Mrejesho: Tatizo langu la kupata mkojo tena dakika chache kila baada ya kumaliza kukojoa

Wakuu Leo nimeleta mrejesho wa tatizo langu la kukojoa Mara kwa mwara na kupata mkojo Tena kila napomaliza kukojoa baada ya dakika kadhaa nabanwa Tena na mkojo yaan kiufupi mkojo hausishi.

Wakuu nilifuata ushauri wenu nikafika Muhimbili kitengo cha urology nikamuelezea daktar kila kitu, daktari akaelekeza nikafanyiwe vipimo vya damu,ultrasound na mkojo.

Majibu yaliyotoka ya vipimo ya sina ugonjwa wowote na wakati nafanyiwa kipimo Cha ultrasound nimemaliza wakanambia kakojoe uje tuendelee kufanya kipimo nilipoenda kukojoa nikakojoa kuumaliza mkojo wote Ila baada ya kurud kuendelea na kipimo wakapima Tena ultrasound wakaona kibofu kina mkojo tena, nikawaambia hilo ndio tatizo langu sasa.

Ikabidi waendelea kuangalia ini ktk mbavu chembe ya moyo koote hawakuona kitu wakasema labda huyu afanyiwe kipimo wakataja kipimo sjui kipimo gani skukielewa walitaja kingereza. Kesho yake nilirudi kwa daktar akanisomea majibu akasema majibu yanaonyesha hakuma chochote tezi dume iko sawa ndogo Sana pia kibofu kipo sawa pia figo ziko sawa pia nakipimo Cha damu kipo sawa.

Dokta akanambia inabid Sasa labda ufanyiwe kipimo cha kupitisha kifaa ktk tundu la njia yamkojo mpaka katika kibofu kuangalia kuna nin shida hapo...kiukweli mimi niliwazaaa hili lakupitisha kifaa katika njia yamkojo nkaogopa ikabid nimfiche daktari kuwa kwasasa sinapesa yakopimo mpaka baada miezi mitatu ikizingatia naishi mkoani basi daktari akawa kaniandikia nirudi mwezi wanne kwa ajili ya hiko kipimo
Wakuu huu ndio mrejesho wangu je kipimo hicho nilichoandikiwa je ni salama kweli kwa afya ya uume wangu na njia pia ya mkojo.

Utakuwa na enlarge prostatic ambayo inatokea kwa umri unavyoenda. Mimi nimekuwa na matatizo kama yako nimefanyiwa hii procedure na tatizo linaisha polepole. Watakupa dawa ya flomax utumie inasaidia kulegeza misuli na kukupa unafuu kwa muda ni kidonge kimoja kwa siku. Hii procude mpya Rezum ndiyo nimefanyiwa Sijui kama ipo Tanzania lakini ni best 🙏 lakini inabidi size isizidi cc 80 ili iwe best option hivyo usisubiri sana . Mimi nimefanyiwa Sept 5 na nimeshapata mafuu sana na tarehe 26 mwezi huu wanaenda kunitoa kwenye dawa kabisa

Rezūm Therapy is typically performed right in your urologist’s office, or at an outpatient surgery facility and completed in one short appointment.

During each 9-second treatment, sterile water vapor is released throughout the targeted prostate tissue. When the steam contacts the prostate tissue, all the stored energy is released into the tissue. Your doctor will determine the amount of treatments you need, based on the size of your prostate.

Over time, your body’s natural healing response absorbs the treated tissue, shrinking the prostate. With the extra tissue removed, the urethra opens, reducing BPH symptoms.

Most patients begin to experience symptom relief in as soon as two weeks, and maximum benefit may occur within three months.*1,2 Patient responses can and do vary.
 
Attachments

  • B3524A79-5BF8-42CB-9A69-5D42261F3E67.png
    B3524A79-5BF8-42CB-9A69-5D42261F3E67.png
    109 KB · Views: 4
Jaribu pia kupunguza gharama, ulishawahi kunitajia gharama ya dawa ya pumu nilichoka mwenyewe.

Nashukuru Mungu mwanangu amepona kwa gharama nafuu.
Kuna rafiki yangu mtoto wake anateswa na kifua sana
 
Inaitwa Cystoscopy , haina maumivu yoyote mkuu.

Hutumika kuangalia kama Kibofu cha mkojo kina shida

Hichi kipimo nimefanyiwa ni lazima kabla ya kufanya surgery maana ni kamera ndani ya kibofu cha mkojo. Ushauri ukizia procedure ya Rezum na kama haipo ni bora utafute pesa uende kenya au South Africa. Lakini usifanye surgery kubwa wakati kuna hii na bado haitaharibu chochote ni procedure mpya sana lakini kuwa makini na zile za zamani wasije wakaharibu nguvu zako za kiume
 
Jaribu pia kupunguza gharama, ulishawahi kunitajia gharama ya dawa ya pumu nilichoka mwenyewe.

Nashukuru Mungu mwanangu amepona kwa gharama nafuu.
Huyo jamaa Mzizimkavu ni noma ni Mganga wa kienyeji alikuwa akiishi Uturuki mimi niliongea naye kwenye simu ndipo nilipomgunduwa kuwa mpiga pesa tu.
 
Wakuu Leo nimeleta mrejesho wa tatizo langu la kukojoa Mara kwa mwara na kupata mkojo Tena kila napomaliza kukojoa baada ya dakika kadhaa nabanwa Tena na mkojo yaan kiufupi mkojo hausishi.

Wakuu nilifuata ushauri wenu nikafika Muhimbili kitengo cha urology nikamuelezea daktar kila kitu, daktari akaelekeza nikafanyiwe vipimo vya damu,ultrasound na mkojo.

Majibu yaliyotoka ya vipimo ya sina ugonjwa wowote na wakati nafanyiwa kipimo Cha ultrasound nimemaliza wakanambia kakojoe uje tuendelee kufanya kipimo nilipoenda kukojoa nikakojoa kuumaliza mkojo wote Ila baada ya kurud kuendelea na kipimo wakapima Tena ultrasound wakaona kibofu kina mkojo tena, nikawaambia hilo ndio tatizo langu sasa.

Ikabidi waendelea kuangalia ini ktk mbavu chembe ya moyo koote hawakuona kitu wakasema labda huyu afanyiwe kipimo wakataja kipimo sjui kipimo gani skukielewa walitaja kingereza. Kesho yake nilirudi kwa daktar akanisomea majibu akasema majibu yanaonyesha hakuma chochote tezi dume iko sawa ndogo Sana pia kibofu kipo sawa pia figo ziko sawa pia nakipimo Cha damu kipo sawa.

Dokta akanambia inabid Sasa labda ufanyiwe kipimo cha kupitisha kifaa ktk tundu la njia yamkojo mpaka katika kibofu kuangalia kuna nin shida hapo...kiukweli mimi niliwazaaa hili lakupitisha kifaa katika njia yamkojo nkaogopa ikabid nimfiche daktari kuwa kwasasa sinapesa yakopimo mpaka baada miezi mitatu ikizingatia naishi mkoani basi daktari akawa kaniandikia nirudi mwezi wanne kwa ajili ya hiko kipimo
Wakuu huu ndio mrejesho wangu je kipimo hicho nilichoandikiwa je ni salama kweli kwa afya ya uume wangu na njia pia ya mkojo.
Mkuu ili tatizo ushapona?
 
ikabid nimfiche daktari kuwa kwasasa sinapesa yakopimo mpaka baada miezi mitatu ikizingatia naishi mkoani basi daktari akawa kaniandikia nirudi mwezi wanne kwa ajili ya hiko kipimo
Wakuu huu ndio mrejesho wangu je kipimo hicho nilichoandikiwa je ni salama kweli kwa afya ya uume wangu na njia pia ya mkojo.
Huoni kuwa umemnyima ushirikiano Dr wako? Je na yeye akikudanganya utajisikiaje?
 
Mkuu pole kwa tatizo. Once a time nilikuwa na tatizo kama lako ila nashukuru liliisha lenyewe tu nilikuwa napata tabu sana especially at night dah 😂... Ilikua ni full kutoka toka nje hadi manzi yangu akawa hanielewi mwanzoni nilijua labda ni kunywa maji mengi kunasabisha nikaacha kabisa kunywa maji inapokaribia usiku lakini wapi tatizo likawa pale pale.

Kwa sasa nashkuru limepona lenyewe na niko fresh kabisa.... so mkuu hata ww usikate tamaa utakaa sawa cha muhimu jaribu kufanya sana mazoezi ya pelvic ili kufanya misuli ya pelvic kuwa imara. Punguza mawazo au ile psychology ya kwamba ukikojoa muda si Mrefu utakojoa tena hali hiyo inafanya ubongo unakuwa wired automatically na hivyo utaendelea kuenda na hiyo hiyo routine. Jitahidi ukiwa unakojoa from one interval to another uchukue a reasonable space kwahiyo utalazimika kubana haja ikikupata kwa haraka toka ulivopata haja ya kwanza kwa kufanya hivyo utaji condition automatic kutoenda haja mara kwa mara.
 
Inaweza ikawa una makovu kwenye njia ya mkojo ambayo inaweza kuwa imesababishwa na infections za kipindi cha nyuma sana kwenye njia ya mkojo zilizosababishwa na magonjwa kama UTI nk
Yeah hii pia inasababisha sana
 
Back
Top Bottom