stubborn wa Njombe
Member
- Dec 8, 2016
- 79
- 170
Habari za wakati huu waungwana.
Nakumbuka week kadhaa nyuma niliomba msaada wenu kwa hali ninayoisikia katika mwili wangu.
Nilikuwa ninahisi maumivu sehemu za mbavu zote mbili pia nilikuwa sipati choo vizuri.
Nashukuru kwa wale walionishauri nikapime UKIMWI kwani nilipima pia nikaonekana negative ila nilipima vipimo vingi sana ikiwemo magonjwa mengine ya zinaa ingawa nayo pia hayakuonekana katika mwili wangu.
Ila ilikuja kugundulika nina typhoid tena imeshanishambulia sana. Nikaandikiwa dawa za hospital ambazo nilitakiwa nizitumie within 2 weeks. Ambazo ni ciprofloxacin nashukuru mungu mpaka leo hii ninavyoongea na nyinyi hali yangu imetengamaa.
Ila limeibuka tatizo la bawasili kwa kipindi kile ambacho nilikuwa sipati choo na ikitokea kupata choo basi napata choo kigumu sana so ikapelekea zile nyama zikatokeza njia ya haja kubwa.
Kiufupi kwa hili tatizo naogopa kwenda hospital kama mtu anajua tiba mbadala anisaidie ili niweze kutatua kwa sababu nasikia hospital hakuna jinsi zaidi ya upasuaji na inaweza ikarudi tena siku za usoni.
Waungwa kwa hekima zenu naomba na hili mnisaidie ushauri wenu ili niweze kurudi na kuendelea na maisha kama zamani