Mrejesho wa kutafuta mchumba

wewe si kirahisi vile nataka nikupigie simu kila siku usiku saa 7 tuongee tena kwa sauti kwa muda wa mwezi mzima kabla ya chochote ujue mtu usiyemjua usimkurupukie kama zile risasi za Kinondoni mkuu
nipigie mm hata mwaka mfulilizo.
 
Mwanamke ukikosa bwana hata wa kukukamua mtaani kwako we ndio mwenye matatizo tena makubwa!! Unakuja tafuta mchumba JF na unawatangaza juu aseee no wonder umekosa hata kiben10 cha kukuliwaza panya wewe!
 
Hahahahahaha mkuu mimi ni mwanamke kabisa najua huwezi kuamini ila nilivyo ni ngumu kudanganywa na wanaume wenye akili ndogo mpaka uwe mjanja zaidi yangu
Yani we kama ni mwanamke kweli hujakutana na mwanaume mjanja na nakuombea usikutane nae usije leta thread ya kutaka jinyonga!!
 
Mwanamke ukikosa bwana hata wa kukukamua mtaani kwako we ndio mwenye matatizo tena makubwa!! Unakuja tafuta mchumba JF na unawatangaza juu aseee no wonder umekosa hata kiben10 cha kukuliwaza panya wewe!
Kwani nilikua natafuta hawara ?
 
Mwanamke ukikosa bwana hata wa kukukamua mtaani kwako we ndio mwenye matatizo tena makubwa!! Unakuja tafuta mchumba JF na unawatangaza juu aseee no wonder umekosa hata kiben10 cha kukuliwaza panya wewe!
Nmekosa mwenye sifa nizitakazo hlf kila mtu ana akili tofauti yawezekana mimi nilivutiwa kupata huku jf vipi una jingine ?
 
hahahah mpk uachane na yule mwanachuo anaekupigaga vimzinga vidogo vidogo...alafu uje upate vimzinga heavy huku
Haaa haa haa yule tulishapga chin
Ktambo ndo maana najileta
Kwako najua miznga yako

Hua inakuaga na huruma
Ndo nnachokupendea
 
Kwakweli mpaka nahakikishe
Inna amekaa kwenye 18 zang
I got you Comrade.

Ujue kila kitu kinazungumzika?, ni namna tu ya kutafuta msogeleo sahihi (Approach).

Yupo vizuri, Inna , Up-stairs the brain. Ukimkosa huyu mtoto, hutokaa uipate bahati kama hii. Trust me..

Impossible is nothing.
 
Habari zenu wanajukwaa.

Andiko hili nalileta kwenu ili kuwapa mrejesho wa kile nilichokiandika hapo juu.

Ni kama miezi miwili na kidogo nilileta tangazo la kutafuta mchumba hapa ktk jukwaa hili. Kweli watu walikuwa na muitikio mkubwa tuu mamia ya watu walinitafuta PM lakini duh nilikutana na vituko mpaka vinachekesha.

Ni vingi mno siwez kuwaelezea vyote ila nitawaelezea baadhi tuu ambavyo ni vya kushangaza zaidi;

Kituko no 1 ambacho kiliniacha mdomo wazi nilikutana PM na jamaa mmoja akajinadi weeee kama mtu. Akaomba tukutane nae tuongee vizuri kwa mapana nikamjibu hakuna tatizo nitakujuza ni lini siku ya kukutana, akanipatia namba tukaanza kuchat. Kumbe mimi namchunguza sehemu mbalimbali kwa kutumia ID yake siwez kukurupuka kukutana na mtu simjui lazima nifanye uchunguzi yakinifu.

Nikagundua jamaa ana mke tena ni mjamzito ila kwa wakati ule mke alikuwa kwao mkoani kujifungua. Nikazichukua picha za dada wa watu nikamtumia mumewe nikaandika na caption kuwa dhambi hiyo fanya mwenyewe. Jaman wanaume hawa!

Alishangaa nikamwambia usinitafute la sivyo nitampa taarifa mke wako alikuwa mpole akaniblock faster WhatsApp na miadi ya kuonana ikafa.

Kijeba no 2. Ni jamaa mmoja hiviiii tulipeana no tukazama inbox kila wakati mabusu moto inbox wacha wewe ila tatizo akiandika hatengi maneno mf. "Nipohapa".

Tukachatiiiii ila ukimtafuta usiku hapokei simu asubuhi ataniambia nilikua nimechoka nikalala fofofo, mara nilipata homa nikawa mbali na simu, mara mtandao wa shida nyakati za usiku ila yupo mjini Daslam tena kati.

Ikaja siku ya kukutana, tukaipanga siku ya kukutana sawa hee nikamwambia tukutane jirani na nyumbani kwako ikiwezekana nikutembelee. Jamaa akaanza sababu, mara vitu sijapanga ndani pako vuluvulu, tuanzie kukutana kwako. Nikaona kimeo nikampa block kwendaaaa

Njemba no 3 na 4. Hawa wanafanana kauli, kikwazo cha kuwatembelea makwao ni kwamba mmoja anaishi na mtoto wa dada'ake wa kike mwenye miaka 28 na mwingine anaishi na binamu yake miaka 26 wa kike anamsomesha, wanaishi nae wawili tuu kwahiyo nisiende kwanza tukutane bar. Hapo wewe kama una kauwezo kadogo tuu ka kufikiri jiongeze.

Binadamu no 6. Huyu ni kiboko, mwalimu huyu balaa tumechatiiiii mambo mengi sana ila nilipofika kwenye point ya kufika akasema ana mpango wa kuhama alipo kwahiyo nyumbani kwake vitu kavifunga vipo ktk mafurushi kwahiyo nisubiri ahamie kwingine ila mimi na yeye tukutane kwangu.

Mimi nikamwambia kwangu hapana mpaka nifike kwako sasa. Akasemaaaa tukutane hotelini nikamwambia poa. Etiii akaniuliza siku hiyo utarudi nyumbani au tuchukue room ili tuongee kiundani kabisa deeply? Nadhani alimaanisha maongezi gandamizi kuminywa. Kwikwikwi!

Niishie hawa tuu ila vituko vilikua vingi mnoooo ila mpaka sasa sijabahatika kukutana face to face na yeyote baada ya kuona yale tuu sikuingia humu tangu january lol na sitaki tena mchumba nimeshiba.
 
Hapo ngoma droo, wote mmeishia kuchunguzana, kila mmoja hataki kumpeleka mwenzake kwake,

Wewe hutaki kupeleka mgeni kwako na wao pia hawataki kupeleka mgeni kwao,

Nakushauri, ni bora ukubali kukutana na mtu bar kabla ya nyumbani kwake au kwako ,

kwanza itasaidia ikiwa mtu hutamridhia labda ki muonekano au hata namna ya uongeaji wake basi inakuwa rahisi tu quit mawasiliano,
 
Hapo ngoma droo, wote mmeishia kuchunguzana, kila mmoja hataki kumpeleka mwenzake kwake,

Wewe hutaki kupeleka mgeni kwako na wao pia hawataki kupeleka mgeni kwao,

Nakushauri, ni bora ukubali kukutana na mtu bar kabla ya nyumbani kwake au kwako ,

kwanza itasaidia ikiwa mtu hutamridhia labda ki muonekano au hata namna ya uongeaji wake basi inakuwa rahisi tu quit mawasiliano,
yawezekana sikua serious ila reaction yake inatia hofu unajua kabisa ni tapeli utaendelea kutaka kutapeliwa? :)
 
  • Thanks
Reactions: sab

Similar Discussions

Back
Top Bottom