Mrejesho: Tatizo langu la kupata mkojo tena dakika chache kila baada ya kumaliza kukojoa

malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
2,780
2,704
Wakuu Leo nimeleta mrejesho wa tatizo langu la kukojoa Mara kwa mwara na kupata mkojo Tena kila napomaliza kukojoa baada ya dakika kadhaa nabanwa Tena na mkojo yaan kiufupi mkojo hausishi.

Wakuu nilifuata ushauri wenu nikafika Muhimbili kitengo cha urology nikamuelezea daktar kila kitu, daktari akaelekeza nikafanyiwe vipimo vya damu,ultrasound na mkojo.

Majibu yaliyotoka ya vipimo ya sina ugonjwa wowote na wakati nafanyiwa kipimo Cha ultrasound nimemaliza wakanambia kakojoe uje tuendelee kufanya kipimo nilipoenda kukojoa nikakojoa kuumaliza mkojo wote Ila baada ya kurud kuendelea na kipimo wakapima Tena ultrasound wakaona kibofu kina mkojo tena, nikawaambia hilo ndio tatizo langu sasa.

Ikabidi waendelea kuangalia ini ktk mbavu chembe ya moyo koote hawakuona kitu wakasema labda huyu afanyiwe kipimo wakataja kipimo sjui kipimo gani skukielewa walitaja kingereza. Kesho yake nilirudi kwa daktar akanisomea majibu akasema majibu yanaonyesha hakuma chochote tezi dume iko sawa ndogo Sana pia kibofu kipo sawa pia figo ziko sawa pia nakipimo Cha damu kipo sawa.

Dokta akanambia inabid Sasa labda ufanyiwe kipimo cha kupitisha kifaa ktk tundu la njia yamkojo mpaka katika kibofu kuangalia kuna nin shida hapo...kiukweli mimi niliwazaaa hili lakupitisha kifaa katika njia yamkojo nkaogopa ikabid nimfiche daktari kuwa kwasasa sinapesa yakopimo mpaka baada miezi mitatu ikizingatia naishi mkoani basi daktari akawa kaniandikia nirudi mwezi wanne kwa ajili ya hiko kipimo
Wakuu huu ndio mrejesho wangu je kipimo hicho nilichoandikiwa je ni salama kweli kwa afya ya uume wangu na njia pia ya mkojo.
 
Mkuu Pole sana kuhusu hicho kipimo cha kutia katika tundu la dushelele lako hakina ubaya. Nikuulize swali unakuw amtu mwenye mawazo sana? na ninahisi utakuwa na maradhi yanayotokana na mambo ya giz aikiwa vipimo vyote umepima na hakuna maradhi yaliyo onekana basi utakuwa unayo maradhi ya kichawi . Ushauri wangu pia jaribu utibiwe na dawa zetu za asili ili uweze kupata kupona ikiw aunaogopa kutiwa kipimo katika dushelele lako.
 
Mkuu Pole sana kuhsu hicho kipimo cha kutia katika tundu la dushelele lako hakina ubaya. Nikuulize swali unakuw amtu mwenye mawazo sana? Na ninahisi utakuwa na maradhi yanayotokana na mambo ya giza aikiwa vipimo vyote umepima na hakuna maradhi yaliyo onekana basi utakuwa unayo maradhi ya kichawi . Ushauri wangu pia jaribu utibiwe na dawa zetu za asili ili uweze kupata kupona ikiwa unaogopa kutiwa kipimo katika dushelele lako.
Muhakikishie kama akipona ndiyo alipie bidhaa maana ni kama umeiona fursa hivi
 
Wakuu Leo nimeleta mrejesho wa tatizo langu lakukojoa Mara kwa mwara nakupata mkojo Tena kila napomaliza kukojoa baada ya dakika kadhaa nabanwa Tena namkojo yaan kiufupi mkojo hausishi...
Nakumbuka uzi wako ule dah pole sana kumbe bado hujapata nafuu, hicho kipimo daktari amekuambia kitagharimu kiasi gani cha pesa
 
Wakuu Leo nimeleta mrejesho wa tatizo langu lakukojoa Mara kwa mwara nakupata mkojo Tena kila napomaliza kukojoa baada ya dakika kadhaa nabanwa Tena namkojo yaan kiufupi mkojo hausishi...
Ningeshauri utafute hospitali ingine pia nenda hata kcmc jaribu kufanyiwa hicho kipimo
 
Muhakikishie kama akipona ndiyo alipie bidhaa maana ni kama umeiona fursa hivi
Nita muhakikishia kupona kwani mimi ni Mungu? Kuna binadamu ana Garanti ya binadamu mwenzake? Mimi nimempa ushauri akitaka ataufuata ushauri wangu asipo taka aendelee na Hospitali mpaka ajuwe mwisho wake. Je wewe ingelikuwa una uwezo wa kumtibia mtu ungeweza kumuhakikishia kuwa atapona maradhi yake ukimtibia?
 
Sukari nayo uleta hilo tatizo.sukari uja kwa njia tofauti sana ambazo zengine si rahisi kuzigundua.

Hata hilo la kukojoa ni nililiona kwenye symptoms za sukari

Note

Imeandikwa na ULY CLINIC

Kukojoa mara kwa mara

Kukojoa mara kwa mara husababishwa na nini

Kukojoa mara kwa mara ni hali ya kuhisi haja ya kwenda kukojoa zaidi ya kawaida yako, unaweza kuwa unakojoa kiwango kikubwa cha mkojo kuliko kawaida ama kiasi kidogo kidogo na mara nyingi.

Kukojoa mara kwa mara huweza kutokea wakati wa mchana au usiku tu au wakati wote yaani usiku na mchana, hii ina maana sana katika tiba na unatakiwa mwelezea daktari wako unakojoa mara kwa mara wakati gani.

Kukojoa mara kwa mara huweza kuathiri hali ya usingizi, kazi ama utu wako.

Visababishi ni nini?

Kukojoa mara kwa mara huweza kusababishwa na magonjwa yanayoathiri sehemu yoyote ile ya mfumo wa mkojo. Mfumo wa mkojo huhusisha figo, mirija ya mkojo (ureter) inayotoka kwenye figo mpaka kwenye kibofu, kibofu cha mkojo, na mrija unaotoa mkojo nje ya mwili (urethra)

Mambo mengi yanaweza kuambatanishwa na kukojoa mara kwa mara ni;

Maambukizi au magonjwa kwenye kibofu cha mkojo
Hali zinazoongeza uzalishaji mkojo kwa wingi
Mabadiliko katika misuli, mishipa ya fahamu ya kibofu cha mkojo
Matumizi ya dawa za kutibu saratani
Matumizi ya dawa na vinywaji vinavyoongeza uzalishaji wa mkojo

Ikitegemea nini kinachosababisha kukojoa mara kwa mara, unaweza kupata dalili zingine kama

Maumivu au kupata shida wakati unakojoa
Kukojoa kwa kutumia nguvu
Kutoa mkojo kwa shida
Kushindwa kuzuia mkojo kutoka
Rangi ya mkojo kubadilika

Magonjwa yanayosababisha kukojoa mara kwa mara ni haya yafuatayo;

Wasiwasi uliopitiliza
Kuvimba kwa tezi dume
Mawe katika kibofu cha mkojo
Kubadilika kwa ufanyaji kazi wa figo
Kisukari
Matumizi ya dawa kundi la diuretics (zinazoongeza kukojoa)
Kunywa maji mengi au vyakula vya majimaji kwa wingi
Maambukizi kwenye kibofu
Maambukizi ya figo
Kufanya kazi kupita kiasi kwa kibofu cha mkojo
Ujauzito
Maambukizi kwenye tezi dume (prostitis)
Matibabu ya mionzi sehemu ya chini ya tumbo ama nyonga
Kuziba kwa mrija wa mkojo wa urethra
Kushindwa kwa kibofu kutunza mkojo wa kutosha
Maambukizi ya njia ya mkojo(UTI)
Maambukizi kwenye uke
 
Mkuu Pole sana kuhsu hicho kipimo cha kutia katika tundu la dushelele lako hakina ubaya. Nikuulize swali unakuw amtu mwenye mawazo sana? Na ninahisi utakuwa na maradhi yanayotokana na mambo ya giza aikiwa vipimo vyote umepima na hakuna maradhi yaliyo onekana basi utakuwa unayo maradhi ya kichawi . Ushauri wangu pia jaribu utibiwe na dawa zetu za asili ili uweze kupata kupona ikiwa unaogopa kutiwa kipimo katika dushelele lako.
mkuu acha atibiwe na tiba rasmi usimshauri mambo ya shirki
 
Nita muhakikishia kupona kwani mimi ni Mungu? Kuna binadamu ana Garanti ya binadamu mwenzake? Miminimempa ushauri akitaka ataufuata ushauri wangu asipo taka aendelee na Hospitali mpaka ajuwe mwisho wake. Je wewe ingelikuwa una uwezo wakumtibia mtu ungeweza kumuhakikishia kuwa atapona maradhi yake ukimtibia?
Kama ingekua ndiyo mimi yes Inategemea na uhakika wa tiba yangu nayotaka kumpa of course nitampa guarantee, kama ninaiamini tiba yangu kwanini nisimpe matumain eti
 
Kama ingekua ndiyo mimi yes Inategemea na uhakika wa tiba yangu nayotaka kumpa of course nitampa guarantee, kama ninaiamini tiba yangu kwanini nisimpe matumain eti
Hata Huko Hospitali Hakuna hata Daktari mmoja anayetoa Garanti kwa mgonjwa kuwa akimtibia mgonjwa atapona Itakuwa wewe unaye sema maneno ya uongo?

Unayo garanti ya kumponyesha mgonjwa kwani wewe ni Mungu? Mungu peke yake ndio mwenye garanti ya kumponyesha viumbe wake hakuna binadamu yoyote yule mwenye uwezo wa kumponyesha binadamu mwenzake pasipo na idhini toka kwa Mungu.
 
Hata Huko Hospitali Hakuna hata Daktari mmoja anayetoa Garanti kwa mgonjwa kuwa akimtibia mgonjwa atapona Itakuwa wewe unaye sema maneno ya uongo? Unayo garanti ya kumponyesha mgonjwa kwani wewe ni Mungu? Mungu peke yake ndio mwenye garanti ya kumponyesha viumbe wake hakuna binadamu yoyote yule mwenye uwezo wa kumponyesha binadamu mwenzake pasipo na idhini toka kwa Mungu.
Huna haja ya kupaniki
 
Pole sana mkuu
nikuulize maswari machache hunijibu

1*je kasi (presha ya mkojo) imepungua
yaan unajikwinya sana kuutoa mkojo
2*je mkojo hutoka ukiwa mwembamba sana(yaan ukubwa wa mkojo vile unatoka upo tafauti na zamani)
3*je wakati mwingne mkojo hutoka km mabomba mawiri au matatu yaan hutawanyika hasa km ukiwa umetoka kuamka
4*je ukimaliza kukojoa ushafunga zipu huwa unajihisi km chembechembe za mkoja zinatoka zinamalizia
5*umeoa au unaishi na mwanake au mpenz ambaye mnakutana(sex) mara kwa mara
6*je huwa unafanya au uliwahi kuwa unafanya punyeto sana
7*je chini ya mbavu au juu ya kitovu pande zote huwa unajihisi maumibu makari hasa mkojo ukiwa umekubana ?
8*kutoka kwenye mbavu kuja kwenye kibovu huwa unahisi km kuna tube(mithiri km bomba) zinawaka moto au maumivu yanafanana na kidonda km kimewekwa ndimu
8*je huwa unahisi maumivu kwenye kibofu yaan kibofu km kinawaka moto mitihili kidonda kilichowekwa ndimu
9*ukimaliza kukojoa huwa unahisi ahueni kubwa kwenye kibofu mpk ureta ambayo udumu kwa muda mchache
10*je kiasi cha mkojo huwa unatoa kwa wingi kutokana ns kukuuma kwa kasi au ni kwa uchache mkojo wa asubuhi huwa unakoa kwa uchache pia
11* je hilo tatizo tangu limekuanza lina muda gani ?
12* swali la mwisho je imefikia hstua unaogopa kunywa maji mengi kuhofia mkojo?
 
Back
Top Bottom