MREJESHO: Social anxiety, depression, panic attack vinanitesa, vinaniua taratibu

Mungu atakufanyia njia naamini huu ndo mwanzo. Hongera sana kuongea na kushare masumbuko yako kwa watu inasaidia sana
 
MWENZIOO WAMESHAMFUKIA SHAURI YAKO....MEMBER W HUMU
ALIJAZA MAPOST YAKE HIVI HIVI KIUTANI KANYWA SUMU
MPAKA LEO ANA RIP 4898 SIJAJUA MCHANA HUU
ENDELEAA

Sijakuelewa Mkuu, unamaanisha natania au?
 
JERUSALEMA pole sana tena sana kwa maswahibu hayoo iyo hali inatesa sana sio siri,ila ni hali ya kuweza kuondokana nayo usiwe mtumwa wa ivo vitu ,jitazame kwenye kioo sehemu tulivu jiangalie kwa muda uso kwa uso,kwa dk kadhaa tabasamu,kwa dk kadhaa kunja sura kwa dk kadhaa fanya hali flani,kwa dk kadhaa ongea
Fanya ivo kwa muda flani,

Jaribu kujiita jina lako anza kwa sauti ya chini, alafu ongeza sauti isiwe sana



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye njia yako upo mwenyewe. Hakuna atakayetembea kwa ajili yako bali wewe ndiye mtembezi. Iweje unajiwekea uzio kwenye njia yako? Hiyo hali unao uwezo wa kuiepuka! Punde utakapoanza kutembea tu njia utaiona.

Inakubidi utembee kwenye safari, safari ambayo utaidhibiti hiyo hali yako. Wala haina masafa wala urefu wa aina yoyote baina ya hiyo safari na wewe isipokuwa ni fikra uliyoizalisha wewe mwenyewe.

Tatizo lipo kwenye fikra umejiwekea gereza! Na kwa nini ujiweke kwenye gereza wakati milango yake ipo wazi?

Kazi iliyopo mbele yako si kutafuta madawa ama vitu kama hivyo, bali ni ya kutafuta barriers zote zilizomo ndani yako wewe mwenyewe ambazo umezijenga kwa fikra zako wewe mwenyewe zitafute na uzivunje. Na ni kitu rahisi kwako kwa sababu najua uwezo wa kuzivunja hizo barriers unao.

Jiweke huru! Jiamini. Hisiya za uoga zikikuvaa usiziruhusu zikuvae. Jiambie hapana! Mimi ni jasiri na usiviweke sana vitu kichwani. Chochote utakachokiweka sana kichwani kitakuendesha. Ukiiweka sana pesa kichwani zitakuendesha! Akiwa ni mwanamke atakuendesha! Muhimu ni kutoruhusu hiyo hali ikutawale.

Jichanganye na watu vilevile na zungumza nao hata kuelezea hiyo hali kwani vitu vingine vinaondoka kwa kuzungumza na watu kuna faida utaipata.

Umezaliwa ukiwa na mabawa, usiruhusu utambae.
 
JERUSALEMA iyo hali usijichukie binafsi niliteseka sana japo nilikua sijijui Ila nilikua najiona tofauti na wengine kipind nipo sec had chuo,nafikiri kama sio kukulia uswazi ningekua na tatizo zaid, watu wengi wanañijua mi siwajui majina zaid ya sura tu, nilipenda kujitenga mno mpka wenzangu wakawa wananiogopa,

Hakuna hali iliyokua inanitesa kama kulala ktk hadhara mfano kanisani,darasani na mahali penye utulivu, sio siri nilikua naaibika sana sana sana yote ni kwasababu siwezi kaa mahala penye utulivu lazima nilale,hakuna aliekua hanijui so mwalimu mpya au wazamani kama mi nalal punde tu anapoingia darasani

Niliteseka mno ila sikujichukia kupitiliza na kwasababu nilikua sijui kama ni tatizo

Mimi sikua muongeaji ,nikipointiwa moyo utanipasuka nikiongea sijui nasema nini,nikimaliza kuongea naanza kujidoubt ivi wamenielewa au nilikua napiga kelele tu,


Nitaongea na MTU au watu akinishauri zuri kuhusu mim nabaki natabasamu tu,huku nafsin natamani aondoke niwe peke angu,akianza kuonyesha dalil ya kuniacha nitachangamka kumbe nafurahi aondoke


Hadi nakua Mimi nimekua ni MTU wa kukaa sehemu moja au kulala sana, sipendi sehemu iliyotulia,

Kuna siku mazazi alinikera nikatamani kujiua Ila nikagairi kwanza nilisonya kwa kile kitendo nilichokua nataka kufanya,ile hali ikaondoka kabisa basi hadi saiv wazo baya likinijia nasonya hapo hapo linavurugika

Mkuu JERUSALEMA umri umeenda tafuta mke mpate watoto hao pia watakua tiba yako,usipate mke aliepoozaa tafuta aliechangamka

Ila malezi pia yanachangia hii hali sio siri ,tunavyolea watoto wetu tuwe makini hasa wale wenye maisha mazuri,wale wa uswazi hii hali kwao ni ngumu mtoto kuiexpirience, mi wazazi walinilea vizur ila kuna malezi waliya overdoz,
 
JERUSALEMA pole sana tena sana kwa maswahibu hayoo iyo hali inatesa sana sio siri,ila ni hali ya kuweza kuondokana nayo usiwe mtumwa wa ivo vitu ,jitazame kwenye kioo sehemu tulivu jiangalie kwa muda uso kwa uso,kwa dk kadhaa tabasamu,kwa dk kadhaa kunja sura kwa dk kadhaa fanya hali flani,kwa dk kadhaa ongea
Fanya ivo kwa muda flani,

Jaribu kujiita jina lako anza kwa sauti ya chini, alafu ongeza sauti isiwe sana



Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kuwa nimeshafanya na still naendelea kufanya tiba ya hivi nimekuelewa vizuri sana
Sijui na mleta uzi atakuelewa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugonjwa wa akili ni ugonjwa kama magonjwa mengine. Mtu akiwa na malaria au typhoid haaimbiwi aache kujiendekeza au aangalie video YouTube au amrudie mungu ndo apone.

Brain inaendeshwa kwa chemical reaction sasa zisipo balance ndo mtu anapata shida kama hizi.

Nicheki pm. Naweza kukusaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CONTROLA mdogo wangu, Naomba upite hapa.!!
JERUSALEMA wadau wamekushauri mengi sana na naomba nikuambie kuwa Mungu akazidi kukupigania akawe ngao na mlinzi wako muda si mrefu kutoka sasa unakwenda kuivunja vunja kabisa hiyo minyororo ya adui.!
Wewe ni Mshindi..!!
Be Positive, Just be Positive, We are here to support you in Prayers.!

btw, nilivyosoma tu jina lako jipya this song came to my mind..
 

Attachments

  • master_kg_ft_nomcebo_jerusalema_lyrics_video_h264_11690.mp4
    7.9 MB
Hii ni shida ....
Sisemi mengi....
maana ... tunaoumwa ni wengi nusu na wazima.

Angalia movie zenye kufurahisha...labda comedy ..sio zenye kufikirisha..

Jichanganye na tafuta marafiki hata humu wamo wa kuongea mkafurahi...hii itakusaidia sana..taratibu utaanza kuiona tofauti

Hii kutumia dawa..liepuke sana ..utakuwa teja wa dawa hizo maisha..jitahidi utafanikiwa...inuka...

Ukipata Maalim mzuri...atakusomea ..hiyo hofu itaondoka.....na haiathiri imani yako..

Epuka kukaa kimya sana na upweke...

Mimi nimetoka mbali sana...hadi kufikia hapa nilipo nakwambia kwa kujua...usione humu tunacheka na kuchangia mada hata za.. .

Hii ni moja ya tiba....Gf ndio rafiki yangu ...

daima angalia zaidi vile vitavyokupa furaha..

Taratibu utabadilika...ila usikate tamaa
ongea na nafsi yako kuwa unaweza kabisa kufanya kitu flani...na ufanye...

Usisahau kuchangamka na wadada...kama unawatania flani vile..jifunze kubembeleza..hata kwenye sim...

Kuna mtu namjua yeye alishindwa kuvuka hapa .....
matokeo kawa shoga..
wanambembeleza yeye..mabazazi!

Unaweza sana ..kila kitu..nakuona kabisa hapo ulipo... ...badili na mwendo huo dunda..... sio unyatie kama paka!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshindwa kwenda hospitali kubwa hasa muhimbili sababu wale ni gharama mno tena kuna daktari wa moja ya hospital nliyoenda alinambia kutoa ushauri tu/ kupewa ushauri ni lazima pesa itumike, hivyo nikienda huko lazima nijipange kweli kweli mfukoni.
umeshaulizia Gharama ya kumuona Dr. ni kiasi gani mkuu?
 
Kwa kweli ila kwa nguvu ya wanaJF wanaojali binadamu wenzao huyu israel kashindwa mno kikombe cha kifo nimekikwepa
Hongera sana mkuu kwa kuwa na mtazamo chanya. Mwanzo ulikuwa mbishi kinoma hukutaka hata kushaurika. BTW kuna movie moja inaitwa BEATS mule kuna jamaa anatatizo kama lako sijui kama niko sawa? Kama ni hivyo then jichanganye sana na watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NYONGEZA
Usitumie kabisa pombe ukiwa n stress mkuu.niliwahi kujaribu kipindi fulani nikiwa na msongo wa mawazo ndo nilizidisha matatizo hangover ni nuksi.
Matumizi ya smartphone
Hapa lazima uwe makini sana simu inaweza kukuletea stress kama hautaitumia vyema.
Uninstall FACEBOOK, INSTAGRAM hizi social media ni uchafu na zinaathiri brain especially ukiwa under depression (fake smile,fake life,fake reality) hakikisha una app hizi zitakutoa stress kabisa TWITTER (real time update),JF, QOURA (questions with answer), MEDIUM. ukiona hofu inakuja unafungua kati ya hizo apps utaoa hiyo hofu kupitia contents zake.
Mkuu hapo kwenye Apps inategemea na interest zake. Cha msingi sana aifundishe akili yake kukubali levels za kimaisha. Kwangu mimi naona Insta nirefleshment nzuri sana kwa sisi majobless. Kule Quora kunachosha ubongo, twitter nayo inawatu wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom