ambaye wakati wa uchaguzi aliendeshwa puta sana na yule mgombea wa CHADEMA aliyepataga ajali...pia wanapendelea uzawa..kama ilivyo kawaida ya majimbo ya vijijini si rahisi kumpa mrema ..unless kama ile influence ya mrema kuwatatulia ule mgogooro mkubwa wa KANISA LA KKKT MERU kujitenga na KKKT kaskazini...kule wanamfahamu sana kwa kazi ile....ila evaluation ya haraka haraka siasa za arusha ni ngumu sana kwa asiye na mizizi ..ukiondoa ARUSHA MJINI....
 
Back
Top Bottom