MREJESHO: Social anxiety, depression, panic attack vinanitesa, vinaniua taratibu

JERUSALEMA

Senior Member
May 14, 2018
153
500
Hello wanandugu,

Naona PM nyingi zikiulizia hali yangu kuhusiana na lile tatizo nililowahi kupost hapo mwanzo.

Socialphobia + anxiety + depression + panic attack inaniua taratibu! Msaada

Naomba niwajulishe kwa ujumla kuwa hali yangu kidogo nafuu tofauti na hapo mwanzo. Nilichukua baadhi ya ushauri nikaufanyia kazi kwa kuji-force maana mimi ni mzito kwenye kufanya maamuzi hivyo imenipa ahueni kiasi, hivyo uzima wangu hadi leo naamini ipo siku nitapona 100%. JamiiForums kuna watu wanajali sana na ningependa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa members kama Avriel Oscar Awards Gdd Technicians hawa nilifanikiwa kuwasiliana nao moja kwa moja kwa simu na kunipa ushauri ambao ulinipa imani sana guys you the best thank you sana kwa kuokoa maisha yangu.

Kitu ambacho bado napambana nacho hadi sasa ni anxiety iliyopitiliza yaani naweza kukaa mwenyewe nikiwaza kidogo basi mwili una-react na kuanza kutetemeka, nasikia kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda mbio, hofu kujaa, upungufu wa pumzi yaani nakua navuta hewa kwa shida. Nilienda hospitali wakagoma kunipa dawa wakaishia kunipa ushauri tu na pia nilijaribu kwenda kwenye maduka ya dawa karibia 6 wengi waligoma kunipa dawa za antidepressants hadi waione barua ya ruhusa kutoka kwa daktari ndo wangenipa.

Hivyo bado naendelea kupokea maoni nini cha kufanya ili hii hali iishe hata ikitokea nikafa basi niwe na cha kumwambia Muumba kuwa nilijitahidi kujitetea na kujipigania ila ikashindikana japo wapo baadhi ya watu wako walinisaidia kwa mawazo na nikayafanyia kazi.

Nawapenda wote ❤. Naendelea kupokea ushauri. Maombi yenu muhimu sana kwa afya yangu.
 

lulu za uru

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
1,038
2,000
Unajiita maiti halafu unaishi formula ya waliohai? Kuna nguvu ktkt hilo jina yaan kiroho hilo ni tatizo kabisa

..
Badili hili jina
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom