Elections 2010 Mrejesho wa barua ya mwanakijiji tume ya uchaguzi, Membe apata mpinzani

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Bernard Membe, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi na anayegombea tena ubunge katika jimbo hilo sasa kapata mpinzani kutoka TLP. Awali Msimamizi wa uchaguzi alikubali pingamizi la Membe dhidi ya mgombea huyo wa TLP kwamba wadhamini wake hawakuwa wamejiandikisha kupiga kura.

Baadaye Tume ya uchaguzi ilikubali rufani ya mgombea wa TLP na hivyo kumrejesha tena mgombea huyo, hivyo ina maana Membe sasa inabidi afanye kampeni.

Source: Kipindi cha Nipashe cha Radio One Sterio.

My take: 1. Ni haki wapinzani sasa wawe na wasiwasi kwa hawa ma-returning officers ambao ni makada wa CCM.

2. Kwa nini imechukua muda mrefu kuanzia 4.9.2010 hadi 28.9.2010 barua ya majibu ya rufani ya mgombea huyo wa TLP kumfikia kutoka NEC?
 
Ni nafasi pekee kwa watu wa Mtama, Nyangao, Nyengedi, Mahiwa, Namupa, Mtua na kwingineko kuonyesha hasira zenu dhidi ya mfumo dume kwa kumpatia kura zenu huyo mgombea wa Upinzania kupitia TLP. Achanane na imani kuwa Membe atakuja kuwa Rais...
 
Mfumo wa NEC kutoa taarifa za maamuzi ya rufaa una walakini mkubwa sana. Kwanini NEC haiandiki barua moja kwa moja kwa mgombea na kuandika nakala kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo? Hizi taratibu nyingine zinafanya kazi in favor of CCM, tusije kushangaa wiki ya mwisho ya Kampeni tukiambiwa kuna rufaa nyingine imekubaliwa.
 
Nina mashaka na NEC hasa wasimamizi wake huko majimboni.
Hili dubwasha lapaswa kufumuliwa na kuundwa upyaa tukianzia sheria yake, kanuni mpaka watendaji.
Nina mashaka si utani
 
Crazy NEC, walikuwa wapi muda wote huo? Haihitaji kwenda shule kujua taratibu za kazi za NEC ni rahisi mno lakini wanavyocomplicate ndivyo wanavyofanya mambo kuwa magumu. NEC watamaliza maisha yao vibaya, kwani kama wanajua watz bado twalala wasahau kabisa. Bora watende haki kwa maana hawatabaki NEC muda wote.

Mfumo wao unamashaka kila kona sijui hawalioni hilo. Anyway, ngoja tusubiri muda ukifika tutaona itakavyokuwa.
 
Nina mashaka na NEC hasa wasimamizi wake huko majimboni.
Hili dubwasha lapaswa kufumuliwa na kuundwa upyaa tukianzia sheria yake, kanuni mpaka watendaji.
Nina mashaka si utani

Hapo ndipo ambapo kuna matatizo makubwa kwa kutumia sheria ya uchaguzi wa sasa. Hao wasimamizi ni waajiriwa wa TAMISEMI. Wasimamizi ambao wameonyesha kuwa makini tayari wameishahamishwa. Wiki iliyopita Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kapigwa transfer. Jana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kahamishwa. Wote hao inasemekana sababu za uhamisho zinahusiana na uchaguzi mkuu. Wasimamizi wengine wakishaanza kuona hizo transfer watapata kiwewe na kuanza kuboronga zaidi in favor of CCM.
 
Ni nafasi pekee kwa watu wa Mtama, Nyangao, Nyengedi, Mahiwa, Namupa, Mtua na kwingineko kuonyesha hasira zenu dhidi ya mfumo dume kwa kumpatia kura zenu huyo mgombea wa Upinzania kupitia TLP. Achanane na imani kuwa Membe atakuja kuwa Rais...
Its too late, na mbaya zaidi wanajua kuwa Membe atakuwa Rais baada ya (Kikwete, Slaa, Lipumba............)
 
msimamizi wa uchaguzi nimmkurugenzi wa mji, wilaya etc ajira yake purely ni ya kiserikali je unategemea nini. Akileta unoko anapelekwa wizarani bench na msoto.
 
matokeo haya ni muhimu sana kwa mustakabali wa demokrasia nchini.........hureeee tlp japo mnamnadi kikwete badala ya rais wenu
Bernard Membe, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi na anayegombea tena ubunge katika jimbo hilo sasa kapata mpinzani kutoka TLP. Awali Msimamizi wa uchaguzi alikubali pingamizi la Membe dhidi ya mgombea huyo wa TLP kwamba wadhamini wake hawakuwa wamejiandikisha kupiga kura.

Baadaye Tume ya uchaguzi ilikubali rufani ya mgombea wa TLP na hivyo kumrejesha tena mgombea huyo, hivyo ina maana Membe sasa inabidi afanye kampeni.

Source: Kipindi cha Nipashe cha Radio One Sterio.

My take: 1. Ni haki wapinzani sasa wawe na wasiwasi kwa hawa ma-returning officers ambao ni makada wa CCM.

2. Kwa nini imechukua muda mrefu kuanzia 4.9.2010 hadi 28.9.2010 barua ya majibu ya rufani ya mgombea huyo wa TLP kumfikia kutoka NEC?
 
Kuanzia Tendwa (Msajili)
Makame lewis (NEC) naona wamekalia madudu na majungu dhidi ya upinzaia tanzania. Najua wanalinda ajira zao.
sasa tegemea baada ya jaji mkuu kustaafu baadae anateuliwa kuwa mwenyekiti wa taasisi kama hizi ndipo ujue kuwa uzembe wa hawa unaanzia mbali sana kwa kigezo cha maisha baada ya kustaafu.
 
safi sana hii imenipa siku yangu kuwa njema sana.Kuna mtu amesema membe atakuwa rais badala ya kikwete?sijaelewa maana mimi nachoamini ni kuwa kikwete anatoka Dr.Slaa ndo prezida sasa Membe anakuwa rais wapi?
 
Ni fursa ya Chadema kuitumia katika jimbo hilo kumpigia kampeni huyo mgombea ili waindoshe ccm madarakani
 
mwezi na ushee ndiyo majibu yanatoak, anyway bado muda unaruhusu kufanya mabadiliko
 
Inawezekana kuna mkono wa EL katika hili. Nasikia wawili hawa -- Membe na EL hazungumzi kwa miaka 4 sasa, kwani wote macho yao yako 2015. Mafweza ya EL, sorry ya Watz aliyowapora, yanamuwezesha EL kufanya vitu kama hivi. Tumeona jinsi ma-returning officers wawili wa Arusha Mjini na Hai walivyon'golewa ili kukidhi malengo yake.
 
Hii ni dhuluma isiyokuwa na kipimo.

NEC wanawajibika kwa hili kwani haiwezekani ukamdhulumu mtu haki yake ya kupiga kampeni na kuwafikia watu. Kwa nini majibu ya rufani yapelekwe kwa msimamizi wa uchaguzi na si mrufani? Kwa hiyo hata kama mrufani atashindwa kwenye uchaguzi atakuwa na haki ya kupinga matokeo kutokana na kudhulumiwa haki yake ya kufanya kampeni kama wagombea wengine.

Itabidi na NEC wamlipe kwani nao wameshiriki katik kumhujumu. Haiingii akilini kuona kuwa Jaji Makame bado anasema kuwa tume yake inasimamia uchaguzi ambao ni huru na haki wakati ukweli kuwa tume hiyo ipo kuwapotosha utashi wa Watanzania. Jaji Makame na tume yako yote mnatakiwa mjiuzulu.
 
Inawezekana kuna mkono wa EL katika hili. Nasikia wawili hawa -- Membe na EL hazungumzi kwa miaka 4 sasa, kwani wote macho yao yako 2015. Mafweza ya EL, sorry ya Watz aliyowapora, yanamuwezesha EL kufanya vitu kama hivi. Tumeona jinsi ma-returning officers wawili wa Arusha Mjini na Hai walivyon'golewa ili kukidhi malengo yake.

Umepatia kabisa hapo mkuu! Hii ni kazi mzuri ya EL, RA, Chenge & Co kuudhohofisha mtandao. Na wanafanikiwa sana, mzee Malecela ni victim wao wa kwanza. Mwakyembe na Sitta waanze kutia maji vichwa vyao. EL for 2015, take my words.
 
Back
Top Bottom