Mrejesho: Nimepata haki yangu hatimae

Raynavero

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
38,413
56,029
Habarini wana jamvi
Siku kadhaa zilizopita nilileta malalamiko humu kuhusiana na dhulma niliyofanyiwa na kutapeliwa ardhi yangu.

Naomba nilete feedback na kutoa shukrani kwa wote walionishauri, na kunipa mawazo chanya ya namna ya kupigania kile kidogo cha haki yangu nikakipata

Nashukuru sana mawazo yenu mengi yalikua mazuri na ktk hilo nikajikuta nampata mwanasheria wa ardhi ambae kwa kweli alinisimamia mpk nikapata haki yangu yote bila usumbufu.

Nawashukuru sana kwa sapoti yenu jf is my second home,watu humu wengine mmebarikiwa vipawa vya ushauri wa kila aina japo wengine wachache sana wanachukulia hapa km kijiweni.

Ahsanteni sana Mungu awe nanyi nyote na awaruzuku kila hiitaji lenu.
 
hiyo sehemu ni bora ungeiuza sisi binadamu hatukubali kushindwa kirahisi wala hatukubali kushindwa vyote

uza kisha nunua sehemu nyingine
 
Safi kabisa kwa kupata haki yako bila kuogopa.

Kuwa makini sasa wale ndugu watakua wana kinyongo na wewe,wakidhan umewaonea kumbe wao ndio wakorofi.
Ukiwa unadai haki yako usiangalie nani atachukia na nani atafurahi
Ilmradi uko kwenye haki, usipepese macho...wanadamu watakuchukia tu hata kama ukiwa unawagawia hela kila siku..watasema anatugawia hela inamaana ametuona sisi maskini sana
Kwaiyo ishi unavyotaka siyo wanavyotaka utakufa na presha
 
Safi sana. ni vema kuwa makini sasa mkuu, nduguzo watakuwa bado wana kinyongo na wewe, tena ikiwezekana uza hicho kiwanja ununue kingine...
 
Hongera G..

Ila hakikisha hiyo inakuwa haki rasmi ili lisiibuke lingine baadaye..

All the best
 
Hongera G
Wale ndugu hawakuchukuliwa hatua yoyote?
thank uu...nilimtafuta mwanasheria wa ardhi baada ya kuona hii ishu familia inaiogopa akawatumia barua ya Onyo wanapaswa kunilipa ndani ya siku 7 unless wanapeleksa mahakamani

Wakaomba sana wasipelekwe mahakamani Ila wakaambia watalipia gharama ya kesi na na wakaahidk watalipa ndani ya siku 14 kweli after 14 days wakalipa nusu baadae wakamalizia kiasi cha gharama zilizobaki
 
Back
Top Bottom