Mrejesho wa kutafuta mchumba

Mrejesho wa kutafuta mchumba

Habari zenu wanajukwaa.

Andiko hili nalileta kwenu ili kuwapa mrejesho wa kile nilichokiandika hapo juu.

Ni kama miezi miwili na kidogo nilileta tangazo la kutafuta mchumba hapa ktk jukwaa hili. Kweli watu walikuwa na muitikio mkubwa tuu mamia ya watu walinitafuta PM lakini duh nilikutana na vituko mpaka vinachekesha.

Ni vingi mno siwez kuwaelezea vyote ila nitawaelezea baadhi tuu ambavyo ni vya kushangaza zaidi;

Kituko no 1 ambacho kiliniacha mdomo wazi nilikutana PM na jamaa mmoja akajinadi weeee kama mtu. Akaomba tukutane nae tuongee vizuri kwa mapana nikamjibu hakuna tatizo nitakujuza ni lini siku ya kukutana, akanipatia namba tukaanza kuchat. Kumbe mimi namchunguza sehemu mbalimbali kwa kutumia ID yake siwez kukurupuka kukutana na mtu simjui lazima nifanye uchunguzi yakinifu.

Nikagundua jamaa ana mke tena ni mjamzito ila kwa wakati ule mke alikuwa kwao mkoani kujifungua. Nikazichukua picha za dada wa watu nikamtumia mumewe nikaandika na caption kuwa dhambi hiyo fanya mwenyewe. Jaman wanaume hawa!

Alishangaa nikamwambia usinitafute la sivyo nitampa taarifa mke wako alikuwa mpole akaniblock faster WhatsApp na miadi ya kuonana ikafa.

Kijeba no 2. Ni jamaa mmoja hiviiii tulipeana no tukazama inbox kila wakati mabusu moto inbox wacha wewe ila tatizo akiandika hatengi maneno mf. "Nipohapa".

Tukachatiiiii ila ukimtafuta usiku hapokei simu asubuhi ataniambia nilikua nimechoka nikalala fofofo, mara nilipata homa nikawa mbali na simu, mara mtandao wa shida nyakati za usiku ila yupo mjini Daslam tena kati.

Ikaja siku ya kukutana, tukaipanga siku ya kukutana sawa hee nikamwambia tukutane jirani na nyumbani kwako ikiwezekana nikutembelee. Jamaa akaanza sababu, mara vitu sijapanga ndani pako vuluvulu, tuanzie kukutana kwako. Nikaona kimeo nikampa block kwendaaaa

Njemba no 3 na 4. Hawa wanafanana kauli, kikwazo cha kuwatembelea makwao ni kwamba mmoja anaishi na mtoto wa dada'ake wa kike mwenye miaka 28 na mwingine anaishi na binamu yake miaka 26 wa kike anamsomesha, wanaishi nae wawili tuu kwahiyo nisiende kwanza tukutane bar. Hapo wewe kama una kauwezo kadogo tuu ka kufikiri jiongeze.

Binadamu no 6. Huyu ni kiboko, mwalimu huyu balaa tumechatiiiii mambo mengi sana ila nilipofika kwenye point ya kufika akasema ana mpango wa kuhama alipo kwahiyo nyumbani kwake vitu kavifunga vipo ktk mafurushi kwahiyo nisubiri ahamie kwingine ila mimi na yeye tukutane kwangu.

Mimi nikamwambia kwangu hapana mpaka nifike kwako sasa. Akasemaaaa tukutane hotelini nikamwambia poa. Etiii akaniuliza siku hiyo utarudi nyumbani au tuchukue room ili tuongee kiundani kabisa deeply? Nadhani alimaanisha maongezi gandamizi kuminywa. Kwikwikwi!

Niishie hawa tuu ila vituko vilikua vingi mnoooo ila mpaka sasa sijabahatika kukutana face to face na yeyote baada ya kuona yale tuu sikuingia humu tangu january lol na sitaki tena mchumba nimeshiba.
Hakuna wachumba humu wengi ni wakandamizaji tu pole sana
 
Kwani humu MMu kuna wanaume wakuoa kweli humu, humu kuenjoy na kucheka tu. Nikijihisi Niko board nazama humu basi nacheka mpaka basi, lakini sio kuoa.

Utapoteza muda wako my
Hahahahahaha yani wewe acha tuu vituko mwingine aliniambia atoke moro aje akae kwangu siku mbili tuongee vizuri tupange mipango eti hana pa kufikia wengine tuliwashiana moto kabisa kuchambana kisa kuwapa live
 
We dawa yko ni kutafutiwa geto makini la kukodi, nauhakika siku iyo iyo nitakugegeda.
 
Yani ukitaka kumkamata tapeli mwambie akuoneshe kwake atasimama mita 200
Mimi naona yafuatayo.

Huu mtandao unasifika kwa members wake kuhitajika na jeshi la polisi, mtu asingetaka mkutane sehemu isiyo ya public kwa mara ya kwanza. Analinda usalama wake.

Unaweza usiwe askari vipi kama ni mwizi na ndo kwanza hatujajuana vizuri hata pa kukukamatia sina, ukija kwangu ukiniibia?

Kubwa kuliko, wanaume hua tunaepuka kumpeleka tunapoishi mwanamke asiye sahihi. Hatujaonana bado siwezi jua kama ni sahihi kwangu ama la na katika tabia inayokifu wanaume ni ya kukazana upajue home.

Hata hatujakutana unataka uje nyumbani!? Kweli? We ungekua mwanaume ungekubali?
 
Kwani humu MMu kuna wanaume wakuoa kweli humu, humu kuenjoy na kucheka tu. Nikijihisi Niko board nazama humu basi nacheka mpaka basi, lakini sio kuoa.

Utapoteza muda wako my
Kwahiyo maombi yangu huwezi kuyafanyia kazi?
 
ukiweka tangazo humu asilimia kubwa watakao kufuata ni wanaume ambao wameshaoa ila tamaa tu

me nafikir kijana alie serious hawezi kutamfuta mke dizain hii labda incase ikatokea kuna jambo fulan mmesaidiana huko pm mkazoeana hao atleast wanaweza kua na mahusiano serious..otherwise my dear muombe tu Mungu akuonyeshe ikiwa mtaani au humu kwa namna yoyote ile.njia za Mungu ni za ajabu
 
Mimi naona yafuatayo.

Huu mtandao unasifika kwa members wake kuhitajika na jeshi la polisi, mtu asingetaka mkutane sehemu isiyo ya public kwa mara ya kwanza. Analinda usalama wake.

Unaweza usiwe askari vipi kama ni mwizi na ndo kwanza hatujajuana vizuri hata pa kukukamatia sina, ukija kwangu ukiniibia?

Kubwa kuliko, wanaume hua tunaepuka kumpeleka tunapoishi mwanamke asiye sahihi. Hatujaonana bado siwezi jua kama ni sahihi kwangu ama la na katika tabia inayokifu wanaume ni ya kukazana upajue home.

Hata hatujakutana unataka uje nyumbani!? Kweli? We ungekua mwanaume ungekubali?
Yawezekana sikua serious kwenda makwao ni kuwapima tuu lkn reaction zao zina walakini unajua kabisa something fishy mkuu kuwa mpembuzi
 
Subiri subiri kaumri kasogee sogee utafikia hatua wala hutohangaika kutafuta kwa njia ya mtandao, utampata wa kukutana nae ana kwa ana mtaani, kazini, njiani, kanisani n.k
 
ukiweka tangazo humu asilimia kubwa watakao kufuata ni wanaume ambao wameshaoa ila tamaa tu

me nafikir kijana alie serious hawezi kutamfuta mke dizain hii labda incase ikatokea kuna jambo fulan mmesaidiana huko pm mkazoeana hao atleast wanaweza kua na mahusiano serious..otherwise my dear muombe tu Mungu akuonyeshe ikiwa mtaani au humu kwa namna yoyote ile.njia za Mungu ni za ajabu
Ktk kufanya assessment ni lazima uwe na maswali ambayo mtu hayatarajii na wew uwe makini na reaction ya huyo mtu ni rahisi sana kupata majibu mwenyewe
 
Back
Top Bottom