Mrejesho :Mapenzi yameurarua moyo wangu..

Namge

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
1,356
1,804
Wana janvi natumai mu wazima.. Na mnaendelea kugangamala na uchumi wa hapa kazi tu.. Ambao sio rafiki na mifuko yetu.

Dhumuni kubwa la uzi huu ni kutoa shukrani zangu za dhati kwa ushaur na ushirikiano katka wakat wote wa mpito wa maumivu ya mapenzi na kuvunjika kwa mahusiano..

1)Baada ya ushaur na maoni ya wana janvi pamoja na kuchanganya na zangu nikaona hamna zaidi ya kupiga chini uhusiano na kuanza upya. (kuanza upya si ujinga)

2)Shukrani za dhati kwa wana janvi ambao walikuja pm na kushauriana nao zaid na kunipa experience zao ambazo zilinijenga Sana na kunitia moyo.. Mbarikiwe Sana

3)Dada zangu wapendwa ambao mlisimama upande wangu na kuonyesha kuwa alichofanya mwanamke mwenzenu sio busara.. Kwakweli mlinitia nguvu kias kwamba. Nmemsamehe bure na wala sitabeba chuki dhidi ya jinsia ke (I believe Wanawake wazur na waaminifu bado wapo)

Na mwisho tuzid kuwa na moyo huu.. Na msichoke kushaur Wengine..
Na Mbarikiwe sana

Sina cha kuwalipa lakini mmekuwa faraja kubwa Sana
Nawapenda wana janvi wote wa jukwaa hili pendwa.
 
katika magonjwa hatari kupenda upo maana ukitendwa unatukana na kusema umeachana na mapenz BT ukipata mwingine full kusifia na kusahau yote ya zaman
 
Unachotakiwa kuzingatia ni kuwa furaha yako ndio jambo la msingi. Usikubali mtu akuondolee furaha yako lkn pia kumbuka anaependwa kwa dhati ni mke na sio mpenzi.
 
Unachotakiwa kuzingatia ni kuwa furaha yako ndio jambo la msingi. Usikubali mtu akuondolee furaha yako lkn pia kumbuka anaependwa kwa dhati ni mke na sio mpenzi.
Nmejifunza Mkuu.. I won't put so much expectations to anyone anymore.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom