MREJESHO: Social anxiety, depression, panic attack vinanitesa, vinaniua taratibu

Hello wanandugu,

Naona PM nyingi zikiulizia hali yangu kuhusiana na lile tatizo nililowahi kupost hapo mwanzo.

Socialphobia + anxiety + depression + panic attack inaniua taratibu! Msaada

Naomba niwajulishe kwa ujumla kuwa hali yangu kidogo nafuu tofauti na hapo mwanzo. Nilichukua baadhi ya ushauri nikaufanyia kazi kwa kuji-force maana mimi ni mzito kwenye kufanya maamuzi hivyo imenipa ahueni kiasi, hivyo uzima wangu hadi leo naamini ipo siku nitapona 100%. JamiiForums kuna watu wanajali sana na ningependa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa members kama Avriel Oscar Awards Gdd Technicians hawa nilifanikiwa kuwasiliana nao moja kwa moja kwa simu na kunipa ushauri ambao ulinipa imani sana guys you the best thank you sana kwa kuokoa maisha yangu.

Kitu ambacho bado napambana nacho hadi sasa ni anxiety iliyopitiliza yaani naweza kukaa mwenyewe nikiwaza kidogo basi mwili una-react na kuanza kutetemeka, nasikia kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda mbio, hofu kujaa, upungufu wa pumzi yaani nakua navuta hewa kwa shida. Nilienda hospitali wakagoma kunipa dawa wakaishia kunipa ushauri tu na pia nilijaribu kwenda kwenye maduka ya dawa karibia 6 wengi waligoma kunipa dawa za antidepressants hadi waione barua ya ruhusa kutoka kwa daktari ndo wangenipa.

Hivyo bado naendelea kupokea maoni nini cha kufanya ili hii hali iishe hata ikitokea nikafa basi niwe na cha kumwambia Muumba kuwa nilijitahidi kujitetea na kujipigania ila ikashindikana japo wapo baadhi ya watu wako walinisaidia kwa mawazo na nikayafanyia kazi.

Nawapenda wote. Naendelea kupokea ushauri. Maombi yenu muhimu sana kwa afya yangu.

hongera kwa kupata nafuu...na hongera kwa wadau wote waliokuwa msaada kwako..jambo la msingi ilikuepukana na hiyo hali ni kujua ni kitu gani (driving forces) kinachokufanya uingie kwenye hiyo hali....hawezi kupona completely kama hautaweka wazi au kukubaliana na hali inayokupeleka huko ...

tafuta mwarobaini wa hayo mawazo kwa kushare na watu wako wa karibu au kama uliyemkosea yupo nenda kazungumze naye...kitaalamu wanasema kufungua moyo na kuyazungumza yale yakupayo hofu inakupa nguvu na amani ...

usipende kujitenga kama nyama za mishikaki..penda kujichanganya na wana ila kukupa usahaulifu wa yanokusibu ...also you have to watch what your eating...too much fat ujue kabisa itafika siku utazima kama mshumaa..

pole kwa changamoto...

OVAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Nimeshindwa kwenda hospitali kubwa hasa muhimbili sababu wale ni gharama mno tena kuna daktari wa moja ya hospital nliyoenda alinambia kutoa ushauri tu/ kupewa ushauri ni lazima pesa itumike, hivyo nikienda huko lazima nijipange kweli kweli mfukoni.
Una kadi ya bima ya afya? Nipe jibu
 
hongera kwa kupata nafuu...na hongera kwa wadau wote waliokuwa msaada kwako..jambo la msingi ilikuepukana na hiyo hali ni kujua ni kitu gani (driving forces) kinachokufanya uingie kwenye hiyo hali....hawezi kupona completely kama hautaweka wazi au kukubaliana na hali inayokupeleka huko ...

tafuta mwarobaini wa hayo mawazo kwa kushare na watu wako wa karibu au kama uliyemkosea yupo nenda kazungumze naye...kitaalamu wanasema kufungua moyo na kuyazungumza yale yakupayo hofu inakupa nguvu na amani ...

usipende kujitenga kama nyama za mishikaki..penda kujichanganya na wana ila kukupa usahaulifu wa yanokusibu ...also you have to watch what your eating...too much fat ujue kabisa itafika siku utazima kama mshumaa..

pole kwa changamoto...

OVAAAAAAAAAAAAAAAA

Asante sana mkuu, hiyo ya kujitenga ndo napambana nayo sana, kwa sasa najichanganya na watu inanisaidia kiasi.
 
Ningependa kufahamu uwepo na idadi ya washauri wa maswala ya saikolojia kwa hapa kwetu Tanzania ,je idadi yao inakidhi mahitaji ya watu katika jamii?

Kwangu mimi naona hili ni moja ya matatizo ambayo tunayo kwenye jamii yetu lakini nahisi haijachukuliwa serious kuwa huenda ikaleta madhara kwa afya ya mwanaadamu,kuanzia ngazi ya familia mpaka jamii yote nahisi hatujagundua mambo mengi kuhusu saikolojia ya watu/mtu katika familia mie kiukweli nasisitiza hili ni tatizo tujifunze kuzingatia haya mambo na kuacha kupuuzia jamani kauli yako moja ina impact kubwa sana kwa mtu mwenye uhitaji.

Kwa jamii za wenzetu nchi zilizoendelea hili tatizo limeratibiwa vizuri kabisa kwa kuweka washauri katika ngazi mbali mbali mpaka vituo maalum kwa ajili ya watu kupata huduma hii nadhani hata kwetu inawezekana, kuna muda mwanadamu unahitaji mtu wa kuongea nae kumpunguzia mzigo ulionao moyoni.

Kama wawakilishi wa jamii iliopo nje ya JF tuna nafasi ya kusaidia wenzetu japo kwa kuwapa muda wa kuwasikiliza yalio ndani a mioyo yao na kuwapa ushauri pia.

Hongera JERUSALEMA kwa kupiga hatua mungu akupe nguvu zaidi.
 
Ni kweli kabisa mkuu. Asante
 
Hello wanandugu,

Naona PM nyingi zikiulizia hali yangu kuhusiana na lile tatizo nililowahi kupost hapo mwanzo.

Socialphobia + anxiety + depression + panic attack inaniua taratibu! Msaada

Naomba niwajulishe kwa ujumla kuwa hali yangu kidogo nafuu tofauti na hapo mwanzo. Nilichukua baadhi ya ushauri nikaufanyia kazi kwa kuji-force maana mimi ni mzito kwenye kufanya maamuzi hivyo imenipa ahueni kiasi, hivyo uzima wangu hadi leo naamini ipo siku nitapona 100%. JamiiForums kuna watu wanajali sana na ningependa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa members kama Avriel Oscar Awards Gdd Technicians hawa nilifanikiwa kuwasiliana nao moja kwa moja kwa simu na kunipa ushauri ambao ulinipa imani sana guys you the best thank you sana kwa kuokoa maisha yangu.

Kitu ambacho bado napambana nacho hadi sasa ni anxiety iliyopitiliza yaani naweza kukaa mwenyewe nikiwaza kidogo basi mwili una-react na kuanza kutetemeka, nasikia kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda mbio, hofu kujaa, upungufu wa pumzi yaani nakua navuta hewa kwa shida. Nilienda hospitali wakagoma kunipa dawa wakaishia kunipa ushauri tu na pia nilijaribu kwenda kwenye maduka ya dawa karibia 6 wengi waligoma kunipa dawa za antidepressants hadi waione barua ya ruhusa kutoka kwa daktari ndo wangenipa.

Hivyo bado naendelea kupokea maoni nini cha kufanya ili hii hali iishe hata ikitokea nikafa basi niwe na cha kumwambia Muumba kuwa nilijitahidi kujitetea na kujipigania ila ikashindikana japo wapo baadhi ya watu wako walinisaidia kwa mawazo na nikayafanyia kazi.

Nawapenda wote. Naendelea kupokea ushauri. Maombi yenu muhimu sana kwa afya yangu.
Asante Mungu nafurahi kusikia hivi... Amini ushindi upo mbeleni. Nakuombea Baraka Uzima na Amani tele.
 
Back
Top Bottom